Hatimaye Dk. Juma Mwaka ajisalimisha Polisi

Hatimaye Dk. Juma Mwaka ajisalimisha Polisi

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,715
Reaction score
59,244
Jeshi la polisi limefanikiwa kumtia nguvuni tabibu Juma Mwaka, maarufu Kama Dokta Mwaka, baada ya kumsaka Kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Polisi yasema mmiliki wa Foreplan Clinic tabibu Juma Mwaka amejisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi Dar leo, atakiwa kurudi kesho kwa mahojiano.

Jeshi la polisi linatekeleza agizo la Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuwa tabibu huyo mashuhuri akamatwe Kwa kukiuka agizo la Serikali la kuacha kutoa huduma za tiba asili na tiba mbadala baada ya kufutiwa kibali na Baraza la tiba asili na tiba mbadala, ambao walimkuta na hatia ya kukiuka masharti ya sheria ya tiba asili na tiba mbadala ya Mwaka 2002, sheria namba 23, ulaghai wa kujiita dokta na kujifanya amesomea tiba ya kisasa kumbe la, kukutwa na shehena ya dawa za kisasa zaidi ya boksi 200 bila vibali vya mamlaka ya chakula na dawa, TFDA na kukutwa na shehena ya dawa za tiba asili na tiba mbadala kinyume cha sheria, haswa baada ya kufutiwa usajili wa kutoa huduma hizo.

Tabibu Mwaka alikuwa Polisi Kwa mahojiano katika kituo cha kati.
 
Mungu pekee ndiye anajua nchi hii inaelekea wapi!!
Mungu ni mkuu sana hatotuacha tutumbukie shimoni..

Tukeshe tukiomba before things get out of hand.!!!
 
ambao hawakumuelewaa TL wasubiri pale makatibu kata watakapotoa amri za kuwekwa vizuizini bila maelezo!
 
Hizi tiba asili Ni muda muafaka sasa zipigwe kabisa marufuku kufanyiwa marketing kwa hali zote, na hadi mtu ahitinu mafunzo fulani, hata Kama Ni ya uchawi na kugagua......
Kwa nchi iliyojaa wajinga wengi Ni jukumu la serikali kuwalinda wananchi wake na walaghai.
Pamoja Na tofauti zangu za kisiasa Ila kwa hili namuunga Dr Kigws mkono
 
d31af8f450522495d828eac335b39b28.jpg
uku wamewema kajisalimisha na kesho atarudi kwa mahojiano.
 
Hizi tiba asili Ni muda muafaka sasa zipigwe kabisa marufuku kufanyiwa marketing kwa hali zote, na hadi mtu ahitinu mafunzo fulani, hata Kama Ni ya uchawi na kugagua......
Kwa nchi iliyojaa wajinga wengi Ni jukumu la serikali kuwalinda wananchi wake na walaghai.
Pamoja Na tofauti zangu za kisiasa Ila kwa hi
li namuunga Dr Kigws mkono
Aanzeni na baby wa loliondooo,maana hata magu alienda kunywa kikombe
 
Back
Top Bottom