Hatimayee boeing sasa kukubali makosa

Hatimayee boeing sasa kukubali makosa

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,867
Reaction score
8,275
1552545249320.png


Boeing 737 Max: Kampuni ya Marekani inayotengeneza ndege iliyoanguka Ethiopia yasitisha matumizi ya ndege zote aina hiyo

Kampuni ya Boeing Marekani inayotengeneza ndege iliyoanguka Ethiopia imesitisha matumizi ya ndege zote aina hiyo baada ya wachunguzi kubaini ushahidi mpya katika eneo ambako ndege ya Ethiopia Airlines ilianguka.

Kampuni hiyo ya Marekani imesema itasitisha usafiri wa ndege zote 371 zinazohudumu.

Shirika linalosimamia usafiri wa anga Marekani FAA, limesema ushahidi mpya pamoja na data mpya za satelaiti zimechangia uamuzi huo wa kupiga marufuku kwa muda usafiri wa ndege hizo.

FAA awali lilisisitiza ndege ya Boeing 737 Max 8 ni salamawakati mataifa mengine yakipiga marufuku usafiri wa ndege hizo.

Ajali hiyo siku ya Jumapili mjini Addis Ababa ulisababisha vifo vya watu 157.

Ni ajali ya pili kuwahi kushuhudiwa ya ndege hiyo chapa Max 8 katika miezi mitano baada ya ajali nyingine nchini Indonesia mwaka jana Oktoba iliosababisha vifo vya watu 189.
 
Lazima wakubali ni ndege mbili zimepata ajali kwa kipindi kifupi lazima wachunguze wajue tatizo ni nini maana inahusisha roho za watu ndio maana wanaanga wengi kutoka USA wameenda Ethiopia kwa ajili ya uchunguzi...
 
Hata Trump kishazipiga stop zisiruke Nyumbani

Itabidi walipe fidia kubwa Sana wao ama Makampuni yao ya Bima ikigundulika kuna kosa la Kiufundi ndio linagharimu Maisha ya watu
 
Back
Top Bottom