Hatimaye Waziri Mkuu Majaliwa, apiga marufuku mifuko ya Plastiki

Hao Wanyarwanda hawazidi watu 6m, hao Wazanzibara ukijumlisha na Wanzibari idadi yao haizidi 1.5m....!

Huwezi kulinganisha na mahitaji ya nchi yenye zaidi ya watu 49.5m.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kuna wa

Mkuu kuna watu wapo vizuri soon utasikia mashine zishaingia bongo kwa ajili.ya bidhaa mpya ya mifuko isiyo ya plastic pia kuna wachina wapo bongo kwa surveg so washapeleka habari kwao kuhusiu kubadilika kwa soko la tanzania hivyo washaanza michakato ya kutengensza bidhaa mpya mwezi wa 5 tu zishatua bongo
Binafsi nimewahi kuitengeneza mifuko ya karatasi,gundi ilikuwa uji wa Muhogo. Ila malighafi ilikuwa ile mifuko ya cement ya zamani ilikuwa ina karatasi nying ndani, hivyo tiliinunua kutoka site za ujenzi na kutoa karatasi ya juu na kutengeneza mifuko, lakini hiyo ili kuwa kwa mahitaji ya kijieneo kidogo tu. Hii tunaongelea mahitajoi ya population ya 50milion people. Kama taifa hatuna kiwanda chetu hata kimoja cha kutengeneza vifungashio mbadala wa hiyo mifuko ya plastic. Ndio maana nikasema tunaiga kila kitu lakini huwa hatujiandai kujua tuta sustain vipi hiyo shortage ya vifungashio.
Wewe umeongea wachina, na vipi ikiwa hawatakuja kuwekeza tutaendelea kuagiza kutoka china?!
 
Hoja dhaifu sana umetoa.
1.) Tanzania haiigi kila kitu, tunaiga mazuri na kukataa mabaya, mfano tulikataa ushoga.

2.)Unajua madhara ya sumu zitokanazo na hiyo kuteketeza taka za plastic?

3.)Aliesema hatuna mifuko ya karatasi / mbadala ni nani?

4.)Hao wawekezaji wamepewa muda wa kuboresha mitambo yao ili kutengeneza vifungashio mbadala, mfano vikapu vigumu vya aina mbali mbali, mifuko ya vitambaa, mifuko ya karatasi nk.
Hahaha wewe hoja zako siyo DHAIFU usije niua bure.
(1) umesema mashoga mlikataa, Mbona wapo mtaani wengi sana, au hawa waliopo walikuwa imported kutoka nje au tulipewa msaada na watu wa marekani?
(2)sifahamu ni sumu gani iko kwenye hivyo vifungashio vya plastic , inekuwa bora kama ungetutajia na maelezo ni jinsi gani tukitumia hiyo mifuko inatuathiri.
(3)kam mifuko mbadala ipo, iko wapi na inatengenezwa kwa malighafi gani na wapi?
(4) sikuwa nafahamu kama wawekezaji walipewa muda wa miaka mitatu. niliona tangazo la kuzuia na hotuba ya waziri mkuu lakini haikusema huo muda wa miaka mitatu.
 
Unapoita maamuzi ya kijinga nakuona wewe ndio mjinga zaidi. Hauelewi madhara ya hii mafuko kwa afya na mazingira.

Afya
Jambo moja tu hapa nakupa. Hii mifuko ndo wamegeuza kifungashio cha chakula cha haraka - fast food. Chips na kuku wa moto, wali au ugali ndio vifungashio. Je unatambua madhara ya huu ujinga unafanywa na wananchi mjini na vijijini? Kingine, watu wanapika viazi, mihogo na wali wanafunike na hayo maplastic. Kansa nje nje hapa.

Mazingira
Hii mifuko imeenea mijini na vijijini. Je kwa uelewa na ujinga wa watanzania wengi ni nani anawaza ku recycle hii kitu zaidi ya kutupa na kufukia ardhini! Kwa ujinga wa watu wengi suala la recycle halipo. Sio suala la kupayuka tu mdomoni ni kitu inahitaji ustaarabu fulani vile.

Naunga mkono hoja ya Waziri mkuu kwani wawekezaji katika mifuko hiyo walipewa notice ya miaka 3 wabadili mfumo wa viwanda, kama waliendelea kuwekeza shauri yao
Ni sumu gani iliyoko kwenye hiyo mifuko ya plastiki? na mechanism yake ikoje au inafanyaje kutuathiri watumiaji, tukibebea nguo au vyakula tu, na mfuko huwa hauyeyuki hata ukiweka ugali au chips sasa inakuwaje unasema cancer, ni jinsi gani cancer inaletwa na hii mifuko, ungetoa elimu ili tuelewe nasisi badala ya kututisha ukiwa gizani.
Recycling ndiyo muhimu ni hili lingefanywa na serikali maana ndiyo inamiliki ma dampo yote nchini, na kama serikali haiwezi ingeomba msaada wa technologia hiyo kutoka nchi wanazoshirikiana kama marekani,japan, na uchina.
China,marekani na japan na mataifa mengi makubwa na madogo wanatumia vifungashio vya plastiki na sijasikia wakisema source za cancer huko kwao ni mifuko hiyo, wao hawajapiga marufuku lakini sisi tunajidai tunajuuua sana. Zama hizi ni za kuleta technologia sio kuzuia, kama hujui mpe anayejua, lakini kuzuia siyo solution ya vifungashio, unless mmejiandaa kuagiza nje au kuwapa wafanyabiashara tender za kuleta vifungashio ndani.
 
Poa haina shida,nakumbuka wakati pombe ya viroba vlinapigwa marufuku humu ndani povu liliwatoka mpaka basi na sasa Plastic tupilia kule na karatasi itabaki kileleni,Ahsante sana PM Majaliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini wao hoja yao kuhusu viloba ni kwamba vijana wanaharibika. Je kuna study yoyote iliyoonyesha tangu serikali imezuia viloba sasa vijana hawaharibiki?
 
Ni sumu gani iliyoko kwenye hiyo mifuko ya plastiki? na mechanism yake ikoje au inafanyaje kutuathiri watumiaji, tukibebea nguo au vyakula tu, na mfuko huwa hauyeyuki hata ukiweka ugali au chips sasa inakuwaje unasema cancer, ni jinsi gani cancer inaletwa na hii mifuko, ungetoa elimu ili tuelewe nasisi badala ya kututisha ukiwa gizani.
Recycling ndiyo muhimu ni hili lingefanywa na serikali maana ndiyo inamiliki ma dampo yote nchini, na kama serikali haiwezi ingeomba msaada wa technologia hiyo kutoka nchi wanazoshirikiana kama marekani,japan, na uchina.
China,marekani na japan na mataifa mengi makubwa na madogo wanatumia vifungashio vya plastiki na sijasikia wakisema source za cancer huko kwao ni mifuko hiyo, wao hawajapiga marufuku lakini sisi tunajidai tunajuuua sana. Zama hizi ni za kuleta technologia sio kuzuia, kama hujui mpe anayejua, lakini kuzuia siyo solution ya vifungashio, unless mmejiandaa kuagiza nje au kuwapa wafanyabiashara tender za kuleta vifungashio ndani.
Tatizo huwa hampendi kusoma maandiko mbalimbali na tafiti. Hebu fuatilia hapo chini maana nikianza kuandika hapa muda hautoshi.

HATARI UNAYOWEZA KUIPATA UNAPOTUMIA BIDHAA ZA PLASTIKI | Mtanzania
mtanzania.co.tz › hatari-unayow...

HATARI UNAYOWEZA KUIPATA UNAPOTUMIA BIDHAA ZA PLASTIKI
By
Mtanzania Digital

a50da50d05318db6146a9993112ce4dc-300x235.jpg

Na MWANDISHI WETU,
MAISHA ya mwanadamu kwa sasa yanategemea mno bidhaa za plastiki katika kuhifadhia mizigo mbalimbali ikiwamo vyakula, maji na mafuta ya kula.
Licha ya kutumika katika matumizi mbalimbali katika kuhifadhia vitu, imebainika kuwa plastiki ina madhara makubwa katika matumizi ya binadamu.
Utafiti uliofanywa na Jumuiya ya Madaktari wa Marekani ulitoa tahadhari kuhusu matumizi ya vyombo vya plastiki vinavyotumika kufungashia na kubebea vyakula.
Wanasayansi hao wanasema plastiki ina madhara makubwa endapo ikikutana na joto kali na kutoa kemikali iitwayo BPA(bisphenol A).
Mwaka jana, Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba alipiga marufuku moja kwa moja, utengenezaji, usambazaji, uingizaji na matumizi ya mifuko ya plastiki nchini kuanzia mwaka huu.
Makamba alisema mifuko ya plastiki imekuwa na changamoto kubwa ya mazingira kwa kuwa sehemu kubwa ya mifuko hiyo hutolewa bure na kusambaa ambapo husababisha mafuriko na athari nyingine kubwa za kimazingira.
Anasema ofisi yake inakamilisha majadiliano ndani ya serikali na baadae kuwahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku moja kwa moja matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.
Anasema serikali itatoa muda kwa waliojiajiri na kuajiriwa kwenye biashara ya mifuko ya plastiki kujiandaa kuacha shughuli hizo na itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungashio mbadala.
“Tumetuma wataalamu wa serikali katika nchi zilizofanikiwa kwenye jambo hili ili kujifunza namna bora ya kulitekeleza jambo hili,” anasema Makamba.
Nchi ya Rwanda na Zanzibar zimefanikiwa katika upigaji marufuku wa mifuko ya rambo baada ya kuonekana ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira na mafuriko kutokana na mifuko hiyo kuziba katika mitaro.
Licha ya serikali kupiga marufuku matumizi ya mifuko plastiki, vyombo vya plastiki aina ya sahani, bakuli, vikombe vimeendelea kutumika huku viwanda vikizidi kuvizalisha kwa wingi hivyo kufanya afya ya mwanadamu kuwa hatarini kukumbwa na magonjwa ya saratani.
Walter Miya ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Marafiki wa Watoto wenye Saratani Tanzania, anasema plastiki imetengenezwa kwa kemikali zaidi ya 200 ambazo zinaweza kusababisha aina 100 za saratani.
Anasema toka matumizi ya plastiki yazidi kuongezeka nchini, ugonjwa wa saratani nao umeongezeka hasa kwa upande wa akina mama ambapo ugonjwa huu huharibu ukuaji wa mfumo wa uzazi hususani kwa watoto ambao bado hawajazaliwa, mabadiliko ya kijenetiki, matatizo ya kushindwa kuona, uyeyushaji wa chakula tumboni kuwa wa tabu au kutokamilika na ini kushindwa kufanyakazi vizuri.
Anasema kutokana na utafiti mdogo walioufanya inaonesha kuwa asilimia 60 ya saratani zimesababishwa na matumizi ya vifaa vya plastiki.
“Watu wengi wanatumia vifaa vya plastiki bila kujua madhara yake, ukienda majumbani utakuta wanawake wengi wanachemsha maji na kuyahifadhi katika ndoo za plastiki yakiwa bado ya moto.
“Baada ya muda ukija kuchunguza ile ndoo utakuta ina mabaka mabaka maana yake imeshatoa kemikali nyingi na athari hutoiona kwa muda huu, mpaka ifike miaka 10 au 15 na ndio maana huwezi kugundua saratani yako imesababishwa na nini,” anasema Miya.
Anasema pia kuna kinamama ambao hutumia mifuko ya rambo kufunikia wali wakati wa kupika ili uweze kuiva haraka bila kujua kuwa mifuko hiyo ina athari kubwa kutokana na kemikali zilizopo kuingia katika chakula hicho.
Miya anasema jamii inapaswa kupunguza matumizi ya plastiki au kutumia zilizo na viwango ambavyo hazitoleta madhara na kwa upande wa wachemshao maji wanapaswa kusubiri hadi yapoe ndipo wamimine katika ndoo.
“Licha ya jitihada zinazoendelea kufanywa na watu mbalimbali, bado jamii haina uelewa kuhusiana na vifaa hivyo vya plastiki.
“Hivi karibuni kuna taarifa ilisambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa watu wasitumie vikombe vya plastiki, sahani, bakuli na hata mifuko ya rambo katika matumizi ya vyakula, lakini ukipita mitaani utakuta bado wanaendelea navyo,” anasema Miya.
Anasema kuna vitu vingi ukiviangalia unaweza ukaogopa ila huwezi kuvikimbia ni kuangalia ni namna gani tunaweza kuvipunguza ili athari ya saratani isizidi kuongezeka.
“Binafsi natembea na kontena langu la aina ya glass ili kuweza kuhifadhia chakula pindi ninapoenda kununua , nimeamua kutembea nalo kutokana na mama lishe wengi kutumia vyombo vya plastiki katika kuwekea chakula,” anasema.
“Kutokana na kukithiri kwa matumizi ya plastiki wakati serikali ilipiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki, tunahitaji sera na sheria dhidi ya matumizi ya vifaa hivi.
“Inatakiwa iwepo sera ya kutoruhusu kusafirisha maji bila kuwa na vifaa vinavyodhibiti joto kama wafanyavyo wanaposafirisha maziwa,” anasema Miya.
Anashauri iwepo sheria ya kuwadhibiti wauzaji wa maji juani kuanzia asubuhi hadi jioni kutokana na kupata kemikali nyingi inayotoka kwenye chupa za plastiki kwa sababu ya kuwapo juani kwa muda mrefu.
 
Mifuko ya plastic inamadhara makubwa sana siyo tu kwa mazingira lakini pia hata kwa binadamu!
Kama kuna mtu hayajui hayo basi atafute namna yake kujifunza kujua ni madhat gani na kwa vipi na siyo kupinga maswala ya msingi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao Wanyarwanda hawazidi watu 6m, hao Wazanzibara ukijumlisha na Wanzibari idadi yao haizidi 1.5m....!

Huwezi kulinganisha na mahitaji ya nchi yenye zaidi ya watu 49.5m.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama idadi yetu ni kubwa maana yake ni kwamba fursa za ajira kwa watu wa chini watakakuwa wanatengeneza vikapu na mifuko mingine mbadala zitakuwa nyingi zaidi na kusaidia kupunguza tatizo la ajira nchini, si ndio?
 
Binafsi nimewahi kuitengeneza mifuko ya karatasi,gundi ilikuwa uji wa Muhogo. Ila malighafi ilikuwa ile mifuko ya cement ya zamani ilikuwa ina karatasi nying ndani, hivyo tiliinunua kutoka site za ujenzi na kutoa karatasi ya juu na kutengeneza mifuko, lakini hiyo ili kuwa kwa mahitaji ya kijieneo kidogo tu. Hii tunaongelea mahitajoi ya population ya 50milion people. Kama taifa hatuna kiwanda chetu hata kimoja cha kutengeneza vifungashio mbadala wa hiyo mifuko ya plastic. Ndio maana nikasema tunaiga kila kitu lakini huwa hatujiandai kujua tuta sustain vipi hiyo shortage ya vifungashio.
Wewe umeongea wachina, na vipi ikiwa hawatakuja kuwekeza tutaendelea kuagiza kutoka china?!
Kila mtaa ukiwa na kikundi cha wajasirimali wapatao 10 ambao wanazalisha mofuko mbadala ya karatasi, vitambaa, vikapu nk., unadhani ni ajira ngapo zitatengenezwa, hata nchi iwe kubwa vipi, watu wasio na ajira ni wengi, hivyo hawawezi kushindwa kukodhi mahitaji
 
Amesema kuwa wiki hii Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza kukutana na taasisi mbalimbali ikiwemo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baraza la Mazingira Nchini (Nemc) na Wizara ya Mambo ya Ndani kujadili suala hilo. “Kanuni tayari zinangoja kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali.

Kama tukikubaliana inaweza Mei ukawa mwisho wa matumizi ya plastiki,”
DANADANA ZA MAKAMBA CHALI. KAMA HAKUWAHI KUCHUKUA MGAO MWAKA HUU SHAURI YAKE
Makamba Useless kabisa .

Hii ndio point ya kujichukulia Credit ila yeye kwakuwa na ma hasira yake ya kuonekana hafai dispite ya effort zake kipindi cha uchaguzi uliopita akaamua kukaa kimya forever anajitokeza tu anapojisikia .

Haya sasa kama ndio ana ndoto za kiobama Obama wajanja wanampiga gepu hivi hivi anajiona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila mtaa ukiwa na kikundi cha wajasirimali wapatao 10 ambao wanazalisha mofuko mbadala ya karatasi, vitambaa, vikapu nk., unadhani ni ajira ngapo zitatengenezwa, hata nchi iwe kubwa vipi, watu wasio na ajira ni wengi, hivyo hawawezi kushindwa kukodhi mahitaji
Hahaha haya mambo ya vikundi ni ujinga achana nayo.
Malighafi ziko wapi?!
 
1074163

Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) limeipongeza serikali ya Tanzania kwa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya WWF kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Dk. Dk Marco Lambertin wamejipanga kushirikiana na Tanzania kwenye jitihada za kudhibiti janga la uchafuzi wa mazingira kutokana na plastiki kwa kutumia ufahamu wa kisayansi juu ya suala hilo na kutoa mapendekezo kwenye sera za udhibiti.

“Tunashuhudia zaidi ya tani milioni nane za plastiki zikiingia kwenye bahari kila mwaka huku tani milioni 104 zikitarajiwa kuharibu mfumo wa mazingira ikapo mwaka 2030 kama hatua za haraka hazitachukuliwa, zitaharibu asili, maisha ya binadamu, afya na wanyamapori,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa WWF Tanzania, Dk Amani Ngusaru, ameeleza kuwa plastiki ni sababu ya kwanza ya uharibifu mkubwa wa mazingira ikiharibu mazingira ya asili na rasilimali kuliko watu wengi wanavyofahamu inachukua zaidi ya miaka 100 kwa mfuko mmoja wa plastiki kuoza na hii inaongeza ukubwa wa tatizo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitangaza Marufuku hiyo kuanzia Juni Mosi, alipokuwa akijibu hoja za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya osi ya Waziri Mkuu mwaka 2019/2020.

Tanzania inaungana na nchi nyingine 13 barani Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda na Rwanda, ambazo aidha zimepiga marufuku ya matumizi ya mifuko hiyo ya plastiki au kuweka tozo za mifuko hiyo ili kudhibiti na kuimaliza kabisa.
 
Hahaha haya mambo ya vikundi ni ujinga achana nayo.
Malighafi ziko wapi?!
Kumbe najadiliana na taahira? Yaani unauliza suala la malighafi Tanzania, mikeka wabayosuka akina mama malighafi huwa wanatoa wapi? Kamba za katani malighafi huwa wanatoa wapi? Vitambaa vya khanga malighafi huwa wanatoa wapi? Viwanda vya madaftari na karatasi malighafi huwa wanatoa wapi? Jingakabisa!
 
Makamba Useless kabisa .

Hii ndio point ya kujichukulia Credit ila yeye kwakuwa na ma hasira yake ya kuonekana hafai dispite ya effort zake kipindi cha uchaguzi uliopita akaamua kukaa kimya forever anajitokeza tu anapojisikia .

Haya sasa kama ndio ana ndoto za kiobama Obama wajanja wanampiga gepu hivi hivi anajiona

Sent using Jamii Forums mobile app
Dogo kwisha habari yake. Urais atausikia kwenye redio. Labda aombe nafasi ya yule mgogo mwenye afya dhaifu
 
Waondoe tu hiyo mifuko wajasiriamali wapate solo la bidhaa zingine ambazo hazichafui mazingira. Kongole sana kwa Wizara husika japo wamechelewa.

Back
Top Bottom