Hatua ya Tanzania kurudisha mahusiano na Taifa la Israel.

sily

JF-Expert Member
Feb 20, 2013
926
577
Umofia kwenu wajumbe
Akihutubia wanajumuiya na wageni mbalimbali katika chuo kikuu cha Dsm kampasi ya Mlimani katika uzinduzi wa mabweni mapya ya wanafunzi,

Rais Dr.Magufuli amesema ameamua kuteua balozi na kurudisha mahusiano na Taifa la Israel, binafsi nampongeza Mh.Rais kwa hatua hiyo licha ya kusema kuwa anajua kuna watu ambao hawajapendezwa na maamuzi hayo na kwamba tayari ujumbe wa watalii wengi kutoka Israeli wameanza kuitembelea Tanzania kuja kujionea vivutio mbalimbali hvyo kutupatia fedha za kigeni.

Kuna watu fulanifulani wanachuki za kijinga juu ya Israel nawashauri waache.
 
Nadhani kwa sasa tunapaswa kuangalia wapi tutanufaika zaidi. Israel tunaweza nufaika katika suala la kilimo cha kisasa cha umwagiliaji, sayansi na teknolojia na pia kwenye tiba.
 
Binafsi nafrahia atua alioichukuwa,maana taifa la islael ni taifa lililo balikiwa duniani,so anae chukia AME laaniwa pia.
 
Nadhani kwa sasa tunapaswa kuangalia wapi tutanufaika zaidi. Israel tunaweza nufaika katika suala la kilimo cha kisasa cha umwagiliaji, sayansi na teknolojia na pia kwenye tiba.
Kabisa mkuu,kama serikali kupitia wizara ya kilimo wakitumia fursa hiyo vyema tutanufaika sana katka nyanja hiyo haswa kilimo cha umwagiliaji,kuhusu teknolojia hawa jamaa tunaweza kupata teknolojia nzuri na ya kisasa hususani ni kwenye majeshi yetu n.k
 
Umofia kwenu wajumbe
Akihutubia wanajumuiya na wageni mbalimbali katika chuo kikuu cha Dsm kampasi ya Mlimani katika uzinduzi wa mabweni mapya ya wanafunzi,Rais Dr.Magufuli amesema ameamua kuteua balozi na kurudisha mahusiano na Taifa la Israel,binafsi nampongeza Mh.Rais kwa hatua hiyo licha ya kusema kuwa anajua kuna watu ambao hawajapendezwa na maamuzi hayo na kwamba tayari ujumbe wa watalii wengi kutoka Israeli wameanza kuitembelea Tanzania kuja kujionea vivutio mbalimbali hvyo kutupatia fedha za kigeni.
Kuna watu fulanifulani wanachuki za kijinga juu ya Israel nawashauri waache.
Kwa hilo namuunga mkono rais wetu JP Magufuli. Kama kiongozi SI LAZIMA ufurahishe watu. Kwa sababu wakati mwingine ni LAZIMA uchukue MAAMUZI MAZITO bila kujali nani anapenda na nani hapendi.
Kama TAIFA tunaweza kupata FAIDA kubwa toka kwa Waisraeli. Nchi ya Senegal japo WAISLAM ni zaidi ya 90% walipogundua FAIDA ya UHUSIANO na Israeli iliamua KUSHIRIKIANA na Israeli katika ma,bo mbali mbali.
Na sasa wako MBALI kilimo nk.

Hongera kwa Rais Magufuli maana kuna KUBARIKIWA pia kama TAIFA.
Mimi ni Mkristo na katika kitabu kitakatifu Biblia inasema Zaburi 122:6 " ....Na WABARIKIWE wale WAKUPENDAO."Hivyo ni wakati sisi kama taifa TUBARIKIWE.

Hii haina maana huko ISRAELI WATU wote ni WAZURI bali ni kwa sababu ya BARAKA za baba Abraham alizoambiwa na Mungu. "YEYOTE yule, Iwe ni TAIFA, FAMILIA, nk atakayekupenda ABARIKIWE na Mungu."
Hii ndo sababu nchi ya MISRI chini ya rais SADAT ilipogundua hayo ikaamua KUITAMBUA ISRAELI kama TAIFA na KURUDISHA uhusiano wa KIBALOZI.

Alipoambiwa atakaye KUBARIKI ATABARIKIWA na takaye KULAANI ATALAMIWA. Kitabu cha Mwanzo/Genesis 12:1-3.
Kwa hivo kutembelewa na Waziri Mkuu wa zamani wa ISRAELI, Ehud Barak ni Baraka. Amekuja kama MWASHIRIO.

Hebu tuitumie nafasi hiii KUPATA WATALII wengi toka huko. Maana hawa hawaendagi hivi hivi na kwa nchi HIVI HIVI.
Na kulingana na mtazamo wangu hii ni INDIRECT ENDORSEMENT kwamba Tanzania ni nchi ya AMANI.
 
Back
Top Bottom