Hatma ya Jairo, Luhanjo mkononi mwa Pinda

Hatma ya Jairo, Luhanjo mkononi mwa Pinda

kesi ya nyani unampelekea nyani mkubwa? Pinda nae yuko kwenye list ya kuwajibishwa
 
Shhhhhh! Sasa utawastua mapema waanze kunitoa roho buree! Tungoje labda nianzie ujairo.
Inabidi niweke mtutu chini aisee!


Sitii neno tena 🙂🙂 lakini Ujairo achana nao haulipi 🙂🙂, wewe focus tu kuingia kwenye ile nyumba kubwa nyeupe. Furahia miaka 50 ya uhuru wa nchi yetu ya Tanganyika.
 
Yaani Pinda ndo kwa shockabsorber ya udhaifu wa JK.

Hivi issue ya Jairo na Luhanjo inamhusu vipi Pinda wakati kwa ajiro alishema wazi agekuwa na mamlaka nini angefanya.

Hii issue ni ya JK . Huyu mwandishi anarudisha mkanda nyuma.
 
huyu mwandishi kivibo kweli..Pinda mwenyewe si alishasema kuwa hana mamlaka? Hiki kizibo vipi
 
Kiutendaji ni kweli hatima yao iko mikononi mwa Pinda lakini toka awali ilionyesha kuwa Waziri mkuu hana maamuzi juu ya hili make toka siku ya kwanza pale Bungeni alisema Rais yuko safarini na ingekuwa maamuzi yake angechukua hatua muda uleule. Hivyo naona Waziri Mkuu Pinda yupo kama hayupo wenye maamuzi juu ya hili wapo. Ndo maana alipata aibu kwa kulisemea hilo pale Bungeni lakini wenye mamlaka juu ya hilo wakamsafisha na kumrejesha kazini tena kwa kufanya tafrija ya ushindi dhidi ya Wanoko kuashiria kuwa wenye wivu wajinyonge. sasa iweje leo tutarajie muujiza toka kwa Pinda?"NCHI HII INA WENYEWE BWANA" sisi ni wapigadebe tu.
 
Mimi na wenzangu kilio chetu mbele za Mungu ni juu ya hawa UWT waliowaingiza wahuni hawa kwenye madaraka ya kuongoza nchi wakati tangu mwanzo walionekana mapumba matupu. Ila ninyi UWT mliohusika mjue mbele za Mungu sauti za watanzania zinazomfikia Mungu kila siku matokeo yake ni laana isiyo na mwisho hadi vizazi vyenu. Pole Tanzania!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lakini inakuaje PM ndo ahusike na kuchukua hatua? Mukulu ndo anatakiwa awajibike manake ndo aliewapa kazi! Ili aache kuwapa watu kazi kwa kuangalia sura!

Pinda anajua ukomo wa madaraka yake na ndio maana alisema kuwa ingekuwa yeye ndiye mwenye mamlaka ya uteuzi wakati ule angelikuwa kisha mfukuza kazi; sasa mnaposema tena kuwa hatma ya Jairo na Luhanjo iko mikononi mwa Pinda naona kama nikuspin kuonesha kuwa mkweree yeye sio jukumu lake kuwaadabisha hawa madhalimu bali Pinda ndio aonekane hafai!!! Hawa watu ni wateule wa Jakaya na yeye ndio anatakiwa awafukuze period, aache usanii wake nchi hii sio yake ni yetu sote!!
 
Hatua zingechukuliwa hata kabla ya kamati ya Bunge hapa ni usanii tu kwenda mbele
 
Mimi na wenzangu kilio chetu mbele za Mungu ni juu ya hawa UWT waliowaingiza wahuni hawa kwenye madaraka ya kuongoza nchi wakati tangu mwanzo walionekana mapumba matupu. Ila ninyi UWT mliohusika mjue mbele za Mungu sauti za watanzania zinazomfikia Mungu kila siku matokeo yake ni laana isiyo na mwisho hadi vizazi vyenu. Pole Tanzania!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu hao walishabadilisha jina siku nyingi wanajulikana kama ni UWM na siyo UWT maana baada ya kukatiwa keki ya Tanganyika wameamua kuangalia pembeni ili nao wafaidi na hivyo kula kuku kwa mrija.
 
Back
Top Bottom