Hatma ya Jairo, Luhanjo mkononi mwa Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatma ya Jairo, Luhanjo mkononi mwa Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 8, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,818
  Likes Received: 83,216
  Trophy Points: 280
  [h=3]Hatma ya Jairo, Luhanjo mkononi mwa Pinda [/h]

  Na Mwandishi Wetu
  *Bunge lasema limemaliza linasubiri maamuzi ya serikali
  *Wanasheria: Wabunge walikosea njia kuandaa taarifa ya kamati
  Majira

  SIKU 15 baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuazimia serikali kuwachukulia hatua za kinidhamu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo,
  Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo huku Mkaguzi na Mdhibiti na Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick Utoh, pia akituhumiwa kwa kushindwa kufanya kazi yake, hatma ya viongozi hao sasa ipo mkononi mwa Waziri Mkuu Mizengo pinda.

  Bw. Jairo anadaiwa kuchangisha fedha kinyume cha sheria kwa ajili ya kuwezesha kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo kinyume cha taratibu huku Bw. Luhanjo akidaiwa kumkingia kifua kiongozi huyo kwa kutoa hukumu bila kuhusisha Bunge lililoibua suala hilo.

  Bw. Utoh anadaiwa na bunge kushindwa kazi yake kwa kutoa taarifa inayodaiwa kumsafisha Bw. Jairo kinyume na hali halisi.

  Vyanzo vya habari ndani ya serikali vilieleza Majira kuwa tayari Ofisi ya Bunge imewasilisha taarifa za azimio la Bunge serikalini kwa Waziri Mkuu kama msimamizi wa shughuli za serikali ndani ya bunge na mtekelezaji wa shughuli za kila siku za serikali.

  "Hivi sasa hatma ya akina Jairo na Luhanjo pamoja na Ngelenja zipo mkononi mwa Pinda, tayari amepewa taarifa ya azimio la Bunge tangu wiki iliyopita, "kilisema chanzo chetu ndani ya serikali.

  Akizungumza na Majira Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililla, alikiri Ofisi ya Bunge kuwasilisha taarifa hiyo serikalini na kuongeza kuwa kwa kawaida huchukua muda wa saa 72 tu kuwasilisha Azimio la Bunge serikalini kama hakuna tatizo lolote.

  "Ni kweli ofisi ya bunge imewasilisha taarifa ya azimio la bunge serikalini, kwa kawaida sisi tunawasilisha taarifa kama hiyo ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye ndiye Mkuu wa shughuli za serikali ndani ya Bunge," alisema Dkt. Kashililla na kuongeza.

  Kwa kawaida tunachukua saa 72 tu kuwalisilisha azimio la bunge serikalini baada ya bunge kuahirishwa, sisi kama bunge tumemaliza kazi yetu labda tusubiri tu maamuzi ya serikali," alisema.

  Majira lilipofika ofisi ya Waziri Mkuu kuomba ufafanuzi wa suala hilo lilijibiwa kuwa Bw. Pinda yupo katika ziara za kikazi nje ya Mkoa.

  Majira ilipofika ofisi ya Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge Bw. William Lukuvi, ambaye kwa kawaida hupokea ripoti hizo kabla ya kumfikia Waziri Mkuu naye hakuwepo ofisini.

  "Mheshimiwa Waziri hayupo tangu wiki iliyopita, alikuwa kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI, hajafika ofisini bado, huenda atafika kesho (leo), yeye ndiye anaweza kusema lolote juu ya suala hilo, vuta subira," alisema mmoja wa wasaidizi wa waziri huyo.

  Hata hivyo baadhi ya wanasheria waliozungumza na Majira kuhusu suala hilo walidai kuwa baada ya kupitia taarifa ya Bunge walibaini kuwa chombo hicho kilikosea baadhi ya vipengele vya taarifa ya Kamati Teule iliyochunguza suala hilo hivyo kuonesha wasiwasi iwapo serikali itachukulia hatua stahili kama ilivyoshauriwa dhidi ya wahusika.

  Awali akiwasilisha taarifa ya uchunguzi juu ya sakata hilo la kuchangisha fedha kinyume na taratibu, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Bw. Ramo Makani (CCM) alisema kutokana na utaratibu huo ni vyema Bunge likaendelea kukemea kwa nguvu zote utaratibu wa uchangishaji wa fedha uliofanywa na wizara hiyo.

  "Kamati teule inapendekeza kwamba serikali ichukue hatua za kinidhamu kwa ndugu David Kitundu Jairo, kwa matumizi mabaya ya madaraka, kukusanya na kutumia fedha za serikali kinyume cha sheria, kanuni na taratibu za umma na kuruhusu matumizi mabaya ya fedha za umma," alisema.

  Mbali na hatua hizo kwa Bw. Jairo pia kamati hiyo imependekeza watumishi wote wa wizara hiyo ambao waliainishwa katika taarifa yao wachukuliwe hatua za kisheria.

  "Aidha, kwa kuwa waziri kwa mujibu wa mwongozo wa Baraza la Mawaziri ndiye msimamizi mkuu wa wizara, hivyo suala la uchangishaji halikupaswa kufanyika bila yeye kufahamu, kamati Teule inapendekeza serikali ichukue hatua zinazofaa kwa Waziri wa Nishati na Madini, mheshimiwa William Ngeleja ambaye ni mbunge," alisema Bw. Makani.

  Alisema kamati yake ilisitisha na jinsi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG),Bw. Ludovick Utoh kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake kikamilifu.

  "Hususan katika kulisaidia Bunge na umma kwa ujumla, Kamati teule inapendekeza serikali ichukue hatua zinazofaa kwa CAG kwa upotoshaji huo," alisema Bw. Makani.

  Katika hatua nyingine kamati hiyo ilipendekeza Katibu Mkuu Kiongozi, Bw. Phileom Luhanjo achukuliwe hatua zinazofaa na serikali.

  "Katibu Mkuu kiongozi kwa makusudi aliamua kumsafisha ndugu David Kitundu Jairo kwa kufisha ukweli wa taarifa ya ukaguzi maalumu uliofanywa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali na kuamua kwamba ndugu Kitundu Jairo hakuwa na kosa la kinidhamu,kitendo
   
 2. B

  BMT JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  jaman hvi bado hawajachukuliwa hatua?na bado wamekalia ofisi za serkal,ama kwel hii serkal ya jk ****** wa msoga ni dhaifu,tmechoka hatuwataki kwnye ofis za umma waondoke,nmeandika kwa maskitko na hacra
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,818
  Likes Received: 83,216
  Trophy Points: 280
  Serikali taahira hii, hawa hawatafanywa lolote lile wataendelea kupeta tu. Si unamuona Jemadari mzima eti kuhusu posho mpya za Wabunge kasusa kusaini!!! Sasa sijui Rais akisusa nani anayetakiwa afanye maamuzi magumu nchini. Kama hakubaliani na posho mpya basi asimame na kutwambia Watanzania posho hizi sikubaliani nazo kwa hiyo Wabunge wataendelea kulipwa posho zilizoamuliwa mwanzoni, lakini eti kaamua kususa!!!! Dah!!!! Halafu anajiita Kiongozi wa nchi!!!! Hivi Watanzania walimpa huu wadhifa mzito ili awe ana susa susa au kuingia mitini kila kunapotakiwa kufanywe maamuzi mazito kuhusiana na nchi yetu!!!? Urais si lelema na kususasusa!!!!

   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kila kitu huwa kinafanyika kupitia baraza la mawaziri. Pinda anajua kila kilichotokea, na tayari alisaini mgao wa pesa zile. Lilipo ibuka, kama alivyo ndugu yake J.K., akajifanya kuumizwa na kitendo kile na akajitapa kama angekuwa na uwezo, angechukua maamuzi palepale. USANII TU.

  Hataoweza kufanya kitu chochote, kwa mjibu wa taarifa za malipo zilizopo, yeye mwenyee ni mtuhumiwa kwani tayari alikula mlungula huo
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Lakini inakuaje PM ndo ahusike na kuchukua hatua? Mukulu ndo anatakiwa awajibike manake ndo aliewapa kazi! Ili aache kuwapa watu kazi kwa kuangalia sura!
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Tena Pinda alishasema yeye si mamlaka iliyowateua ndiyo maana alimpigia JK akiwa nje ya nchi. Nadhani kuna upungufu wa uandishi, ilikusudiwa kuandikwa kuwa taarifa imewasilishwa serikalini kwa kupitia PM.
   
 7. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Amini usiamini hao watuhumiwa wanaweza wasishughulikiwe na wakamaliza ungwe yao mpaka 2015....hii ndo tz
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,818
  Likes Received: 83,216
  Trophy Points: 280
  King'asti, Mukulu hahusiki kabisa, yeye kazi yake ni kuchekacheka tu maamuzi mazito hayamhusu kabisa!!!! Pinda naye kapinda!!! Nchi yetu ina pengo kubwa sana la uongozi.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Lol! Umenifurahisha! Na mie napenda kuchekacheka,sijui nigombee 2015? Na tabasamu langu linalipa lipa,hehehe
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hata Jk mwenyewe hatumtaki ofisini kwani kakumbatia mabaya na maovu mengi ambayo inaonyesha dhahiri anausika moja kwa moja
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,818
  Likes Received: 83,216
  Trophy Points: 280
  Hahahahaha lol! We gombea tu ali mradi unipe mie umeneja wa kampeni kisha kama mgombea hutakiwi uendeshe gari :):) ile mashine yako kali uniachie mimi nijidai nayo mjini :):):) kama meneja wa kampeni yako. Kwanza nitakupigia debe la nguvu hapa jamvini, Kingasti for 2015. Hapa kuna wanachama karibu 60,000 fikiria hata tukipata 75% wakubali kukupigia debe!!!....Tukiweza kufanikisha hilo basi Rais wa kwanza Mwanamke wa Tanzania atakuwa King'asti :):):) King'asti for 2015!!!!
   
 12. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #12
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Pinda naye bure, he will never attain anything except kuwafurahisha CCM na kutetea unga wake.
   
 13. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,261
  Trophy Points: 280
  Shhhhhh! Sasa utawastua mapema waanze kunitoa roho buree! Tungoje labda nianzie ujairo.
  Inabidi niweke mtutu chini aisee!
   
 14. Click_and_go

  Click_and_go JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 451
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nimechoshwa kwa kuchezewa akili na hawa viongozi ambao hawataki kuwajibika!!!!
   
 15. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mkuu BAK nakwambia mpaka tufike 2015 hapa Tanzania kazi tunayo, hakuna rangi tutaacha kuona!!!!! Usanii mtupu !!!!
   
 16. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #16
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wanaweza kuwabadilishia vitengo kuwa wakuu wa mikoa, wakurugenzi, makamishina e t c na maslahi yao yakabaki vile vile, changa la macho!!!!!!!!
   
 17. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  We si mjeshi???????
   
 18. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mkuu BAK umejuaje ni mwanamke huyo Kingasti we mtabiri nini??????????
   
 19. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #19
  Dec 8, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hata ujinyonge mkuu hakuna hatua watakayo chukuliwa
   
 20. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #20
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pinda kama kawaida atapiga kimya hadi bunge lijalo likaribie, kisha utasikia wanaisoma hiyo taarifa kwa kina ili kuitolea maamuz hapo bunge la mwez wa kwanza litakuwa limepita tayari, af kama kawaida waTZ tunasahau mapema, jamaa wanaendelea kupiga mzigo hadi wanastaafu, si nasikia Luhanjo bado kidogo tu atimize muda wake?! Itabidi wamsubiri! Nadhani mnakumbuka yale ya yule AG aliyepita, kumbuka maadhimio ya kamati ya mwakyembe.
   
Loading...