Hatimaye Julius Malema atia neno kuhusu Magufuli

Hatimaye Julius Malema atia neno kuhusu Magufuli

Ahsante sana kwa kuyapuuza mapinzani ya Tanzania Dunia inaona Wapinzani wa Tanzania hawaoni kazi nzuri ya Rais wetu
 
Tunaoishi Tanzania tunamfahamu na tunayafahamu anayoyafanya kuliko mtu mwingine yeyote. Ni aheri maneno hayo yangetoka kwa Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania maana huyo anaona mema na mabaya yote yanayotokea nchini mwetu.
Kwahiyo Lissu anapoteza muda huko Ulaya!! Safi sana hii!
 
Tunapokea pongezi za Malema ambaye ni kiongozi wa chama maarufu cha upinzani cha Economic Freedom Fighters EFF. Malema ndiye Lissu w Afrika Kusini. Huku Lissu wetu tumemvua mpaka ubunge na kumtelekeza huko nje akihudumiwa na mabeberu.
Kama Lisu na Malema wanafanana kwa itikadi, tusaidie sababu zinazofanya Lisu asione jema katika vitendo vya Magufuli.

Naamini upizani wa lisu hauna uzalendo ndani yake.
 
tatizo hupendi. kusikia mawazo tofauti jomba, utakufa na kihoro, ukweli ni ukweli tuu hata ufanyeje..hahahah ngazi ya chini ndio ipi..basi wewe wa ngazi ya juu ungetoka humu utuachie sisi jonba..tafuta kwingine
Mtu akisoma niliyoandika mimi na uliyoandika wewe atajua bila ya shaka yoyote ni nani kati yangu na wewe "atakufa kwa kihoro" hili lipo wazi hata katika maandishi tu yaliyowekwa hapa.
 


Hii ni Mara ya kwanza kwa kiongozi machachari na kijana wa Afrika Kusini, Julius Malema kutia neno lolote kuhusu rais Magufuli.

Kwa muda mrefu amekuwa akifuatilia siasa za ukanda huu wa Afrika Mashariki na mara nyingi amekuwa akimkosoa sana rais wa Uganda, Yoweri Museveni na kumuunga mkono Bobi Wine, lakini hajawahi kushughulika sana na siasa za Tanzania.

Uvumilivu umemshinda baada ya kusikia mengi, hasa kitendo cha Magufuli kukataa masharti ya wachina katika mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

Katika "account" yake ya Twitter, amempongeza Magufuli kwa uamuzi wake huo. Hongera sana Magufuli.
Malema ni mpuuzi kama wapuuzi wengine. Huyu atakuwa dictator kama magu
 
Back
Top Bottom