Hatimaye Mbowe amepona, yote yaliyopita yamebatilishwa

Naona Makonda amechukia kweli kweli kuvurugiwa.Sasa majibu mashtaka ya shule za Dar kushindwa kuperform
Asichukie kwanza asubirie kwanza mapepo ya gwajima haalafu na kesi mbowe aliyosema atamfungulia na kusema "its personal".
 
Vita dhidi ya madawa ya kulevya sasa imekabidhiwa kwa wahusika. Imechukuliwa rasmi na Kamisheni maalum inayoshughulika na madawa ya kulevya. Kamishna Mkuu wa Kamisheni husika amekaa front kama inavyompasa

Kutokana na kukoma kwa kutaja na kuita Central Police,ni wazi kuwa kilichofanyika kabla ya leo kilikuwa kinyume cha utaratibu na sheria. Ya Makonda yamebatilishwa leo rasmi. Mbowe amepona. Yote yamekoma leo,mapya yameanza leo.

Zile filamu za kuingia scene na TID halafu kutuonesha leo na zile za akina Gwajima na Wema zimefika tamati. Mapambano sasa yamempata mwenyewe na aliyekuwa anakosea amekiri kwa kukabidhi majina badala ya kuyataja na kuwaita watajwa.

Watanzania tulio wengi tunaunga mkono kutokomezwa kwa madawa ya kulevya nchini. Lakini,hatuungi mkono ukiukwaji wa taratibu na sheria. Sasa,upele umempata mkunaji

Mwafaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
mzee Tupa Tupa upo sahihi kabisaaa
 
Hivi mnavyojadiri na comments hizi mlimuelewa Makonda?
Amesema kuna katika list ya watu 164 kuna watu 46 hawajareport wanatakiwa watafutwe na wakamatwe hiyo ni pamoja na Mbowe,
Pia aliongea kwa kejeri kuwa kuna mtu alisema Makonda hawezi kuniita ni mtoto mdogo kwangu, akasema sasa tutajua shimoni ni wapi na ataniuliza nina miaka mingapi? Huo ni ujumbe kwa Mbowe.
 
Huyu RC hakosi vituko, atakuja tu na episode nyingine. Lakini tukiweka mbali madhaifu yake Kama binadamu, anaweza akaja kuwa kiongozi mzuri Sana siku za usoni akiamua kutulia na kujifunza.

Na inaonekana anatafuta sana mianya ya vufungu vya katiba na sheria ili aweze kumwagia mafuta ya taa kwenye mashimo ili agonge kila aina ya nyoka.
 
Hivi mnavyojadiri na comments hizi mlimuelewa Makonda?
Amesema kuna katika list ya watu 164 kuna watu 46 hawajareport wanatakiwa watafutwe na wakamatwe hiyo ni pamoja na Mbowe,
Pia aliongea kwa kejeri kuwa kuna mtu alisema Makonda hawezi kuniita ni mtoto mdogo kwangu, akasema sasa tutajua shimoni ni wapi na ataniuliza nina miaka mingapi? Huo ni ujumbe kwa Mbowe.
ndio jioni yake sasa commisioner akasema sheria lazima ifuatwe??? je unajua sheria gani alimaanisha??? pia alisema huwezi mtaja mtu bila ushahidi je makonda ana ushahidi juu ya mbowe??? kumbuka siro kasema hakuna ushahidi wa watu zaidi ya 80 walioitwa kuja kituo cha polisi cha kati??

Sitegemei jipya serikali ya ccm kuhusu kupinga madawa ya kulevya ila at least huyu commisisoner general anaonyesha matumani kuliko makonda mtafuta kiki.

USHAHIDI KWANZA NDIO UTANGAZE
 
Huyu RC hakosi vituko, atakuja tu na episode nyingine. Lakini tukiweka mbali madhaifu yake Kama binadamu, anaweza akaja kuwa kiongozi mzuri Sana siku za usoni akiamua kutulia na kujifunza.

Ni kweli anatakiwa kuacha papara ajifunze kwanza..anajiharibia sana
 
Baada ya madawa kuingia kwenye mikono ya wataalamu waliosomea intelijensia namshauri Mako ahangaike na yafuatayo;
Elimu,kuhakikisha shule zinamiundombinu bora kuchagiza ufaulu uloshuka sana.
Usafi na mazingira,kuhakikisha Dar linakuwa jiji safi na masoko yawe safi yenye vyoo na utaratibu nzuri wa kuhifadhi bidhaa na taka sehemu tofauti.
Ajira kwa vijana,walemavu na wajane,ili kupunguza wizi,ombaomba na machangudoa angebuni Namna ya kuanzishwa viwanda kidogo vitoe ajira kwakulink na nchi kama China waliobora kwaviwanda vidogo mf kutengeneza tishu,vyombo Vya plastick,Viatu,furniture na vitu Vya maofisini,kalamu,daftari,chaki nk.
Hapo atakua kajiweka kwenye eneo lililoachwa lakini lenye umuhimu Mkubwa.
Nivema afanye ujasiriamali kuliko ujasiriavita na watu mwishowe akakwama mf Ombaomba,mashooo,machinga nk
 
Mbowe yupo katika wale 65 ambao majina yao yalitajwa ya hayakukabidhiwa kwa kamishna!

Utaratibu mpya utaanza na hayo 97 ambayo kamishna kakabidhiwa rasmi!

Hivyo asifikiri swala la kwenda central linaepukika! Aende tu!
 
Hivi katibu wa bunge anachaguliwa/kuteuliwa na nani? Mbona wabunge wakipitisha maazimio inaelekea kuna ka mkwamo mahali fulani!
 
Vita dhidi ya madawa ya kulevya sasa imekabidhiwa kwa wahusika. Imechukuliwa rasmi na Kamisheni maalum inayoshughulika na madawa ya kulevya. Kamishna Mkuu wa Kamisheni husika amekaa front kama inavyompasa

Kutokana na kukoma kwa kutaja na kuita Central Police,ni wazi kuwa kilichofanyika kabla ya leo kilikuwa kinyume cha utaratibu na sheria. Ya Makonda yamebatilishwa leo rasmi. Mbowe amepona. Yote yamekoma leo,mapya yameanza leo.

Zile filamu za kuingia scene na TID halafu kutuonesha leo na zile za akina Gwajima na Wema zimefika tamati. Mapambano sasa yamempata mwenyewe na aliyekuwa anakosea amekiri kwa kukabidhi majina badala ya kuyataja na kuwaita watajwa.

Watanzania tulio wengi tunaunga mkono kutokomezwa kwa madawa ya kulevya nchini. Lakini,hatuungi mkono ukiukwaji wa taratibu na sheria. Sasa,upele umempata mkunaji

Mwafaaaa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Tangu lini chama kikapinga Madawa? Mmmh
 
Back
Top Bottom