Hatimaye Libya yawa shamba la Bibi, officially

Ndio demokrasia waliokuwa wanaitaka, eti Uhuru Wa kuongea.. Haya sasa hayupo Gaddafi ongeeni sasa na huo Uhuru mnaoutaka.

Waafrica bado hawajui nini wanakitaka, bado na huku Tanzania kuna jitu linazunguka huko ulaya kwa kisingizio za kuitafuta haki ndani ya Tanzania eti Tanzania kuna udikteta na wajinga wachache wanaliunga mkono pasipokujua kuwa anafanya hayo kwa maslahi yake.
 
Inauma lakini tatizo kubwa la viongozi wa ki Africa na hata za ki Arab ni kung'ang'ania madarakani kwa njia moja ama nyingine.

Huwezi kuwatawala watu wenye akili na ufahamu kwa zaidi ya miaka 42 na bado ukataka mwanao akurithi !!. Watakufanyia fitna tu.
.... watetezi wa Gadafi hawaoni hilo! Tena ukitawala kwa mkono wa chuma ukiwapoteza wenye mawazo tofauti; ni lazima fitna zitaingia tu no matter unatoa huduma bora za kijamii kwa kiwango gani. Hicho ndicho kiini cha tatizo ...
 
Tusijifiche kwenye kiongozi bora au chama bora. Utaratibu ukiwepo wa kupokezana madaraka uheshimiwe .

Mataifa yenye maendeleo endelevu ni yale ya kidemocrasia. Kabla kiongozi hajawaza kuwa mungumtu apumzishwe.
Mataifa yenye maendeleo endelevu ni yenye demokrasia? Unatuojaje aise. China? Russia? Monarch in europe countries. USA wenyewe wanasema wameibiana kura. Afu unakuja kutudanganya hapa live live
 
Nasisitiza kuwa lengo la Ghadafi kuvamiwa sio hoja ya demokrasia, wakubwa hawakunyonya mafuta bure. Mbona Saud Arabia hakuna hiyo demokrasia? Kwa nini wasiwavamie sasa wapeleke hiyo demokrasia?
Mbona Venezuela Wana demokrasia nzuri tu, kwa nn wanamsumbua Madulo?
Mbona hawamvamii M7?
Kama wanakupa kwako wanapiga kimya tu.
Africa tuamke
Hapa kwetu Tanzania tangu 95 Multipartism imefeli vibaya. Vyama kibao vya kijinga tupu. Kwa nini tusiamue sisi wenyewe kuwa na vyama viwili tu Tena kikatiba halafu tukapambana kwa hoja na kukubali kubadilisha madaraka kwa amani?
 
Tukubali tu kuwa watu wenye asili ya kiarabu uongozi wa kifalme ndo njia sahihi, wangeuboresha tu Basi,mfano angalia Iraq demokrasia wapi na wapi?
Ni kweli Ghadafi alikaa sana madarakani, na Hawa wazungu hawajamtoa kisa demokrsia, sio, he was a big threat to their economic interests.
Huoni walivyo muua demokrasia iko wapi?
Wenye maono ya kitaifa wanataka kiongozi bora na sio uchaguzi wa Kila Mara. China wamepata mwamba Xi na Ususi wamepamata mtaalamu Vladimir Putin
Linganisha hao na sisi ambao Kila Mara tunawaza uchaguzi hamna kitu
mbona china na russia hakuna aliyemaliza hata miaka kumi kama raisi? hata magu afanye mema gani akitaka kubadili ukomo wa uongozi ataharibu kila kitu, sisi hatupo katika mifumo hiyo. sisi waswahili husema 'tenda wema uende zako'
 
Hapo ndipo ukweli huwa hausemwi, ukiwa km kiongozi lazima usome nyakati na unachokijenga ili kiwe faida kwa wengine lazma kuwe na kiasi. Binadamu ni mtu asiyerizika kwa hiyo watu walibya waliamini wangepata zaidi na haiwezekani mtu mmoja aongoze nchi kwa zaidi ya miaka arobaini na bado anataka kurithisha mtoto. Gadafi ilibidi aachie madaraka pale alipoanza kuona upingamizi juu yake ampe madaraka kwa mtu mwingine aliyemuamini hata km ingekuwa kwa sanduku la kura then baadae uwezekano wa mwanae kupata uraisi ungeweza kuja na heshima yake ingebaki na nchi ingekuwa salama. Lakini kushupaza shingo akakosa vyote uhai na utajiri wa nchi.
Hivi hapo wa kulaumiwa ni nani? ni Gadafi kung'ang'ania madaraka au hao waliyokinukisha kwa wao nao pia kutaka madaraka?
 
Tusijifiche kwenye kiongozi bora au chama bora. Utaratibu ukiwepo wa kupokezana madaraka uheshimiwe .

Mataifa yenye maendeleo endelevu ni yale ya kidemocrasia. Kabla kiongozi hajawaza kuwa mungumtu apumzishwe.
kwanza:-LIBYA iliwahi kua namfumo wakupokezana madaraka lini ?!

pili:-kwani nilazima dunia kila taifa lifuate mifumo inayofuatwa nawamagharibi wakati nimataifa yalio huru sovereign state

tatu:-usiseme mataifa Mengi ama makubwa lisemee taifa lako linalofuata demokrasia lilikua namaendeleo gani ambalo halikua likiongoza demokrasia kama LIBYA ile ya Canal ?!

nne:- mbna mataifa ambayo ya SAUDIA QATAR UAE yanafuata Mifumo kama yailokua LIBYA ya GADAFI lakini bado US navibaraka wake ndio wanashirikiana nao ama wale sio madikteita ?!



Mwisho:-muache kujazwa ujinga(sio tusi)kwakigezo chademokrasia isioeleweka inayosimamiwa nakupigiwa chapuo na US navibaraka wake wakat wao wenyewe wanafiq tu
 
Tusijifiche kwenye kiongozi bora au chama bora. Utaratibu ukiwepo wa kupokezana madaraka uheshimiwe .

Mataifa yenye maendeleo endelevu ni yale ya kidemocrasia. Kabla kiongozi hajawaza kuwa mungumtu apumzishwe.
Ila duniani kuna vitu vya ajabu sana,yani kwamba wananchi Libya wameona bora waingize nchi vitani kwa sababu ya Gadaffi hataki kuwaachi nafasi na wenzake nao watawale walibya.

Yani kama Tz wananchi tuingize nchi vitani kwa sababu tunataka ccm itoke madarakani imekaa sana hivyo ni zamu ya Chadema au Act nao watutawale.
 
Inauma lakini tatizo kubwa la viongozi wa ki Africa na hata za ki Arab ni kung'ang'ania madarakani kwa njia moja ama nyingine.

Huwezi kuwatawala watu wenye akili na ufahamu kwa zaidi ya miaka 42 na bado ukataka mwanao akurithi !!. Watakufanyia fitna tu.
Mkuu umekuwa brainwashed kwani malkia Wa uingereza yeye amekaa miaka mingapi madarakani. Pia sio lazima kinachopitishwa na wamagharibi ndo kiwe SI unit ya maisha ya wengine. Binafsi uchaguzi unaofanywa ni kupoteza tu Hela bora hizo Hela zingeenda kufanya mambo mengine ya maendeleo ama watu wa campaign na Ku poll electronically
 
Sasa wanatawaliwa kwamkono wa mafuta siwanaona wanavyoinjoy maisha.!?
Factbox: Gaddafi rule marked by abuses ...

1970s - ARRESTS, TELEVISED HANGINGS

Rights groups and Gaddafi’s foes say that throughout the 1970s police and security forces arrested hundreds of Libyans who opposed, or who the authorities feared could oppose, his rule.

Student demonstrations were put down violently. Political opponents were arrested and imprisoned, or simply disappeared.

Police and security forces rounded up academics, lawyers, students, journalists, Trotskyists, communists, members of the Muslim Brotherhood and others considered “enemies of the revolution,” Human Rights Watch says. Gaddafi warned anyone who tried to organize politically they would face repression.

“I could at any moment send them to the People’s Court ... and the People’s Court will issue a sentence of death based on this law, because execution is the fate of anyone who forms a political party,” Gaddafi said in a speech on November 9, 1974.

A number of televised public hangings and mutilations of political opponents followed, rights groups say.

In 1976 Gaddafi authorized the execution of 22 officers who had participated in an attempted coup the previous year, in addition to the execution of several civilians, rights activist Mohamed Eljahmi has written.

1980s: DETENTION, DISAPPEARANCES

In 1980 authorities introduced a policy of extrajudicial executions of political opponents abroad, termed “stray dogs.”

According to a 2009 article in Forbes magazine by rights activist Eljahmi, Gaddafi’s then deputy Abdel Salam Jalloud issued a public justification in 1980 for the assassination of dissidents abroad, telling Italian media:

“Many people who fled abroad took with them goods belonging to the Libyan people ... Now they are putting their illicit gains at the disposal of the opposition led by (then Egyptian leader Anwar) Sadat, world imperialism, and Israel.”

A failed coup attempt in May 1984 apparently mounted by exiles with internal support led to the imprisonment of thousands of people. An unknown number of people were executed.

In 1988 there was a period which appeared to herald important human rights reforms. Authorities freed hundreds of political prisoners in a wide-ranging amnesty.
 
-Libya ile nchi iliyokuwa mfano kwa nchi za Afrika.
-Libya iliwahi kuwa nchi tajiri zaidi barani Afrika.
-Libya nchi iliyokuwa ikitegemewa katika bajeti ya AU.
-Libya ndo nchi pekee iliyowahi kuwekeza ndani ya bara la Afrika zaidi ya dola billioni 200 katika kipindi kifupi.
-Libya ndio nchi ambayo ilikuwa kimbilio la watu weusi wa nchi za Afrika Magharibi hasa WaNigeria katika harakati za kutafuta unafuu wa maisha.
-Libya ndio nchi iliyosaidia nchi za Afrika kupunguza gharama za kupiga simu, kutuma sms, na intaneti . Libya ilifanya hivyo kwa kununua satellite kwa niaba ya bara zima la Afrika kabla hapo nchi za Afrika zilikuwa nchi za ulaya mamilioni ya Euro kila mwaka.

Lakini toka kupinduliwa kwa utawala wa Muammar Gadaffi mwaka 2011 nchi ya Libya imebaki kuwa uwanja wa mapambano, soko la biashara haramu, huba ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mpaka sasa June 2020 , Ndani ya ardhi ya Libya kuna majeshi ya Saudi Arabia, UAE, Misri , Qatar , Urusi na Uturuki kila mmoja akipambana kuweka kiongozi atakayeendana na maslahi yao.

Hili ni funzo kwa nchi za KiAfrika kuwa makini sana na ushauri wanaopokea kutoka nje, miaka 10 tu iliyopita wananchi wa Libya waliishi kama wafalme.

1)Maji bure 2)Umeme bure 3) Bei ya Mafuta ilikuwa sawa na tshs 200 kwa litre 4)Hamna kodi ya nyumba 5)Elimu bure hadi chuo kikuu na kwa wale waliopendelea kusoma nje pia walilipiwa na serikali 6) Serikali ya Libya ilitoa takribani $ 60,000 karibu milioni 150 kwa kila wanandoa wapya ikiwa ni pesa ya kuanzia maisha.
7) Mwanamke aliyejifungua alipewa dola 5,000
8) Pia endapo mlibya atapata tatizo la kiafya ambalo haliwezi tibika nchini kwake alilipiwa gharama zote za matibabu nje ya nchi na Serikali.
9) Libya ndo nchi iliyokuwa na reserve Kubwa barani Afrika na haikuwa na deni la hata senti. Reserve ya Libya ilikuwa Dola Bilioni 150. N.K.

Libya kabla ya kifo cha Gadaffi .....

View attachment 1486154View attachment 1486155View attachment 1486156View attachment 1486157View attachment 1486158View attachment 1486155View attachment 1486156View attachment 1486157View attachment 1486158
Libya baada ya Gadaffi

View attachment 1486160View attachment 1486161View attachment 1486162View attachment 1486163View attachment 1486164View attachment 1486165View attachment 1486166View attachment 1486167View attachment 1486168




HIYO NDO EFFECTS YA KUWA NA MBABE WA KIVITA KAMA KHALIFA HAFTAR
 
Hapo ndipo ukweli huwa hausemwi, ukiwa km kiongozi lazima usome nyakati na unachokijenga ili kiwe faida kwa wengine lazma kuwe na kiasi. Binadamu ni mtu asiyerizika kwa hiyo watu walibya waliamini wangepata zaidi na haiwezekani mtu mmoja aongoze nchi kwa zaidi ya miaka arobaini na bado anataka kurithisha mtoto. Gadafi ilibidi aachie madaraka pale alipoanza kuona upingamizi juu yake ampe madaraka kwa mtu mwingine aliyemuamini hata km ingekuwa kwa sanduku la kura then baadae uwezekano wa mwanae kupata uraisi ungeweza kuja na heshima yake ingebaki na nchi ingekuwa salama. Lakini kushupaza shingo akakosa vyote uhai na utajiri wa nchi.
Exactly mkuu! Alipofushwa na madaraka. Akafa kifo cha aibu.
 
Back
Top Bottom