QALLI MIZOH
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 2,075
- 699
shughuli ipo kwa wanaopenda vya rejareja... pole kaka jombii itabid xaxa utafute ka dogodogo.
ni ukweli ulioje!!! kama pako pananuka anza kusafisha kwako ndipo uendekwengine...OFM}Hili jambo mi naona halizungumzwi katika mawanda yanayostahili. Danguro hilo lilikuwa nyuma ya ukuta wa Dar live, ukumbi unaomilikiwa na ndg Erick Shigongo ambaye anamiliki utitiri wa magazeti hapa nchini. Ni dhahiri kuwa biashara hiyo ilifikia kileleni mara tu ukumbi huo ulipoanzishwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu eneo hilo nyakati za usiku. Magazeti ya huyu jamaa yapo kwenye OPERESHENI FICHUA MAOVU (OFM). Na mara nyingi waandishi wa magazeti hayo hupatikana katika ukumbi ule sasa kwanini hawakuwahi kufichua maovu yanayotendeka upenuni mwa ukumbi wao? Wanahaha kufichua ufuska unaofanyika vyumbani mwa watu ile wanauacha unaofanyika hadharani tena upenuni mwa eneo lao. Hawa watu ni wanafiki sana. Nahisi ni vyema hii ishu iishe katika hali ambayo Shigongo atabaki na majeraha ili awe na weledi katika kazi za magazeti yake.
Mbunge Ndugulile huyu huyu tunayewinda nae ma-babies kila siku au mwingine? Kweli mtu asiye mnafiki hawezi siasa za Bongo!
Ni kweli usemayo lakini issue zinapatikanaje hizo huduma, hata hiyo miaka ya nyuma ulinayosema ilikuwa ni kwa wale ambao wapo interested ndio walijua wapi na nyumba gani lakini kwa tukio hili mtu yoyote tu akiamua anatia timu kwa kuwa kila kitu kilikuwa hadharaniNgono zembe zilikuwepo tangu waqt wa mkoloni waqt huo dada poa wakiitwa WAHAYA. Sio rahisi kkukomesha hii biashara ila inaweza ikadhibitiwa isifanywe kizembe. Tatizo viongozi wetu wengi wanapenda uroda lkn hawako tayari kukubali hilo hadharani
dawa yenu ameangalia kwa jicho la mbali, huenda walikuwa wanapotezea tu maana biashara hiyo ina link na kile wanachokifanya yaani kama wangefanya OFM maana yake wateja wao wangewapoteza. Kumbe na wao waoga aiseeni ukweli ulioje!!! kama pako pananuka anza kusafisha kwako ndipo uendekwengine...OFM}
nimejaribu kuwaza nje ya kiboksi kwamba kondomu ndoo tatu its serious protection.View attachment 152425View attachment 152425View attachment 152425
Ndoo tatu zilizojaa condom daily zilikuwa zinakusanywa
Ngono zembe zipo wakati wote na popote lakini si hadharani. Huko mafichoni wanakojua wenyewe waachwe na hakuna anayewafuatilia huko. Lakini hili la hadharani kama wapo kwenye vilabu vya pombe huku watoto wakishuhudia, hapana. Mbaya zaidi habari zinasema wateja wakubwa walikuwa ni vijana chini ya umri wa miaka 18. Napongeza hatua waliyofanya. Kujipanga msitari kweupe kana kwamba wanaenda kupakuliwa bakuli la maharage? Hili la ukusanyaji wa ndoo tatu za condom kila siku inaonyesha dalili ya kilichokuwa kinaendelea hapo, ni sodoma haswa.
Jaribu kutofautisha, mbunge huyo alikuwa mteja hapo danguroni palipokuwa panafanyika ufuska? Mambo binafsi ya sirini hayatuhusu, jadili kilicholetwa.
Sitatofautisha hata kidogo. Ufuska ni ufuska haijalishi umefanyika Mabagala au Dodoma wakati wa kipindi cha bunge au hotel ya nyota tano! Ebo! Unafiki wa mwafrika huu!
Kujamihiana ni nature, kuna wenye makubaliano ya kuwa wapenzi na pengine wachumba hadi kufikia kuwa mwili mmoja. Hata hivyo katika jamii uwepo wa wanaofanya mahusiano upo kila leo na kwa kiwango kikubwa, jambo la msingi hufanya katika faragha zao wawili zisizoweza kuwa wazi kwa kila mpita njia.
Pale inapotokea kufanyika kwa uwazi kama ilivyotokea Zakhem - Mbagala ni hali ya kujishusha kwa binadamu kuwa sawa na wanyama wa kawaida wasiokuwa na utashi kama utashi wa binadamu. Kilichoendelea pale Zakhem ni sawa na wanayama pori wasio na utashi ila kufuata tu misukumo ya silika zao bila kaungalia mazingira na makandokando yanayowazunguka katika jamii.
Pengine kilichotokea pale Zakhem ni kibaya kwa jamii na familia za maeneo hayo kuliko kinachoendelea kwa machangudoa wanaorandaranda mitaani na barabarani lakini mambo yao hufanyia mafichoni.