Hatimaye nami nimepata mchumba wa kuoa

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
2,894
2,000
Wakuu salam!

Nimekuwa nikihangaika kutafuta msichana wa kuoa kwa miezi kadhaa bila mafanikio. Nikadiriki kuleta uzi kule love connect kutafuta msichana wa kuoa lakini sikuambulia hata salam ya msichana hata mmoja.

Baadae nikawa navizia wasichana wanaoleta maombi ya kutafuta wenza kule love connect lakini kila niliemwendea PM hakuna hata aliejibu

Basi hivi karibuni nikaenda kijijini kwetu kusalimia. Nilikuwa nimekaa muda mrefu kidogo bila kwenda kwetu, almost 4+ years aisee. Nilipofika nikaelekezwa kwa mzee fulani (tumuite Yohana japo si jina lake); nikaambiwa kwa mzee Yohana kuna binti anaweza kukufaa.

Basi nikatafuta namba zake nikazipata. Huyu binti hana simu, ila anatumia simu na laini (namba) ya dada yake. Nikaongea nae, nikajitambulisha vizuri akanifaham, nikamweleza kusudio langu akanielewa japo alitaka kuleta zengwe kwamba sisi ni ndugu, na of course sisi ni mtu na mtani (BINAMU).

Basi bwana, siku kama mbili tukapanga kukutana tuonane na tuongee vizuri. Siku ya kuonana ikafika, akadai location ya kukutania ni KWAO NYUMBANI.

Nikamuuliza "Wazazi wako hawatakuwepo??"
(Maana wazee wake wananifaham vizuri sana na tunaheshimiana mno)

Akasema "watakuwepo lakini ukifika wataondoka"

Daah. Basi nikaenda, nilipoka usawa wa kwao, nikamuona mzee wake na mama wote wapo, aah nikaogopa kukatisha kwao, nikanyooka nikafika mbele kidogo nikamwambia kwa sms "Njoo huku".

Basi mtoto akaja bwana, mashallah!!!! Mtoto maji ya kunde, miaka 19, mrefu kiasi, amejazia mwili kiasi chake!! Of course nililidhika na muonekano wake. Katoto kapole jamani, toka naongea nae kwenye simu sauti ya upole.

Basi tukaongea pale, katoto kana aibu kishenzi, muda wote kameinama chini, kuniangalia hakawezi. Baadae nikaondoka, akanisindikza huku anasukuma baskeli ya yangu aina ya kamongo nyeupe!! Nikamwambia

"Mimi muda si mrefu nitarudi mkoani kutafuta (hela), kwaiyo nakuacha wewe huku, wewe ndio mchumba ninaekutegemea, naomba sana ujitunze na ujilinde, sitapenda nikiwa huko (mkoani) nisikie tabia na skendo chafu kwako, sawa??"

Akajibu "Sawa nimekuelewa, nitajitunza na nakutegemea wewe, naomba usinidanganye, nikakaa nakusubiria halafu usinioe"

Nikamwambia "Nakuahidi, lazima nikuoe mwakani mwezi wa...(nikamtajia mwezi).
Akasema "Sawa, usafiri salama na ufike salama" Nikasema "Asante na wewe ubaki salama, lakini japo huna simu, jitahidi mawasiliano yawe ya mara kwa mara"

Akasema "Sawa, kwaheri"

Hapo tukawa tumeagana. Sijampa hata cent 100, wala sijampa simu wala kumuahidi mambo ya kumnunulia simu.

Keshokutwa yake nikasepa. Ni miezi miwili sasa, tunaendelea na mawasiliano vizuri kabisa kwa kutumia simu ya dada yake.

Siku 1 nikapata wazo, kwamba binti awaambie wazazi wake ili tujue 1 mapema, wanaafiki au wanazingua kwa maana undugu wetu sio wa mbali aisee.
Basi binti akasema nitawaambia kesho na majibu nitakupa kesho hiyo hiyo. Kesho ikafika, jioni ya saa 1 akatuma sms,
"kazi yako tayari."
Nikauliza "Majibu?"
Akasema "Wamekubali tuendelee"
Mimi: "Uliwaambia wote wakiwa pamoja?"
Yeye : "Nilimwambia mama, yeye ndo akaenda kumwambia baba, ndo akaleta majibu kuwa haina shida tuendelee"

Nilifurahi sana jamani, niliruka ruka kwa furaha japo sikuonesha kwa binti kuwa nime-overjoy!

Sasa juzi juzi nikishirikiana na mwanangu fulani alieko pale kijijini nikatuma hela amnunulie simu ampelekee. Jana ndo tumekamilisha mchakato na simu imenunuliwa. Nikampigia simu dogo (mchumba wangu) nikamwambia "Nimekununulia simu anayo fulani (jamaa), nenda ukaichukue kwake.
Akajibu " Kwa leo siwezi kupata muda, nitaichukua jumapili nikienda kanisani"

Kwa ufupi wakuu, mimi kizibo nimepata mchumba. Na bahati nzuri nimepata binti ambae kwa pale kijijini ana sifa nzuri labda abadirike baadae huko. Nimejitahidi kuulizia kwa watu wanaomfaham, wanawake kwa wanaume, mabinti kwa masela, wababu na wabibi lakini wamekuwa wakiniambia "Huyo binti sijasikia mabaya yake, anafaa kabisa kuwa mke, kama umedhamilia kumuoa wee muoe hana makuu"


Mlioko kwenye ndoa naomba mnikaribishe, mnipe ushirikiano, uzoefu wenu na ushauri pia.

NAPOKEA USHAURI JINSI YA KUWA BABA NA MUME BORA. MAMBO YA KUZINGATIA NA YA KUEPUKA ILI NISIIBOMOE NDOA YANGU MWENYEWE.

NDOA NI JAMBO LA KHERI
HE WHO FINDS A WOMAN, FINDS A GOOD THING.

ASANTENI SANA, KARIBUNI
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
51,300
2,000
Wakuu salam!

Nimekuwa nikihangaika kutafuta msichana wa kuoa kwa miezi kadhaa bila mafanikio. Nikadiriki kuleta uzi kule love connect kutafuta msichana wa kuoa lakini sikuambulia hata salam ya msichana hata mmoja.

Baadae nikawa navizia wasichana wanaoleta maombi ya kutafuta wenza kule love connect lakini kila niliemwendea PM hakuna hata aliejibu
Tuletee huyo kuku wa kienyeji tumfundishe kunywa Heineken na kustarehe mjini!😂

Majibu utayapata tu hata kina Shilole walipotoka Igunga na kufika mjini mwanzoni walikuwa na adabu.
 

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
2,894
2,000
Kuwa makini na marafiki mkuu hasa hiyo ulimpa jukumu la kumnunulia Simu
Asante sana mkuu. Jamaa ni mtu poa kabisa, nimesoma nae namfaham kabisa kabisa hana tabia za kihuni na zaidi ameoa na ana familia yake. Na Zaidi ya yote, yeye (jamaa) na huyo binti ni mtu na kaka yake kiukoo
 

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
2,894
2,000
Tuletee huyo kuku wa kienyeji tumfundishe kunywa Heineken na kustarehe mjini!

Majibu utayapata tu hata kina Shilole walipotoka Igunga na kufika mjini mwanzoni walikuwa na adabu.
Usijali mkuu, ikitokea itokee tu! Lakini nitaamini ikitokea
 

Times9

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
3,167
2,000
255744401031_status_10f8121fe8b64dc4b3deba4afc712aa7.jpg
 

Kiraka

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
3,739
2,000
Wakuu salam!

Nimekuwa nikihangaika kutafuta msichana wa kuoa kwa miezi kadhaa bila mafanikio. Nikadiriki kuleta uzi kule love connect kutafuta msichana wa kuoa lakini sikuambulia hata salam ya msichana hata mmoja.

Baadae nikawa navizia wasichana wanaoleta maombi ya kutafuta wenza kule love connect lakini kila niliemwendea PM hakuna hata aliejibu
Hongera sana, tafadhali muwowe huyo binti, kila lakheri.
 

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
2,894
2,000
Sawa mkuu kila LA kheri Kiongozi... Ila unajukumu kubwa sana la kumwelekeza uhalisia wa maisha na Dunia huyo binti ukizingatia ndo kwanza yupo kwenye Ages ya 19 ambapo kila mtu kwenye uso wake atamwona mzuri kwa kuzingatia kile kimvutiacho...
Usisite kumwambia uhalisia Wa maisha yako pamoja an uhalisia Wa watu mjini... Nimeshuhudia kwa asilimia kubwa mabint wanaotoka vijijini wakiharibikiwa kwa kurubuniwa tu na vijana wa mjini (hakikisha unatenga muda wa kukaa nae na kuongea nae mambo mbali mbali pia kama utakuwa na uwezo wa kumtoa out kutokana na mfuko wako mtoe ili umjengee confidence na msimamo mkuu...
Yote kwa yote kila la kheri na hongera kwa kumpata mpendwa wako
Asante sana mkuu. Ushauri wako nimeuchukua na nitaufanyia kazi.
Shukrani sana mkuu
 

Capslock

JF-Expert Member
May 1, 2016
2,034
2,000
Huyo binti namfaham na leo nina miadi nae naenda kumnyandua.
Wakuu salam!

Nimekuwa nikihangaika kutafuta msichana wa kuoa kwa miezi kadhaa bila mafanikio. Nikadiriki kuleta uzi kule love connect kutafuta msichana wa kuoa lakini sikuambulia hata salam ya msichana hata mmoja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom