Hatua nne za kijasusi zinazoweza kumfanya mtu anuse hatari haraka

Western movies zinakuwa na ujumbe mzito sana. Kuna uzi mmoja unaitwa sijuhi kula tunda kimasihara baada ya kukutana na ule uzi na kusoma comments zote, nilichogundua watoto wa kike wanaliwa through intelligence techniques tena za hali juu, ipo siku ntakujaga kuleta thread yake, mbinu za kijasusi zinazotumiwa na wanaume kula tunda kimasihara.
Duh kwahiyo wala matunda kimasihara ni majasusi eeh?? Pongez kwetu tafadhali
 
Kwanza niseme mimi ni mfuatiliaji sana wa hili jukwaa na limenifunza mengi pia, leo na mimi nimeona niwape mbinu kadhaa za kukabiliana na hatari inayoweza kutokea.

Katika ujasusi kuna hii mbinu inaitwa important colours(cooper color codes), ambayo utumiwa na majasusi duniani kunusa na kuzikwepa hatari zinazoweza kuwakuta kwahiyo sio mbaya kuzijua pengine siku moja zitakusaidia.

Hatua nne zinazoweza kumfanya mtu anuse hatari haraka inayoweza kutokea ni hizi hapa zifuatazo;

CONDITION WHITE
Katika ujasusi ukisikia mtu anaambiwa yupo katika condition white, maana yake ni amekaa kaa tu na hawazi jambo gani la hatari linaweza kutokea muda na wakati huo kulingana na mazingira aliopo. Mfano,unamukuta mtu anachart au anaongea na simu huku anavuka barabara, mtu anasinzia kwenye bus akiwa anasafiri muda wote, mtu yuko bar lakini muda wote yuko bize na simu yake, katika hali kama hizo hawezi kuwaza ni Jambo gani la hatari linaweza kutokea, maana yake anakuwa unprepared and totally unaware.

CONDITION YELLOW
Katika hatua hii ni hauoni kama kuna jambo au tukio linaweza kutokea, Ila unakaa na tahadhari na unakuwa unakusanya taarifa kuhusu kitu gani kinaendelea kwa wakati huo kulingana na mazingira uliopo, maana yake unakuwa in relaxed alert. Mfano, unaweza kuwa umekaa kwenye gari unasafiri na unaona hakuna dalili zozote za hatari, ila wewe kama wewe unakuwa unachukua tahadhari kwa mazingira yote mule ndani ya gari bila kujali tukio la hatari linaweza kutokea au lah na katika hatua hii mara nyingi ndo mtu unaweza kunusa hatari inayoweza kutokea na maamuzi ya kuchukua kwa haraka zaidi.

CONDITION ORANGE
katika hatua hii mtu anakuwa na tahadhari maalumu , kwa maana ya kwamba anatambua hatari inayotokea au inayoweza kutokea kwa wakati huo na anajiandaa jinsi ya kukabiliana nayo, kwahiyo ni tunasema a state in which there's a specific alert. Mfano, mtu anatembea sehemu ya watu wengi kama kariakoo, sasa katika pita pita yake kuna sehemu amefika anaona ni crowded, hivyo ananusa hatari labda ya kuweza kuibiwa simu, pesa, au kupigwa roba , kwahiyo kutokana na mazingira hayo anaamua kuchukua uelekeo mwingine au kubadili njia.

CONDITION RED
Katika hatua hii ni pale sasa mtu anajiandaa kiakili ama apambane au aikimbie hatari, katika ujasusi unaambiwa unapokuwa katika condition red inakupasa kuwa na ufanisi wa hali juu muno kuishinda hatari inayotokea au inayotaka kutokea ,hivyo inashauriwa ili kunusa vizuri hatari na kuzikwepa ni vyema kukaa katika condition orange.Mfano, mtu anatembea vichochoroni kwenye giza usiku then ananusa kwamba anaweza kupigwa roba na vibaka, ila kwakujiamini sasa ya kwamba atapambana nao kwa nguvu, kumbe adui wana silaha nzito kumuzidi kwahiyo anajikuta ameingia kumi na nane zao na amepoteza pambano ,ambapo angekimbia au kubadilisha uelekeo ingekuwa na manufaa Zaidi kwake.

Ukiweza kuzielewa hatua hizo, itakusaidia kunusa hatari nyingi na kuweza kuzikwepa.
Darasa zuri mkuu
 
Kibongo bongo ukiangalia kwa umakini bar, barabarani, kwenye vyombo vya usafiri wengi mnoo wanaji'condition in white.. na nadhani kwa7 nchi yetu ipo salama kiasi cha kutosha, ila kuna maeneo ukitembelea lazima unajikuta unaingia kwenye orange na yellow bila kupenda.....
 
Asante kwa darasa mdau! Wabongo wengi wapo condition white, yaani mtu anasafiri toka Dar es salaam mpaka Mwanza amelala tu au anatumia simu/muziki muda wote hawezi kujua hatari ya mazingira yaliomzunguka wakati huo ili kuchukua tahadhari.
Ni vema unaposafiri kuwa mdadisi pembeni yuko nani na nyuma yuko nani au mtu anaingia na mzigo gani au mtu anaeweka mzigo wako pembeni ni mzigo gani?
Mfano1. Nilikuwa safarini kuna mtu alikuwa na dalili za Covid-19 anatumia dawa za kisasa na za kienyeji wakati wa safari na alikuwa homa kali na anakohoa mwanzo wa safari hadi mwisho wa safari baada ya kuongea nae aliniambia ana Covid-19 lakini hakuna abiria alieweza kuhisi au kuchukua taadhari ya kuvaa barakoa au kutumia sanitizer japo yupo pembeni yao muda wote wa safari, watu(abiria) wako busy na simu,wamelala au wanaangalia television.

Mfano 2. Nilikuwa nasafiri wakati gari limefika Dodoma wakati wa chakula niliwai kurudi ila ghafla niliona mtu hatukuwa tunasafari nae ila aliingia kwenye basi na kuweka Tablet(simu) kwenye eneo la kiti la kuifadhia vitu kama maji au biskuti. Yule abiria mwenye kiti aliporudi akusumbuka kukagua pale alipokaa ila baada ya basi kuondoka nikamwambia kuna mtu ameweka Tablet kwenye sehemu yako je unamjua? Jamaa akahamaki kuwa siyo mmiliki wa hiyo simu na wala hana mahusiano na mtu alieiweka Tablet kwenye kiti chake.

Kwa picha iyo lazima ujiulize Je kwa nini kaweka simu kwenye kile kiti, lengo lake ni nini, je alijua kuwa Tablet(simu) inafutilia akaamua kuiweka kwenye kiti hicho ili wale waliokuwa wanamtafuta wapoteze uelekeo wake? Je wanaomtafuta ni kina nani Polisi/Wasiojulikana na jeje wanamtafuta kwa jambo gani? Je wakabaini simu wanayoifuatilia ipo kwenye kiti chako watakufanya nini?

Tuwe makini/wadadisi tunaposafiri ili kuepukana na majanga yanayoweza kuepukika.
 
Kwanza niseme mimi ni mfuatiliaji sana wa hili jukwaa na limenifunza mengi pia, leo na mimi nimeona niwape mbinu kadhaa za kukabiliana na hatari inayoweza kutokea.

Katika ujasusi kuna hii mbinu inaitwa important colours(cooper color codes), ambayo utumiwa na majasusi duniani kunusa na kuzikwepa hatari zinazoweza kuwakuta kwahiyo sio mbaya kuzijua pengine siku moja zitakusaidia.

Hatua nne zinazoweza kumfanya mtu anuse hatari haraka inayoweza kutokea ni hizi hapa zifuatazo;

CONDITION WHITE
Katika ujasusi ukisikia mtu anaambiwa yupo katika condition white, maana yake ni amekaa kaa tu na hawazi jambo gani la hatari linaweza kutokea muda na wakati huo kulingana na mazingira aliopo. Mfano,unamukuta mtu anachart au anaongea na simu huku anavuka barabara, mtu anasinzia kwenye bus akiwa anasafiri muda wote, mtu yuko bar lakini muda wote yuko bize na simu yake, katika hali kama hizo hawezi kuwaza ni Jambo gani la hatari linaweza kutokea, maana yake anakuwa unprepared and totally unaware.

CONDITION YELLOW
Katika hatua hii ni hauoni kama kuna jambo au tukio linaweza kutokea, Ila unakaa na tahadhari na unakuwa unakusanya taarifa kuhusu kitu gani kinaendelea kwa wakati huo kulingana na mazingira uliopo, maana yake unakuwa in relaxed alert. Mfano, unaweza kuwa umekaa kwenye gari unasafiri na unaona hakuna dalili zozote za hatari, ila wewe kama wewe unakuwa unachukua tahadhari kwa mazingira yote mule ndani ya gari bila kujali tukio la hatari linaweza kutokea au lah na katika hatua hii mara nyingi ndo mtu unaweza kunusa hatari inayoweza kutokea na maamuzi ya kuchukua kwa haraka zaidi.

CONDITION ORANGE
katika hatua hii mtu anakuwa na tahadhari maalumu , kwa maana ya kwamba anatambua hatari inayotokea au inayoweza kutokea kwa wakati huo na anajiandaa jinsi ya kukabiliana nayo, kwahiyo ni tunasema a state in which there's a specific alert. Mfano, mtu anatembea sehemu ya watu wengi kama kariakoo, sasa katika pita pita yake kuna sehemu amefika anaona ni crowded, hivyo ananusa hatari labda ya kuweza kuibiwa simu, pesa, au kupigwa roba , kwahiyo kutokana na mazingira hayo anaamua kuchukua uelekeo mwingine au kubadili njia.

CONDITION RED
Katika hatua hii ni pale sasa mtu anajiandaa kiakili ama apambane au aikimbie hatari, katika ujasusi unaambiwa unapokuwa katika condition red inakupasa kuwa na ufanisi wa hali juu muno kuishinda hatari inayotokea au inayotaka kutokea ,hivyo inashauriwa ili kunusa vizuri hatari na kuzikwepa ni vyema kukaa katika condition orange.Mfano, mtu anatembea vichochoroni kwenye giza usiku then ananusa kwamba anaweza kupigwa roba na vibaka, ila kwakujiamini sasa ya kwamba atapambana nao kwa nguvu, kumbe adui wana silaha nzito kumuzidi kwahiyo anajikuta ameingia kumi na nane zao na amepoteza pambano ,ambapo angekimbia au kubadilisha uelekeo ingekuwa na manufaa Zaidi kwake.

Ukiweza kuzielewa hatua hizo, itakusaidia kunusa hatari nyingi na kuweza kuzikwepa.
Somo zuri sana 🤭
 
"SPY SECRETS THAT CAN SAVE YOUR LIFE" by Jason Hanson.

Tafuta hicho kitabu kimeelezea mengi sana, ikiwemo aliyoyatoa mtoa mada.

Tupende kusoma vitabu wadau.
Naambatanisha kitabu...
Usomaji mwema.
 
Attachments

  • Spy Secrets That Can Save Your Life A Former CIA Officer Reveals Safety and Survival Technique...pdf
    1 MB · Views: 33
Back
Top Bottom