Hatimaye Chibuda ca CDM Azinduka !

Wed

JF-Expert Member
Mar 7, 2011
315
266
John Shibuda, ameibuka na kutetea maandamano yanayofanywa na chama chake, huku akionya CCM kuacha kufanya kile alichokiita mchezo wa kugeuza polisi kuwa ‘ICU ya kutibu maradhi yake ya siasa za ufisadi.

Kukosekana kwa Shibuda katika maandamano na mikutano ya Chadema hata yalipotua mkoani kwake Shinyanga, kuliibua mguno wa chini chini miongoni mwa wapenzi na washabiki wa chama hicho.
Source : Gazeti la Mwananchi la leo

Wakuu, huyu " Shibuda" tunaweza kweli kumwamini au ni kauli "danganya toto" ???:A S 13:
 
Huyu anacheza kote kote si mtu wa kuamini hata kidogo. Sasa hivi ameona mafanikio makubwa ya maandamano ya CHADEMA kule kanda ya Ziwa basi ameamua kuwa mpiga debe mkubwa wa CHADEMA wakati katika kila kikao cha bunge hivi karibuni alirudi kuvaa magwanda yake ya CCM. Tusubiri tuone kama kweli Shibuda si pandikizi la CCM ndani ya CHADEMA ili kukivuruga chama hicho kinachokuja juu kwa kasi kubwa sana na hata kuwatia kiwewe viongozi wa juu wa CCM
 
Mtawajua kwa matendo yao.
The more anger towards the past you carry in your heart, the less capable you are of loving in the present- Barbara De Angelis
 
Shibuda,zito na selasini ni watu wa kuwaangalia kwa umakini km wana element za uccm vile. Ila itafahamika tu tunapoendelea na mapambano pumba na mchele vitajitenga!
 
John Shibuda, ameibuka na kutetea maandamano yanayofanywa na chama chake, huku akionya CCM kuacha kufanya kile alichokiita mchezo wa kugeuza polisi kuwa ICU ya kutibu maradhi yake ya siasa za ufisadi.

Kukosekana kwa Shibuda katika maandamano na mikutano ya Chadema hata yalipotua mkoani kwake Shinyanga, kuliibua mguno wa chini chini miongoni mwa wapenzi na washabiki wa chama hicho.
Source : Gazeti la Mwananchi la leo

Wakuu, huyu " Chibuda" tunaweza kweli kumwamini au ni kauli "danganya toto" ???:A S 13:

Na wewe ni nani anayekuamini! Tuache tabia za kitoto. Kama wewe humwamini kaa kimya siyo unaanza kumobilize wengine!
 
Anayengoja kuprove kama shibuda si feki na angoje.Sijui anangoja afanye au aseme nini zaidi!Kwa upande wangu Shibuda simwamini tena tokea siku alipowatukana cdm kwa mipasho bungeni!Yule ndo shibuda halisi huyu anayeongea hivi sasa anaigiza tu.Huwez kumlinganisha na Zito kwasababu angalau the latter anatofautiana na wenzake kwenye vikao vya kichama na anakuwa wazi ubaya ni akiexpose kwenye media.Lakini the former anaongea bungeni kama mwanaccm mzoefu na kusiliba vya kutosha chama kilichompa ubunge!!Sijawahi kuishuhudia kabla hypocrite aina ya Shibuda.Sisubiri nione,tayari nimeona kuwa John Magalle Shibuda ni pandikizi la ccm ndani ya cdm.
 
Naipenda CHADEMA kwa kuwa kila mwanachama yuko huru kuamua ushiriki wake katika kila jambo kwa dhamira yake. Ni utamaduni mpya ambao tunapaswa kuuenzi na kuuzoea. Wajifunze tu kuheshimu maamuzi ya vikao vyao halali.
 
Huyu bwana leo anaweza kuwa wa bluu, kesho mwekundu na keshokutwa wa kijani
 
Huyu bwana leo anaweza kuwa wa bluu, kesho mwekundu na keshokutwa wa kijani

Ni suala la muda tu, mbivu na mbichi zitajulikana. Ina maana kama ni kweli na yuko jikoni, anachukua kila kitu na kukiwasilisha upande wa pili.
 
Shibuda na Zitto wapo kimaslahi binafsi zaidi, shibuda kaona akina Sumaye na wanaharakati wengine wanaiponda CCM na kuisifia CDM wanataka kujiweka kama na yeye Mwana-Ukombozi. KWA TAARIFA YENU HAKUNA MWANA UKOMBOZI LEGE LEGE KAMA HAWA WAWILI AMBAYE ANAANGALIA NA KUSEMA LAKINI CCM WANAFANYA VIZURI, kama ni hivyo kwa nini usijiunge nao. Woote hawa kwenye historia ya ukombozi hawatakuwepo, Zitto alianza vizuri saana sasa tatizo ni umaskini na msimamo ni ngumu kama ngamia kuingia katika tundu la sindano, wakampa pesa akanyamaza.
 
Na wewe ni nani anayekuamini! Tuache tabia za kitoto. Kama wewe humwamini kaa kimya siyo unaanza kumobilize wengine!

Hizi ndizo tabia za CHADEMA za kutafuta CHEAP POPULARITY. Shibuda na Zitto wana shughuli za kufanya majimboni kwao wanakowakilisha siyo kuzurura tu mitaani kwa kisingizio cha maandamano. Kama mna uchungu na nchi hii wapelekeni mahakamani hao mnaowatuhumu siyo kutupigia kelele kila siku. Wanaume kama mabinti!!!!!!!!!!! Ovyooo!!!!!
 
Shibuda: ''Namfahamu JK kama Rais halali wa JM wa Tz''.....

Hata usipomfahamu JK kama Rais halali wa Tz bado JK anabaki kuwa Rais wa Tz.
Halali maana yake ni kwamba "Alitangazwa na NEC" kuwa mshindi.

Sasa tofauti inakuja kwamba Je, NEC walimtangaza mshindi halali??
Baadhi yetu tunaamini mshindi hakuwa JK, lakini chombo halali (NEC) kikampa urais.

Kwa habari ya Shibuda Magalle nawashauri CDM wamkubali kama alivyo, sasa mnataka wabunge wote wa CDM wawe kama Dada Regia au Mnyika hiyo diversity itatoka wapi?? Ruhusuni wenye kuthubutu kuongea wawepo ndani ya chama ili siku Dr. Slaa au Mbowe wakitoka bila nguo awepo wa kusema "mkuu leo umesahau kuvaa".
La muhimu wasimwingize kwenye nafasi nyeti za chama.
 
John Shibuda, ameibuka na kutetea maandamano yanayofanywa na chama chake, huku akionya CCM kuacha kufanya kile alichokiita mchezo wa kugeuza polisi kuwa ‘ICU ya kutibu maradhi yake ya siasa za ufisadi.

Kukosekana kwa Shibuda katika maandamano na mikutano ya Chadema hata yalipotua mkoani kwake Shinyanga, kuliibua mguno wa chini chini miongoni mwa wapenzi na washabiki wa chama hicho.
Source : Gazeti la Mwananchi la leo

Wakuu, huyu " Chibuda" tunaweza kweli kumwamini au ni kauli "danganya toto" ???:A S 13:

Someni alama za nyakati.
 
Naipenda CHADEMA kwa kuwa kila mwanachama yuko huru kuamua ushiriki wake katika kila jambo kwa dhamira yake. Ni utamaduni mpya ambao tunapaswa kuuenzi na kuuzoea. Wajifunze tu kuheshimu maamuzi ya vikao vyao halali.

Waangalie yasije kuwatokea ya Chacha Wangwe!!
 
John Shibuda, ameibuka na kutetea maandamano yanayofanywa na chama chake, huku akionya CCM kuacha kufanya kile alichokiita mchezo wa kugeuza polisi kuwa ‘ICU ya kutibu maradhi yake ya siasa za ufisadi.

Kukosekana kwa Shibuda katika maandamano na mikutano ya Chadema hata yalipotua mkoani kwake Shinyanga, kuliibua mguno wa chini chini miongoni mwa wapenzi na washabiki wa chama hicho.
Source : Gazeti la Mwananchi la leo

Wakuu, huyu " Chibuda" tunaweza kweli kumwamini au ni kauli "danganya toto" ???:A S 13:
Kwangu cha maana ni ujumbe alioutoa kwa chama tawala maana unaendana na hali halisi iliyopo nchini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom