Hatma ya wabunge waliokataa agizo la CHADEMA la kutohudhuria bungeni

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
.

By Sangu Joseph
.
Nimewaza sana juu ya kinachoendelea ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, hasa ule uamuzi wa baadhi ya Wabunge wake Lijualikali, Silinde, Jafary kuamua kukiuka maagizo ya chama chao kuna baadhi ya mambo ambayo mimi nimeyahisi yanaweza kutokea.

Kwanza Wabunge ambao wamekiuka maamuzi ya chama chao nimeona lengo la kwanza Kwa nyakati kama hizi ni kupaa kisiasa hasa ukiangalia huu ni muda wa nyongeza so hiki walichokifanya kinawafanya kuaminika kwa wapinzani wa chama chao.

Cha pili ambacho nimekigundua hapa, Wabunge waliopinga agizo la chama chao, inaonesha mwisho wa safari ndani ya CHADEMA na wanaenda kutafuta maisha kwengine hasa kwa Wapinzani wa chama wakiwemo NCCR - Mageuzi, CCM, ACT - Wazalendo.

Cha tatu ukiangalia kwa idadi ya Wabunge ambao walibaki ndani ya Bunge unagundua uamuzi wao unafanana au kuungwa mkono na Wabunge baadhi ya Wabunge ambao walibainisha uamuzi wa kujiunga NCCR kama Selasini, Komu so unaweza ukahisi NCCR ina uhakika wa Wabunge wengine watatu wa majimbo Lijualikali, Silinde, Jafary Michael, na Wabunge wa Viti maalum wanaweza kusimamishwa kwenye maimbo ya CHADEMA kwa hiyo Approximation unaweza ukahisi NCCR tayari inawatangaza nia zaidi ya Wabunge 10 kwenye uchaguzi ujao ( Ni mawazo yangu si uhalisia)

Chatatu unaweza kusema kwanini wasiende CCM kiukweli ninavyoona Mimi kwa time hii ndani ya CCM wameshachelewa kwa sababu kuna watu walishajipanga kuwakabili tena kwenye uchaguzi wa 2025 so mimi ninavyodhani ni ngumu sana kwao kwenda japo lolote linawezekana, dakika moja ya siasa ni sawa na mwaka mzima

Channe hatua hii inaonesha kuna baadhi ya Wabunge hawakubaliani na msimamo wa chama chao, na hatari kubwa inakuja pale chama wanapohitaji kupanga mipango ya Siri ni rahisi mno kuvuja kwa wapinzani wao.

Chatano : Huu ulikua mtego kwa upande wao Wabunge waheshimu chama, au wananchi waliowachagua kama mimi binafsi Sangu Joseph ningeungana na wananchi kwa sababu wao ndiyo wamenipa hiyo nafasi na kama chama kikinipiga chini naweza kugombea kwa chama kingine, na nikakisema vibaya chama kilichonipiga chini.
.
*Insta : FB : TWIT : SanguJoseph*
.
#MaoniYangu #KijanaMzalendo #IloveTZ

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengi wa wabunge wa Chadema walioasi watapoteza imani kwa wananchi na hawatapata nafasi 2020. Wamepata mahali pa kuonesha nia yao ya kuendelea au kutoka Chadema kwani wabunge wengi wanatafuta tu maslahi yao wakiona kwamba uwezekano wa kushinda ni mdogo basi wanahamia kwingine. Lakini wanatake risk kubwa kwani chochote chaweza kutokea uchaguzi ujao.
 
Salama yao waende ccm ambako obvious wakishiriki kura za maoni za ubunge watashindwa lakini possibility ya kupata uteuzi ni kubwa.
 
Mtazamo wangu naona kuna kila jitihada zinafanywa kuipandisha Nccr mageuzi na kuifukia Chadema. Hii ni kwa sababu tayari Cdm ilishaanza kuwa tishio na ndani ya Ccm watu wameshajaa hivyo ili kuondoa upinzani wa Cdm kinainuliwa chama kingine kijanja na kupewa watu kutoka Cdm
 
Inafikirisha
IMG_20200411_153631.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtazamo wangu naona kuna kila jitihada zinafanywa kuipandisha Nccr mageuzi na kuifukia Chadema. Hii ni kwa sababu tayari Cdm ilishaanza kuwa tishio na ndani ya Ccm watu wameshajaa hivyo ili kuondoa upinzani wa Cdm kinainuliwa chama kingine kijanja na kupewa watu kutoka Cdm
Maana yake Nccr ni CCM B

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom