Hatimaye Easy Tv yazikwa rasmi

ridculouz

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
910
495
Wale wachina wamiliki wa king'amuzi cha Easy tv wameshindwa kuenenda na kasi mpya ya Magufuli .

Ukiacha idadi kubwa ya wateja kuwa kukimbia, lakini walikuwepo wateja wachache waliolishwa limbwata la kichina kutokana na baadhi yao kupenda movie sana na baadhi ya chanel za dini.

Lakini hali imebadilika mwezi huu baada ya king'amuzi chao kukata kabisa chanel zote . Nadhani umefika muda muafaka wateja waaminifu wa Easy kujiunga na Startimes tu maana hakuna namna ingine .

Historia yao

Easy Tv ni kampuni ya wachina iliyojihusisha na huduma ya ving'amuzi ki wizi wizi maana sidhani kama walikuwa wanalipa zile chanel .

Walianza kutoa huduma mwaka 2009 wakitanguliwa na wakongwe Dstv baadae ndoo wakaja Startimes na wengine.

Huduma yao ilikuwa unalipa 9,000 baadae ikapanda mpaka 11,000 lakini ulikuw huwezi kupata voucher mpaka umpigie mfanyakazi wao akuunganishe moja kwa moja ila ilibidi utume 12,000 pamoja na ya kutolea .

Asanteni sana .

By Ridculouz

Mmoja kati walioshishwa limbwata na wachina, ambae ana haha ahamie wapi baada ya Easy kupotea kabisa.
 
Back
Top Bottom