Kuwa makini na hao mabinti watakula nauli yako ushindwe kwenda dar wala kurudi kilifiHabari za muda huu Jamii forum na poleni sana kwa mihangaiko ya hapa na pale ya kutafuta maisha.
Nakumbuka siku mbili tatu za nyuma nilikuwa na mawazo ya kuja Tanzania kutafuta opportunities za maisha kwani nimekaa Kenya muda mrefu na nikaona sio mbaya kama nikija nchi za karibu napo kuangalia opportunities zingine.
Kiufupi ni kwamba niliishi Tanzania kidogo sana nakumbuka tuliondoka wakati nipo mdogo sana wakati bado sina uelewa na tumekuwa tukiishi kenya maeneo ya kilifi. Sasa baada ya siku mbili tatu hizi kuangaika na kuweka sawa ishu za documents hatimaye nimefanikiwa kusafiri na kuja rasmi Tanzania kuja kutafuta opportunities za maisha na kiufupi ni kwamba majuzi nimefanikiwa kufika Tanga ambapo nipo hapa kwa siku ya tatu sasa na malengo yangu ni kufika dar es salaam ndani ya siku mbili hizi.
Hakika niliyojionea hapa tanga ni ya kipekee sana kwani watu wa huku ni wakarimu sana na wanapenda kuwa karibu na watu kwani tangu nifike hapa sijajisikia mpweke kwakweli. Vile vile utamaduni wa watu wa huku kwenye mambo ya ngoma zao pia nimevutiwa sana na mazingira ya huku nimeyapenda kwakweli.
Nimepita kwenye fukwe kwakweli panapendeza na vilevile mabinti wa huku ni wazuri sana na wakarimu hasa kwa mtu mgeni. Nilipanga kukaa siku mbili tu lakini ningependa kuongeza siku nyingine mbili zaidi.
Hizi ni baadhi ya picha za sehemu nilipotembelea na ningependa nishare hapa kwenye jukwaa.
View attachment 1508529View attachment 1508530View attachment 1508531View attachment 1508532View attachment 1508533