Hatimaye Chuo cha Madini Dodoma chapatiwa Mkuu Mpya

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Ni Dr. Mwachayeki (kama sija sikosei).

Kwa muda mrefu Chuo cha Madini Dodoma kimekuwa katika hali mbaya ya kiuongozi na kitaaluma kiasi kwamba kusoma kwenyewe kumekuwa ni kama kuchimba madini kwa nyundo. Na kwa sababu zinazoeleweka huko juu chuo hicho kilikuwa chini ya mtu anayekaimu nafasi iliyokaimiwa kwa muda mrefu. Tulipolichukua jambo hili mwishoni mwa mwaka jana tulielewa changamoto iliyopo na hasa kwa wanafunzi ambao wangependa kulitumia taifa lao katika chuo hicho. Hata hivyo, wakufunzi wake na mkuu wake wengi walikuwa ni wale wenye BA/BS na hivyo kutilia mashaka kama ni aina gani ya elimu inatolewa katika chuo hicho muhimu chenye kutengeneza makada wa ngazi za kati katika katika madini.

Pamoja na matatizo mengine ya kudumu kama ya malazi kwa wanafunzi chuo hiki kimesahauliwa sana - angalau kwa maoni ya baadhi ya walimu na wanafunzi pale - kiasi kwamba kuwa kama mtoto aliyesahauliwa.

Je sasa kiko njiani katika kuboreshwa? Je kinaweza kuinuliwa zaidi ili kiweze kutoa wataalamu wengi zaidi katika sekta hii muhimu ambayo bado inaajili "wataalamu" wengi kutoka nje kana kwamba nchini hawapo au hakuna mahali pa kujifunzia? Kwa sasa tutaangalia ni jinsi gani serikali inatenga fedha ya kuboresha chuo hiki katika bajeti inayokuja. Vinginevyo tutaendelea kutegemea wataalamu wengi kutoka nje wakati wengi wanaweza kupatikana nchini.
 
Madini na uchimbaji na utafutaji wa gesi na mafuta, unatakiwa utatuzi wa haraka wa namna ya kuwapata wataalamu wazalendo. Vinginevyo tusilaumiane maana wakujilaumu tutakuwa wenyewe. Hizi sector miaka michache ijayo zitakuwa na mchango mkubwa sana kwenye pato la Taifa. Sisi tumejiandaa vipi kushika hatamu? Au tutaendelea kusikiliza hadithi za wathungu wanaotubabaisha?
 
Sina knowledge kuhusu madini sana, sana sana nikiulizwa naweza kujibu kuwa madini mengi yanapatikana Tz, dhahabu, almasi, shaba, Tanzanite. Nasema hivi kwa sababu nimekaa Dodoma- Miyuji, ni km chache kutoka chuo tajwa... kwa miaka 8, lakini sijaona Tz inafaidika nini na haya madini, ni ufisadi kwa kwenda mbele.... sio kosa lao km mkuu wa kaya kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa...
 
Back
Top Bottom