Hatma ya ATCL, Sonangol ya China kujulikana wiki ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatma ya ATCL, Sonangol ya China kujulikana wiki ijayo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 15, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  Hatma ya ATCL, Sonangol ya China kujulikana wiki ijayo[​IMG]Na Leon Bahati

  HATMA ya mpango wa serikali wa kuingia ubia na Kampuni ya China Sonangol International Ltd (CSIL), kwa ajili ya kuendesha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), itajulikana wiki ijayo.

  Taarifa zilizoifikia Mwananchi jana na kuthibitishwa na Msemaji wa Wizara ya Miundombinu, Martin Ntemo, zilisema maofisa wa CSIL walikwishawasili nchini tangu juzi tayari kwa mazungumzo na serikali.

  "Ni kweli wamewasili jana (juzi) kwa lengo hilo, lakini bado ofisi yangu haijapata taarifa rasmi kuhusu namna mazungumzo hayo yatakavyoendeshwa," alisema Ntemo.

  Kwa mujihu wa chanzo chetu ndani ya wizara hiyo, mazungumzo hayo yalitarajiwa kuanza jana jioni kwa kuwashirikisha Makatibu Wakuu wa Wizara za Fedha na Uchumi, Miundombinu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wataalamu wengine wa serikali.

  Mazungumzo hayo yanafanyika wakati serikali ikifahamu wazi kuwa iliwahi kujikwaa kisiki katika mkataba wa namna hiyo, ilipoingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mwaka 2002.

  Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawamba, aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa tayari CSIL na serikali zilikwishatilia saini hati za makubaliano.

  Alisema hati hizo zilisainiwa Februari mwaka huu na kwamba zinaainisha maeneo mbalimbali ya uwekezaji, ikiwa ni pamoja na kununua ndege saba kabla ya mwaka 2012.

  Kutokana na makubaliano hayo, CSIL limegharimia moja ya kampuni za nje kufanya tathmini ya mfumo mpya wa kuiendesha ATCL na idadi ya wafanyakazi watakaoajiriwa.

  Serikali ilivunja mkataba mwingine wa namna hiyo kati yake na SAA Septemba mwaka 2006, baada ya kubaini kuwa haukuwa na manufaa.

  Baadaye, serikali ilitangaza azma ya kuifuifua upya ATCL lakini mambo yalikuwa mabaya zaidi baada ya kunyang’anywa leseni yake ya kutoa huduma mwaka jana kutokana na kasoro kadhaa za kiutendaji. Baada ya kusahihisha kasoro hizo, ATCL ilirejeshewa leseni yake lakini majeraha ya kupokonywa leseni yaliifanya ichechemee sokoni.
   
Loading...