Hatimaye naanza kuona amani ya moyo

Kila siku nasema Wapigeni Matukio Mademu wenu! Usipofanya hivyo Unapigwa wewe....
 
Wewe ndo hujanielewa mkuu, hapa nilipo huenda kurudi ikafika mwakani ndo nikarudi ila siku tatu nazifurahia kuona amani inarejea. Nimejipa hadi mwaka wote huu uishe nitakuwa nishaona lolote ndani yake ,sitaacha kupiga simu kwa sababu ya mwanangu.
Hahahahaha eti "sitoacha kupiga simu kwasababu ya mwanangu" hicho ndio kisingizio chenu, unawezaje kukaa mwaka bila kumuona mwanao kama kweli unampenda? Ukweli ni kwamba hiyo simu unapiga ili uongee na mama yake na wala sio mtoto kama unavyojaribu kujiongopea hapa, anyways mkuu zipo njia nyingi za kujifariji kama hii unayoitumia wewe cha msingi rudiana na barafu ya moyo wako usijipe tabu na usisikilize maneno ya wana JF humu ndani wao pia wana vimeo vyao.
 
Yes Jo...

Mimi huwa naamini kitu kimoja, mwanamke unapaswa umfanye mume/boyfriend wako awe rafiki yako kindakindaki...

Wanaume huwa hawana hulka ya kusaliti marafiki wao wa moyo...

Kitu wanakosea wanawake, ni kujaribu kwa nguvu kuchukua nafasi ya mwanaume...
Katika series ya wakorea iitwayo king of tears :lee bang won

Mfalme lee bang won baada ya kuwa mfalme mkwe akataka waongoze wote nchi kitu ambacho lee bang won alikataa kata kata japo kuwa anapenda sana mkewe na hajawahi kuwa na michepuko

Malkia akataka kuhusika na siasa za nchi jamaa alikataa kabisa malkia akaanza vimba kichwa jamaa akaanza mpiga matukio .

Akanza kula ma court maid ,akataka kuoa malkia mpya ,familia ya malkia ikaanza onjeshwa joto ya jiwe

Mwisho wa siku malkia akalegeza mwenyewe

Mafahari mawili hawakai zizi moja hata siku moja

Mwanaume hagawani madaraka na mwanamke hata siku moja.

Hizo 50/50 campaign ni kelele tu ila uhalisia mwanaume atasimama mahala pake maana ameumbwa kuwa kiongozi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom