Hatua nne za kuizuia simu janja yako isikuzidi wewe ujanja

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yametuletea bidhaa na huduma bora kabisa kuwahi kutokea hapa duniani.

Chukua mfano wa simu janja (smartphone) na mtandao wa intaneti, vitu hivi viwili, vimeleta mapinduzi makubwa sana duniani, vimetengeneza mabilionea wengi mno na hata kurahisisha kila kitu kuliko kilivyokuwa awali.

Kwa kuwa na simu janja na kuunganishwa na intaneti, una uwezo wa kujifunza chochote ukiwa popote, una uwezo wa kuwasiliana na mtu yeyote popote alipo duniani na unaweza kuuza au kununua chochote ukiwa popote duniani.

Kifaa hiki kidogo kabisa kina uwezo mkubwa mno, uwezo wa kufanya mambo makubwa pale kinapotumiwa vizuri.

Lakini kama ilivyo, hakuna kizuri kisichokuwa na kasoro, na kitu chenye manufaa makubwa, huwa pia kina madhara makubwa watu wanapotumia bila ya kuwa na tahadhari.

smartphone-slave

Na hilo ndiyo linatokea kwenye mapinduzi haya makubwa tunayoyaishi sasa. Simu janja ambazo tunazisifia kwa kuweza kufanya mambo mengi, zimefika hatua ya kuwazidi ujanja wamiliki wake.

Unaweza kuamini hilo? Yaani wewe mwenyewe, ununue simu, lakini baada ya muda simu hiyo inakutawala wewe, badala ya wewe kuitawala.

Unaweza kusema kwamba simu janja yako haijakuzidi ujanja, lakini kabla hujakimbilia huko, hebu kwanza jibu maswali haya?

  1. Je unaweza kukaa siku nzima bila ya kuigusa simu janja yako? (tafiti zinaonesha kwa wastani mtumiaji wa simu janja anagusa simu yake zaidi ya mara 100)
  2. Je huwa unalala na simu yako kitandani au karibu na kitanda chako? (Tafiti zinaonesha zaidi ya asilimia 80 ya watumiaji wa simu janja wanalala nazo kitandani au karibu na kitanda)
  3. Je huwa inakuchukua muda gani tangu unapoamka mpaka kugusa simu janja yako? Ni kitu gani cha kwanza huwa unakigusa unapoamka asubuhi? (tafiti zinaonesha zaidi ya asilimia 90 ya watumiaji wa simu janja huwa wanagusa simu zao ndani ya dakika 15 baada ya kuamka, na wengi ndiyo kitu cha kwanza wanachogusa.)
  4. Je unaweza kuacha kupokea simu janja yako inapoita, au kuacha kujibu ujumbe ulioingia pale unapokuwa na kazi muhimu au mazungumzo muhimu? (tafiti zinaonesha watu wengi huwa hawawezi kujizuia kupokea simu au kujibu ujumbe, hata kama kuna kitu cha muhimu zaidi wanafanya.)
  5. Je simu janja yako imeshakuwa chanzo cha mgogoro baina yako na mwenza wako? (tafiti zinaonesha kwamba wanandoa wapo tayari kutokufanya mapenzi mwaka mzima kuliko kuacha kutumia simu janja, mahusiano mengi yamevunjika kutokana na simu janja.)
Kama upo upande wa tafiti kwenye maswali hayo matano hapo juu, basi simu janja yako imekuzidi ujanja. Na wala usijisikie vibaya, kwa sababu karibu kila mtu amezidiwa ujanja na simu janja.

Lengo ni kujua kwamba simu janja zetu zimetuzidi ujanja, na kisha kuchukua hatua sahihi ili turudishe uhuru wetu na tutawale simu zetu badala ya simu zetu kututawala sisi.

Nir Eyal mwandishi wa kitabu kinachoitwa Indistractable: how to control your attention and choose your life, kwa muda mrefu amekuwa akifuatilia na kutafiti jinsi ambavyo maisha yetu yametawaliwa na usumbufu unaotokana na vitu mbalimbali vinavyotuzunguka.

Kupitia kitabu chake, Nir ameonesha kwamba tatizo la usumbufu kwenye maisha yetu huwa linaanzia ndani yetu wenyewe. Na hivyo ameweza kutoa njia bora za kuondokana na usumbufu unaotuzuia kufanya makubwa na kufanikiwa zaidi.

Moja ya maeneo ambayo Nir ametufundisha jinsi ya kuyadhibiti yasiwe usumbufu kwetu ni kwenye simu janja (smartphone) zetu. kwenye kitabu chake cha INDISTRACTABLE, Nir ametushirikisha hatua nne za kuzuia simu janja yako isikuzidi wewe ujanja. Kwenye makala hii tunakwenda kujifunza hatua hizo nne, na kwenye makala ya TANO ZA JUMA tutapata uchambuzi wa kitabu hicho kwa kina na kujua jinsi ya kuwa na maisha tulivu yasiyo na usumbufu.

Zifuatazo ni hatua nne za kuizuia simu janja isikuzidi ujanja

MOJA: ONDOA

Hatua ya kwanza ya kuondoa usumbufu wa simu yako ni kuondoa app zote ambazo huzitumii mara kwa mara au hazina manufaa yoyote kwako.

Kuna tabia moja ambayo watumiaji wengi wa simu janja wanayo, mtu akisikia kuna app mpya imetoka anaiweka, akikutana na mwenzake ana app fulani na yeye anaweka.

Mwisho unajikuta una app nyingi kwenye simu yako, nyingi huzitumii na nyingine hazina manufaa kwako.

Kadiri unavyokuwa na app nyingi kwenye simu yako, ndivyo unavyokaribisha usumbufu kwako kupitia simu hiyo. Kwa sababu kila app huwa inaleta taarifa kunapokuwa na kitu kipya na hapo unajikuta ukigusa simu yako kila wakati.

Anza kwa kujiuliza ni app zipi kwenye simu yako zina manufaa kwako. Na kama ambavyo nimekuwa nashauri kwenye KISIMA CHA MAARIFA, weka vipaumbele vyako kwa kutumia mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA. Kama app haikufanyi uwe na afya bora, haikuingizii kipato na haikufanyi uwe na hekima zaidi, inakupotezea muda wako.

Unapaswa kuondoa app zote ambazo hazina matumizi au hazina manufaa kwako. Baki na zile chache ambazo zinaendana na mahitaji yako binafsi. Kumbuka umenunua simu janja iyafanye maisha yako kuwa rahisi, na siyo iwe sehemu ya kuweka kila kitu na kukaribisha kila usumbufu.

SOMA; Hivi Ndivyo Mitandao Ya Kijamii Imeharibu Akili Za Watu Wengi Na Hatua Tatu Za Kuchukua Ili Kunusuru Akili Yako Isiharibiwe.

MBILI: BADILI

Kuna app unaweza kuziacha kwenye simu yako kwa sababu zina manufaa fulani, lakini pia zina nafasi kubwa sana ya kukusumbua.

Kwa mfano YouTube, unaweza kujifunza mambo mengi na mazuri kwenye YouTube, lakini pia inapokuwa kwenye simu yako inarahisisha usumbufu, unapoangalia video moja unaletewa nyingine nyingi, mtu unayemfuatilia anapoweka video unaletewa taarifa. Sasa hii inaweza kuwa usumbufu kwako.

Njia sahihi ya kuchukua kwa app za aina hii ni kubadili matumizi yake, badala ya kuzitumia kwenye simu janja yako, chagua kuzitumia kwenye kompyuta. Hivyo unazifuta app hizo kwenye simu yako, na kila unapotaka kuzitumia unaenda kwenye kompyuta.

Kwa njia hii unaondokana na usumbufu ambao unakuwa karibu, unazitumia huduma hizo kwa muda ule tu ambao unaweza kuwa kwenye kompyuta. Hii itakufanya uwe na utulivu kwenye vitu vingine unavyokuwa unafanya.

Hivyo pia ndivyo unavyopaswa kufanya kwa mitandao ya kijamii. Mitandao mingi ya kijamii unayotumia kwa sasa haina tija yoyote kwako, kama unatumia mitandao ya kijamii zaidi ya miwili, na hakuna unachouza mtandaoni, unapoteza muda wako.

Unaweza kuchagua mtandao mmoja ambao unakuleta karibu na watu wako wa karibu, na kisha kuchagua kutumia mtandao huo kwa kompyuta tu. Usiweke app ya mtandao huo kwenye simu janja yako, kwa sababu utakuwa unakaribisha usumbufu kwako.

Unapokuwa na app za mitandao ya kijamii kwenye simu yako, kila ambacho marafiki zako wanafanya unapewa taarifa. Mtu kaweka picha unapewa taarifa, mtu kaweka maono kwenye picha yako unapewa taarifa. Sasa taarifa hizi zinapomiminika kila wakati, huwezi kuwa na utulivu kwenye kile unachofanya.

Badili kutumia app, kutoka kwenye simu na kwenda kwenye kompyuta, na kama huna kompyuta ndiyo vizuri zaidi, kwani itakubidi uende kwenye mkahawa au kuomba kompyuta ya mtu kwa ajili ya kuingia, hivyo unapunguza usumbufu zaidi.

TATU: PANGA UPYA

Baada ya kuondoa zile app ambazo hazina manufaa kwako, kubadili sehemu ya kuzitumia zile ambazo huwezi kuacha nazo kabisa, utakuwa umebaki na app chache kwenye simu janja yako.

Hatua inayofuata ni kupangilia upya simu yako ili kuondoa tamaa ya kuingia kwenye usumbufu pale unaposhika simu yako.

Kwenye kioo chako cha mbele cha simu yako, usijaze app nyingi, badala yake weka chache na za msingi pekee. Hii ni kwa sababu unapoweka app nyingi kwenye kioo chako cha mbele, kila unapoangalia simu yako, unashawishika kufungua app hizo na kuangalia. Mfano umetoa simu na unataka kuangalia saa, mara ukaona alama nyekundu kwenye app ya instagram, utajikuta umeshafungua na kuangalia nini kinaendelea.

Pangilia upya app kwenye simu yako, kwenye kioo cha mbele weka zile app ambazo ni muhimu kwako na unazitumia mara kwa mara. Mfano app unayotumia kusoma vitabu, kutafuta usafiri, kufuatilia kazi au biashara zako na mawasiliano na watu muhimu. Hata kama app za mitandao ya kijamii umeziacha kwenye simu yako kwa sababu yoyote ile, hakikisha hazikai kwenye kioo cha mbele.

Kadiri unavyopeleka usumbufu mbali na wewe, ndivyo unavyojizuia usisumbuliwe na app ambazo umeweka kwenye simu yako na hivyo kuweza kuishinda ujanja simu janja.

SOMA; Tano Za Juma Kutoka Kitabu; Digital Minimalism (Falsafa Bora Ya Matumizi Ya Teknolojia Itakayokuondoa Kwenye Utumwa Na Kukupa Uhuru.)

NNE: KATAA TAARIFA

Simu janja na mitandao ya kijamii imetengenezwa makusudi kukufanya wewe utumie kifaa na huduma hizo muda wote. Kwa sababu kadiri unavyotumia kwa muda mrefu ndivyo wamiliki wa mitandao hiyo ya kijamii wanavyonufaika.

Ili kuhakikisha unatumia kila mara, wamekuwa na njia ya kukupa taarifa ya kila kinachoendelea ili ufungue na kuangalia. Na hiki ndiyo kimekuwa chanzo kikubwa cha usumbufu kupitia simu janja. Umekaa unafanya kazi yako muhimu unasikia simu inatoa mlio au mtetemo, unajua kuna kitu cha maana kinaendelea, unafungua kuangalia unakuta umepewa taarifa kwamba rafiki yako ameweka maoni kwenye picha yako, unafungua kuona maoni hayo unakuta ameandika “umependeza sana”.

Fikiria hapo ulikuwa na kazi muhimu unaifanya, taarifa imekujia ukafikiri ni muhimu, ukaacha kazi yako, halafu unaenda kuangalia kumbe ni mtu anakuambia umependeza? Kuna uharaka gani wa wewe kuyasoma maoni hayo? Si unaweza kuja kuyaona tu baadaye ukiwa umeshamaliza kazi zako?

Ili kuondokana na usumbufu, ondoa kabisa mfumo wa kutumiwa taarifa na simu janja yako au mitandao na huduma nyingine unazotumia. Ingia kwenye mpangilio wa simu yako na sehemu ya Notification kisha zima kabisa zile app ambazo hutaki ziwe zinakuletea taarifa kuhusu yanayoendelea. Kuondoa kupokea taarifa haimaanishi hutaona, badala yake inaondoa ule usumbufu wa kukukatisha kwenye mambo muhimu. Unaweza kuja kuona baadaye utakapokuwa na muda.

Kwa kuondoa mfumo wa kupokea taarifa kwa kila kinachotokea, utapunguza sana usumbufu unaokutana nao sasa kwenye simu yako. Utaweza kuwa na utulivu kwenye kazi unayofanya na kuja kupitia yanayoendelea baadaye.

NYONGEZA: ONDOA USUMBUFU KABISA

Kuna hatua moja ya nyongeza na muhimu sana kwa wale ambao wapo makini na muda wao. Kwa wengi, hata baada ya kuchukua hatua hizo nne, kuna vitu vitawasumbua, labda ni simu zinazoingia ambazo siyo zote zenye umuhimu au ujumbe unaoingia.

Kwa watu kama hawa, hawawezi kuzima simu kwa sababu labda kuna simu muhimu wanataka wazipate, labda kutoka kwa familia, au bosi au wafanyabiashara wengine. Hivyo wengi hujikuta wanajiambia inabidi wawe karibu na simu kwa sababu kuna watu muhimu ambao wanapowapigia lazima wawe wanapatikana, lakini hilo linapelekea kukaribisha usumbufu wa wengine ambao hawana umuhimu.

Katika hali kama hiyo, simu janja yako ina kitu kinaitwa DO NOT DISTURB. Ingia kwenye sehemu ya mpangilio wa simu yako (setting) kisha utaona hiyo. Unapowasha hiyo, hakuna simu wala ujumbe wala chochote kitakachokusumbua kwa muda ambao hutaki usumbufu. Lakini uzuri wa huduma hiyo ni kwamba unaweza kuchagua namba ambazo zikipiga simu au kutuma ujumbe basi utapata mlio au mtetemo, kwa namba nyingine zote, hutasikia kabisa, utakuja tu kuona baadaye kama mtu alipiga au alituma ujumbe.

Mimi binafsi nimekuwa natumia huduma hii ya DO NOT DISTURB na imekuwa inanipa utulivu mkubwa sana wakati ambao nasoma au naandika. Najua kabisa hakuna simu au ujumbe utakaonisumbua na kama simu au ujumbe umeleta mlio basi najua ni wa mtu muhimu na hivyo kuchukua hatua.

Rafiki, hizo ndizo hatua nne na moja ya ziada ambazo ukizichukua utaweza kuizidi ujanja simu janja yako na kuacha kuwa mtumwa wa simu yako.

Karibu kwenye makala ya TANO ZA JUMA hili la 46 la mwaka 2019 ambapo tutajifunza kwa kina jinsi ya kuondokana na usumbufu wa vifaa tunavyomiliki. Nir ametushirikisha maeneo manne muhimu ya kukabiliana na usumbufu, moja ni kudhibiti vichocheo vya ndani, mbili ni kutenga muda wa kuwa tulivu, tatu ni kudhibiti vichocheo vya nje na nne ni kuondokana na usumbufu kwa kutumia mbinu bora kabisa.

Tano za juma hili siyo za kukosa, kwa sababu watengenezaji wa simu janja na wamiliki wa mitandao ya kijamii wanatumia mabilioni ya dola kuhakikisha wewe unakuwa mtumwa kwenye huduma zao, usikubali kabisa kuwa hivyo, soma uchambuzi wa kitabu cha INDISTRACTABLE na utaweza kurudisha uhuru wako.

TANO ZA JUMA zinapatikana kwenye channel ya telegramu pekee, kuzipata, karibu ujiunge na channel hiyo. Maelezo ya kujiunga yako hapo chini, soma na chukua hatua sasa ili uweze kupata maarifa mengi.

PATA KITABU NA UCHAMBUZI ZAIDI

Rafiki yangu mpendwa, kama ungependa kupata kitabu tulichochambua kwenye makala hii ya tano za juma, pamoja na kupata uchambuzi wa mafunzo zaidi kutoka kwenye kitabu hiki, karibu ujiunge na channel ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA.

Hii ni channel ambayo ipo kwenye mtandao wa TELEGRAM MESSENGER, ambapo kila juma nakutumia kitabu cha juma, uchambuzi huu na mafunzo ya ziada yote kwa mfumo wa pdf ambapo utaweza kusoma na hata kuhifadhi vizuri kwa matumizi ya baadaye. Pia kwa kujiunga na channel hii, utaweza kupata mafunzo yote ya nyuma na hata ukipoteza mafunzo hayo utaweza kuyapakua tena muda wowote unapoyataka.

Ada ya kujiunga na channel hii ni ndogo mno, ni shilingi elfu moja tu kwa wiki. Au unaweza kuchagua kulipa kwa mwezi (elfu 3) au kwa mwaka (elfu 30). Lakini wiki ya kwanza ni bure na hulipi chochote. Karibu ujiunge leo bure kwa kutuma ujumbe kwa njia ya telegram kwenda namba 0717396253. Ujumbe uwe na maneno TANO ZA MAJUMA YA MWAKA.

Makala hii imeandikwa na Kocha Dr Makirita Amani.

Dr. Makirita ni Daktari wa binadamu, Kocha wa mafanikio, Mwandishi na Mjasiriamali.

Dr. Makirita anaendesha mafunzo ya mafanikio kwa wale waliojitoa hasa kufanikiwa kupitia program ya KISIMA CHA MAARIFA.

Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma sasa ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa njia ya wasap namba 0717 396 253 (tumia wasap tu)
 
Ahsante mkuu
 
Nitarudi Kuipitia..
 
Back
Top Bottom