Hatimaye Chibuda ca CDM Azinduka !

acha aseme ameshaona huu muelekeo hivyo simshangai,Karibu Kundini Shibuda...,
 
Shibuda na Zitto wapo kimaslahi binafsi zaidi, shibuda kaona akina Sumaye na wanaharakati wengine wanaiponda CCM na kuisifia CDM wanataka kujiweka kama na yeye Mwana-Ukombozi. KWA TAARIFA YENU HAKUNA MWANA UKOMBOZI LEGE LEGE KAMA HAWA WAWILI AMBAYE ANAANGALIA NA KUSEMA LAKINI CCM WANAFANYA VIZURI, kama ni hivyo kwa nini usijiunge nao. Woote hawa kwenye historia ya ukombozi hawatakuwepo, Zitto alianza vizuri saana sasa tatizo ni umaskini na msimamo ni ngumu kama ngamia kuingia katika tundu la sindano, wakampa pesa akanyamaza.

Kuna baadhi ya Wabunge CHADEMA hawapendi kuburuzwa buruzwa na kufuata hoja na mkumbo wa maamuzi ya viongozi wa juu bila kutafakari kama yana athari au laa kama walivyo wabunge wengi ndani ya chama.

Zitto na Shibuda ni mifano hai, hawa ndio wabunge mastaa (wakomavu wa kisiasa) ambao wamekuwa wanatofautiana na maamuzi ya Chama kwa mara nyingi tu, wakati wa kugomea hotuba ya Rais, Hata kwenye mikutano ya kanda ya ziwa na mambo mengine mengi tu.

Zitto na Shibuda HAWABURUZIKI kama walivyo wabunge wengi ndani ya CHADEMA, hii ndiyo tafsiri sahihi ya hawa watu wawili na ndiyo maana ni vigumu sana kuwaelewa misimamo yao, Wasituchanganye sisi washabiki na wapenzi wa chama hiki cha ukombozi.

Hawa ndiyo typical Zitto and SHIBUDA - mimi nafikiri CHADEMA inalijua hilo na wana CHADEMA msiwe na wasiwasi kabisa chama kipo IMARA.
 
Hata usipomfahamu JK kama Rais halali wa Tz bado JK anabaki kuwa Rais wa Tz.
Halali maana yake ni kwamba "Alitangazwa na NEC" kuwa mshindi.

Sasa tofauti inakuja kwamba Je, NEC walimtangaza mshindi halali??
Baadhi yetu tunaamini mshindi hakuwa JK, lakini chombo halali (NEC) kikampa urais.

Kwa habari ya Shibuda Magalle nawashauri CDM wamkubali kama alivyo, sasa mnataka wabunge wote wa CDM wawe kama Dada Regia au Mnyika hiyo diversity itatoka wapi?? Ruhusuni wenye kuthubutu kuongea wawepo ndani ya chama ili siku Dr. Slaa au Mbowe wakitoka bila nguo awepo wa kusema "mkuu leo umesahau kuvaa".
La muhimu wasimwingize kwenye nafasi nyeti za chama.


Ni sawasawa na kusema kwamba,binti amebakwa akapata mimba.Yule mtoto atakaezaliwa atapokelewa na jamii lakini jamii itaendelea kuhoji mchakato uliotumika kupata huyo mtoto
 
John Shibuda, ameibuka na kutetea maandamano yanayofanywa na chama chake, huku akionya CCM kuacha kufanya kile alichokiita mchezo wa kugeuza polisi kuwa ‘ICU ya kutibu maradhi yake ya siasa za ufisadi.

Kukosekana kwa Shibuda katika maandamano na mikutano ya Chadema hata yalipotua mkoani kwake Shinyanga, kuliibua mguno wa chini chini miongoni mwa wapenzi na washabiki wa chama hicho.
Source : Gazeti la Mwananchi la leo

Wakuu, huyu " Chibuda" tunaweza kweli kumwamini au ni kauli "danganya toto" ???:A S 13:

....ngoja tusome mchezo wake!!!!
 
Na wewe ni nani anayekuamini! Tuache tabia za kitoto. Kama wewe humwamini kaa kimya siyo unaanza kumobilize wengine!


Mkuu, Kama unazo taarifa tofauti naomba utupatie.

mimi bado nitabaki na msimamo wangu kwani :-
Tatizo ni kwamba hakuna taarifa yeyote iliyotolewa ni kwa nini hakushiriki kwenye maandamano tena yaliyofanyika mkoani mwake. Je huoni hapa kuna kitu ?? . Kweli Ugeni Mkubwa wa CDM unakwenda kufufua mapambano nyumbani kwake yeye asiwepo ??? Je aliogopa kushushwa kwenye jukwaa kama ilivyotokea Musoma ??? Au pia aliogopa moto ambao ungewashwa na CHADEMA ungemuunguza yeye pamoja na maswahiba wake wa chichiemu ???
: tafakari hili. :A S 13::A S 13:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom