esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 552
WAZIRI wa Nchi, Osi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amesisitiza kuwa zuio la mifuko ya plastiki, litakuwa la kisheria na hivyo hakutakuwa na msalie mtume. Akizungumza Dar es Salaam jana, January alisisitiza kuwa marufuku ya mifuko hiyo, lengo lake ni kulinda afya za wananchi na mazingira.
“Madhara yanayotokana na matumizi ya mifuko hiyo ni makubwa sana na hivyo si rahisi kwa mtu kuona katika hali ya kawaida,” alisema. Aliongeza kuwa wizara yao, itahakikisha zuio hilo linafanikiwa bila vikwazo na kwamba wananchi wataendelea kuelimishwa.
“Katika kukabiliana na zuio hili, changamoto ni nyingi ikiwemo kutokuwa na ufahamu mpana wa wananchi juu ya athari zake, lakini tumejipanga kuhakikisha linafanikiwa na hatua muhimu zaidi ni kutoa elimu kwa wananchi,” alisisitiza. Aliongeza, “Katazo la kitu kama hiki halikosi vikwazo, kelele na hata vitisho kutoka kwa watumiaji na wazalishaji. Hivyo tumejipanga kukabiliana na yote hayo.
” Alisisitiza kuwa elimu ya kutosha, itatolewa kuhusu madhara ya mifuko ya plastiki na njia mbadala zitaanza kutumika wakati wa kipindi cha zuio. “Tumejipanga kiasi cha kutosha juu ya namna ya kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza na jambo muhimu sana ni ushirikiano kwa kuwa mazingira ni suala muhimu kwa kizazi cha leo na kesho; hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuyalinda,” alisema January.