Hatimaye serikali yajenga matuta tumaini makumira

kinganola

Senior Member
Aug 16, 2011
117
30
Lile sakata la vurugu baina ya polisi na wanachuo wa Tumaini Makumira hatimaye limepata ufumbuzi baada ya Serikali kupitia kampuni ya ROCK TRONIC LTD kukubali kujenga matuta na kazi imeanza leo tarehe 15.11
 
Damu ya Emmanuel Ulomi hatimaye imekuwa chachu ya kuleta mabadiliko baada ya kufuata protoko na kuandika barua zaidi ya kumi kuomba matuta bila ya mafanikio,HATIMAYE VURUGU ZIME ZAA MATUNDA.
 
Hongereni, hiyo ndo serikali yetu bila kuishinikiza hakifanyiki kitu, utaona wenzenu wakija kutoka vijijini/ng'ambo wanagongwa na kukatishwa maisha. Sasa hao police walikuwa wanazuia nini badala ya kuwalinda, polisi wa Tz bwana, hata hao RPC au OCD sijui kama wanajua kazi zao vizuri?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Lile sakata la vurugu baina ya polisi na wanachuo wa Tumaini Makumira hatimaye limepata ufumbuzi baada ya Serikali kupitia kampuni ya ROCK TRONIC LTD kukubali kujenga matuta na kazi imeanza leo tarehe 15.11
. Hiyo ni matokeo ya nguvu ya umma maana vijana wangekaa kimya wangelea kugongwa na magari hadi mwisho
 
Bila damu kumwagika seikali iko kiziwi. Kweli hatuna serikali.
 
Lile sakata la vurugu baina ya polisi na wanachuo wa Tumaini Makumira hatimaye limepata ufumbuzi baada ya Serikali kupitia kampuni ya ROCK TRONIC LTD kukubali kujenga matuta na kazi imeanza leo tarehe 15.11

hiyo kazi imeanza saa ngapi?
 
Nipo kwenye eneo la tukio,nimezungumza na Mkandarasi wa kampuni ya ROCKTRONIC amenihakikishia kwamba ifikapo kesho,kazi itakuwa tayari.
 
poleni wote mlio haribiwa magari yenu,poleni wanachuo wote mlio risk maisha yenu na kuumia kwa ajili ya haki ya kizazi kijacho,sasa misiba ya ajali hapa makumira,kilala na denish itapungua kwani bams ndo zinajenwgwa.
 
Tunategemea kuwa na msafara wa kwenda kwenye mazishi ya Emmanuel Ulomi aliye fariki baada ya kugongwa na gari hapo getini Tumaini Makumira,safari itakuwa kuelekea moshi siku ya Alhamisi,wote mlio jirani,karibuni tumsindikize mweenzetu...
 
R.I.P Emmanuel Ulomi hakika utakumbukwa daima! Kufa kwake kumewakomboa wanachuo wenzake ambao nao wangefuata mkumbo huo wakupoteza maisha kwakugongwa na mabasi yenye kuendeshwa mota kasi na madereva wazembe kama kweli matuta hayo yatajengwa.
 
Poleni kwa msiba ingawa mimi siyo mmoja wa wale wanaopenda kila sehemu ikitokea ajali tujenge matatu bila kuangalia sababu hasa iliyosababisha ajali hiyo.
 
Damu ya Emmanuel Ulomi hatimaye imekuwa chachu ya kuleta mabadiliko baada ya kufuata protoko na kuandika barua zaidi ya kumi kuomba matuta bila ya mafanikio,HATIMAYE VURUGU ZIME ZAA MATUNDA.
Afadhari matuta yajengwe eneo hilo ni hatari saana, kuanzia kwenye sheli kupita darajani zimeisha tokea ajali nyingi na watu kupoteza maisha!!!!!!!!!!Ni vizuri uamuzi wa matuta kama pale Kambi ya Chupa hadi Shangarao, na hapo waweke hadi sehemu ya Danish!!!!!!!!
 
bila kuishinikiza serikali au bila damu kumwagika hakuna kitakacho fanyika
 
Mpaka jioni ya leo tarehe 15.11 Rocktronic kampani wamekamilisha matuta makubwa mawili,moja eneo la ajali na moja kwa Mama Jovita,kesho wameahidi kurudi kumalizia kuweka tuta ndogo za rasta moja upande wa juu na jingine upande wa chinni..Nguvu ya umma,jasho pamoja na maumivu yamezaa matunda...
 
Back
Top Bottom