Hatimaye Mbowe apewa dhamana

Hatimaye Mbowe apewa dhamana

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
Watu wamezuiliwa kuingia mahakamani, Lema analumbana nao anawauliza ni sheria ipi inayozuia watu kuingia mahakamani kusikiliza kesi?

Muda si mrefu tutajua kinachojiri humu ndani.

================
FINAL UPDATE:

Kesi imeahirishwa, Mbowe kaachiwa kwa dhamana.

Mdhamini wa sasa wa Mbowe ni John Bayo diwani wa kata ya Elerai baada ya yule wa kwanza kuwa na kesi na yeye hivyo kesi zilikuwa zinagongana..
 
Naam, Mbowe kashafikishwa hapa Arusha mahakama kuu
 
Crashwise! Sipo mbali kuingia hapa mtaa wa uzunguni palipo mahakama kuu! Nitakupataje tuwe pamoja? Jb pls!
 
bado watu wamezuiriwe kuingia mahakamani..
 
kwa haraka haraka kuna zaidi ya polisi ya 70 na magari ya polisi zaidi ya 10..na muona wenje, halima,lema, akonai na wabunge wa viti maalum zaidi ya 7
 
wanaoruhusiwa kuingia ni wale wanaokuja na gari..
 
ZITTO KABWE ameingia anashangiliwa na wana CDM..
 
huku ndani parking imejaa hivyo watu wanaekujana na magari wanashauriwa kupaki nje..
 
Kwa mujibu wa Novatus Makunga aliyekuwa anairopotia ITV hivi punde kile kinachoendelea Arusha nikwamba Mbowe ndo anaingizwa katika chumba cha Mahakama khali iliyomfanya ahairishe kuripoti ili aendelee kufuatilia kinachoendelea.
 
watu wanazidi kuingia na waoga wametanda nje..
 
Freeman Mbowe ameshafikishwa Mahakama ya Arusha asubuhii chini ya ulinzi Mkali! Atapandishwa kizimbani mda wowote kuanzia sasa! Hali nje ya mahakama iko shwari kabisa na hakuna vurugu zozote! Habari zinasema amesafirishwa usiku saa 7 usiku kutoka Dar!
 
Apewe dhamana kama raia wengine kupunguza mvutano. Ni haki yake ya kikatiba
 
Aaaaagh!!! Inauma, inakera na inasikitisha kwakweli.
 
Back
Top Bottom