joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Hii ni Mara ya kwanza kwa kiongozi machachari na kijana wa Afrika Kusini, Julius Malema kutia neno lolote kuhusu rais Magufuli.
Kwa muda mrefu amekuwa akifuatilia siasa za ukanda huu wa Afrika Mashariki na mara nyingi amekuwa akimkosoa sana rais wa Uganda, Yoweri Museveni na kumuunga mkono Bobi Wine, lakini hajawahi kushughulika sana na siasa za Tanzania.
Uvumilivu umemshinda baada ya kusikia mengi, hasa kitendo cha Magufuli kukataa masharti ya wachina katika mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.
Katika "account" yake ya Twitter, amempongeza Magufuli kwa uamuzi wake huo. Hongera sana Magufuli.