Zero One Two
JF-Expert Member
- Sep 16, 2007
- 9,347
- 3,011
Wakuu heshima mbele.
Admin sijui hii utaiweka wapi,lakini ninapata maswali mengi kuzidi majibu kutokana na report ya kamati teule ya bunge ambayo pamoja na hoja na mapendekezo yake yaliyojiri ishirini na tatu,ililishauri bunge hatua za kuchukuliwa dhidi ya wote waliotajwa kuhusika na kashfa nzima ya Richmond.
Kama nilimuelewa vizuri waziri mkuu,ndugu Pinda,aliahidi kushughulikia mapendekezo yote ndani ya report ile baada ya uchunguzi wa pili wa serikali.
Tume ilikwishachunguza na kutoa mapendekezo ni kwa nini serikali nayo kwa upande wake ifanye uchunguzi?Na ni kwa hadidu rejea zipi?
Kwa maoni yangu sioni kama kuna haja ya kuendelea na mjadala wa richmond ifikapo kikao kijacho cha Bunge hapo april,badala yake watuhumiwa wote wafikishwe mahakamani kwa ushahidi ambao umetolewa na kamati teule ya bunge.
Ikumbukwe pia wote waliohusika hawakuwa na hoja ya kujitetea ndani ya bunge ili kujinasua na tuhuma za ufisadi.
Kumcheleweshea mtu hukumu dhidi dhidi ya TUHUMA ni kumnyima haki yake.
Kitendo chao kujiuzulu huku wakiwa wamelisababishia taifa hasara kubwa kiende sawa na kushitakiwa mahakamani ikiwa ni pamoja na kurejesha pesa zote za walipa kodi zilizopotea.
Haiingii akilini kuwa unalipa pesa kila siku iendayo kwa mungu kwa kampuni hewa halafu ukaendelea kuwa huru ukifurahia ujambazi ulioufanya.
Kitendo cha Richmond kuwa kampuni hewa ni sababu tosha kuwatia hatiani kwa kutumia jasho la walipa kodi kujinufaisha kwa mamilioni kila siku.
Safari hii tunataka tujue mwenendo wa kesi zao,tofauti na tulivyozoea kuona watuhumiwa wanafikishwa mahakamani halafu basi hakuna kinachoendelea,na mara nyingine unawakuta wakiwa huru wanaendesha miradi yao ya biashara ya ASALI!
Kwa kuanzia freeze accounts zao kuanzia Richmond na EPA then mahakama iwe suluhisho.
Kinyume na hapo,wabunge na sisi tuwe kitu kimoja ili sauti zetu zisikike.
Naomba kuwakilisha.