Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Chato.
Chato town, population = 17,508. Chato district population = 365,000
Economic activitiy = nothing significant apart from subsistence farming which depend on rain. Contributes less than 1 percent to the GDP.
Tourist attractions = none

At the same time Songwe airport, the main airport serving the southern highlands, an area with more than 5 mil people and also being the bread basket of Tanzania doesn't have runway lights till today!

Mwanza airport yenyewe upanuzi wake has been going on at such a slow pace for the past 2 years and at times even stalled!

We are willing to spend billions on someone's vanity project ambayo will generates nothing in return and adds little value, lakini tunaache sehemu where the money would have been better spent.

A small airport would have been fine, lakini sio kujenga an airport with a runway that could almost "rival" JNIA, at a town/district with a population lower than some suburbs in Dar.

Someone needs to look at themself in the mirror and reevaluate the choices they have been making so far.
Punguza hasira kaka. Historia itakuumbua.

Nikutulize pia kwa kukupongeza kwa kuvikumbuka viwanja vya Mwanza na Mbeya. Ila nipingane na wewe kwa haya yafuatayo.

1. Kigezo cha idadi ya watu kiondoe kwenye equation utachekwa. Mara nyingi viwanja hujengwa mbali na miji na kunakuwa na mji mkubwa ndani ya kilomita 20 hadi 100.

Mfano nikuulize. Hivi walipoamua kujenga uwanja wa KIA hapo ulipo miji ya Moshi Arusha na Boma Ng'ombe ilikuwa na watu wangapi wakati huo. Kwa nini wasingepanua kiwanja cha moshi au cha arusha vilivyo kuwepo.

Je. Hadi leo miji ya Chato na Boma Ng'ombe wapi kuna watu wengi? Wilaya ya Siha na Chato ipi ina watu wengi?

2. Ujenzi wa uwanja wa chato ni muhimu na haujakwamisha wala kuzuia ujenzi wa viwanja vingine muhimu vya Mwanza Tabora Mpanda Mbeya Shinyanga Simiyu Mara Bukoba Kigoma Singida nk.

Kama hivyo vingine havijajengwa basi ama kuna sababu nzuri tu za kutokuvijenga au kuviboresha, ama kuna sababu mbaya au figisu figisu.

Ni jukumu letu kuonyesha umuhimu wa ujenzi au upanuzi wa hivyo viwanja vingine tunapojadili ujenzi wa kiwanja cha chato, na kupiga kelele hivyo viwanja navyo vijengwe. Kuliko kukashifu uwanja kujengwa chato.

Kuna tatizo gani kila walaya kuwa na kiwanja bora cha ndege kama kinalipa?

Mie namwomba JPM na serikali yake mkandarasi aliyeko chato akimaliza wampe mkataba aendelee pale Mugumu kuweka kiwanja cha kisasa maana jamaa anaonekana ni mtaalamu wa ujenzi maana anaweza kujenga hivi viwanja kwa muda mfupi.
 
nchi hii tumekuwa kama vultures ambavyo hugombania mzoga. kila mtu anataka kupeleka kwao. bahati mbaya mwenye nguvu anashinda hata kama hakuna maslahi. Martin Meredith aliandika kuwa, mashirika na viwanda vingi Afrika vilikufa sababu ya kujengwa kikanda na kufuata pride. hawakuangalia uchumi bali sifa. nashauri tukae chini tuone namna ya kugawana mzoga kwa usawa.
 
barafu,

Hongera kwa mada yako.lakini usiwaaminishe watanzania kupitia mtandao na hizo code zinazoonesha level za viwanda vya ndege kuwa sasa kiwanja cha Chato kitakuwa na ubora baada ya kiwanja cha ndege cha Dar na Kilimanjaro.

Pamoja Maelezo mengi ambayo ni hisia hasi kwa utawala wa Rais Magufuli kuhusu huo uwanja wa chato huo uwanja ni muhimu tu kwa matumizi ya Rais akiwa ziara mkoani kwake na hata akiwa mapumziko ni nyumbani kwake. Hilo halina mjadala ndiyo maisha yanavyotakuwa kuwa.

Program ya viwanja vya ndege vingine nchi mzima IPO ktk bajeti ya Wizara ya Ujenzi ktk hatua mbalimbali za utekelezaji. Mfano Dodoma kimeboreshwa sasa na ndege kubwa zinatua sasa,Katavi uwanja ni mzuri sana umejengwa n.k

Naona macho na masikio yote umeyatoa kiwanja cha chato mkoa wa Geita ndiyo kinajengwa hivyo.
 
Asante balafu kwa reports nzuli. Sasa nimeamini kwanini wanamtaka jf CEO adisclose majina harisi ya watoa post.
 
Chato International Airport ni project ya hovyo hovyo iliyo fanywa kwa kumuogopa Rais Magufuli
Mkuu hebu fafanua maana hapa kauli inamaanisha mkuu anajiogopa mwenyewe kwa mantiki kuwa mtu huwezi kwenda hazina kuvuta mabilioni kujenga uwanja wa ndege bila go ahead ya mkuu mwenyewe. Usisingizie raisi anaogopwa kuwa muwazi kuwa raisi kasema.

Basi maarufu la Sabuni linalotoka Mwanza kwenda Chato kujaza abiria huwa ni kazi ngumu sana, nasubiri nione commercial flight ya Dar to Chato au Mwanza - Chato
 
Majungu tu, kwani chato wanakaa nyani? Kwani lazima ndege zote wapande watalii? Hacheni ubwe.ge kwani chato ipo sudan?
Tatizo lenu mmelewa ulevi wa madaraka, kama suala ni kupata upendeleo mngeanza na mambo ya msingi kwenu kama ugonjwa wa mnyauko wa migomba, awasaidie research na suluhisho mngeondokana na njaa kali mliyonayo sasa.

Basi la Sabuni au Lushanga kwenda Chato halijazi abiria nauli chini ya elfu kumi mtajaza ndege nyie? Tumieni upendeleo huu wa raisi kutoka kwenu awasaidie vya maana sio white elephants.

Hakuna mmiliki wa ndege Chato, hakuna kiwanda zaidi ya ginnery ya ushirika, hakuna hata Hotel pale zaidi ya tule tu Lodge tuchafu nani apande ndege kwenda Chato mtukufu akitoka. Mwanakijiji wa Ilyamchele atapanda ndege?
 
Cheza mbali na kilevi kiitwacho madaraka ni kikali sana,kikikukolea unaweza vua nguo hadharani huku ukiamini waliojisitiri ndio wajinga na wapumbavu.
Chato inaenda kuwa mji mkuu wa Tanzania baada ya safari ya kuhamia Dodoma kufifia, watalamu wa viwanja vya soka,mahoteli na NHC wapo busy chato kuangalia jinsi ya kupajenga na kinachofuata ni kutafuta Timu ya soka ikuzwe haraka haraka au inunuliwe Timu yeyote Ligi kuu kisha ihamishiwe Chato na wahakikishe Simba, Yanga, Azam wakitia mguu Chato lazima wafungwe ikibidi hiyo Timu (Chato United) itachukua Ubingwa wa TZ kisha kombe la Kagame pia Champions League ya Africa hayo ndiyo malengo ya Chato.

Mkulu anataka kufikia mwaka 2020 Chato iwe na hadhi ya jiji.
 
Tatizo lenu mmelewa ulevi wa madaraka, kama suala ni kupata upendeleo mngeanza na mambo ya msingi kwenu kama ugonjwa wa mnyauko wa migomba, awasaidie research na suluhisho mngeondokana na njaa kali mliyonayo sasa.

Basi la Sabuni au Lushanga kwenda Chato halijazi abiria nauli chini ya elfu kumi mtajaza ndege nyie? Tumieni upendeleo huu wa raisi kutoka kwenu awasaidie vya maana sio white elephants.

Hakuna mmiliki wa ndege Chato, hakuna kiwanda zaidi ya ginnery ya ushirika, hakuna hata Hotel pale zaidi ya tule tu Lodge tuchafu nani apande ndege kwenda Chato mtukufu akitoka. Mwanakijiji wa Ilyamchele atapanda ndege?
Mkuu Yaani wanataka eti wafanye miujiza wahindi matajiri wote watalazimishwa kujenga hotel Chato, na Nation housing, Veta walalazimishwa wajenge nyumba na Hotel pia NSSF na mashirika mengineyo watalazimishwa kuijenga Chato.

Yaani Chato itajengwa kwa lazima kwa Amri amri bila kupenda.
 
KLM SOON ITATUWA CHATO

OVA
Ikafanye nini kule?

Tatizo la mitanzania ni zile fikra za kimaskini na choyo, mtu yuko radhi apiganie uwanja wa ndege usio na faida yoyote ili mradi tu uko kwao. Viwanja kama Kia, JNIA, Arusha, Mbeya na Mwanza hivi vimeendelea na kuwa vitega uchumi.

Ticket yangu ya ndege kutua Songwe inaonyesha kodi shilingi 13,000- ninaposafiri. Abiria 1,000 wakishukia uwanja mmoja kwa siku shilingi milioni 13 zinaingia na kusaidia kulipa bili, wafanyakazi na gharama zingine za uendeshaji na faida kidogo.

Pia angalia maduka na biashara pale uwanjani. Faida plus plus. Je Chato pale uwanja huo utaingiza hata senti. Nishuke kwenye ndege nikalale Marine Lodge? Jamani jamani jamani Mungu anawaona.

Tunaolalamika hoja yetu ni kuwa kwa sasa nchi yetu bajeti haitoshi tungekuwa na vipaumbele kwa viwanja vyenye uwezekano wa kutatua matatizo ya sasa na kuleta kakipato kidogo, Chato sio kipaumbele.
 
barafu

Mkuu kwani kama ni watalii wa Serengeti ni bora Uwanja wa ndege wa Musoma ukarabatiwe Vizuri kwani upo karibu zaidi na Serengeti kuliko mwanza pia kujenga uwanja wa musoma ni kumuenzi Nyerere na kuongeza mapato ya wasariti toka nchi jirani ya kenya nk.
 
Ikafanye nini kule? Tatizo la mitanzania ni zile fikra za kimaskini na choyo, mtu yuko radhi apiganie uwanja wa ndege usio na faida yoyote ili mradi tu uko kwao.

Viwanja kama Kia, JNIA, Arusha, Mbeya na Mwanza hivi vimeendelea na kuwa vitega uchumi.

Ticket yangu ya ndege kutua Songwe inaonyesha kodi shilingi 13,000- ninaposafiri. Abiria 1,000 wakishukia uwanja mmoja kwa siku shilingi milioni 13 zinaingia na kusaidia kulipa bili, wafanyakazi na gharama zingine za uendeshaji na faida kidogo.

Pia angalia maduka na biashara pale uwanjani. Faida plus plus. Je Chato pale uwanja huo utaingiza hata senti. Nishuke kwenye ndege nikalale Marine Lodge? Jamani jamani jamani Mungu anawaona.

Tunaolalamika hoja yetu ni kuwa kwa sasa nchi yetu bajeti haitoshi tungekuwa na vipaumbele kwa viwanja vyenye uwezekano wa kutatua matatizo ya sasa na kuleta kakipato kidogo, Chato sio kipaumbele.
Mkulu kaamua chato itajengwa hata ikibidi watanzania wale nyasi yy hajali hata KLM ikitokea siku moja ikatua kwa dharula kuchota mafuta watahakikisha TV ,Radio na magazeti wanaitangaza hiyo Habari mpaka Dunia nzima wajue kuwa chato ni Sheli ya ndege za kimataifa zitue kuongeza mafuta watafanya hivyo ili kuwalazimisha wafanyabiashara wakajenge Hotel Chato.
 
Man United, Real Madrid, Barcelona, AC Milan, Paris German, Liverpool nk zote zitaalikwa Chato kucheza Mechi pindi Wajapani wakimaliza kujenga Uwanja wa soka mkubwa kama ule wa malakana kule Brazil.

Vingi vinakuja Chato. Hii itawafundisha watanzania kuwa ni Vizuri kila baada ya miaka mitano wabadili Rais kwani Rais akija mpya toka Songea na yeye atajenga uwanja wa Ndege, soka na mahoteli na barabara songea baadae Rais akitoka Kigoma atajenga Uwanja wa ndege kigoma na barabara ni wakati wa kila mkoa utoe Rais ili style ya kujenga kwao isambae kote Nchini.
 
Katiba mpya ni muhimu sana Utawala wa majimbo unahitajika Tanzania kwani Utawala wa majimbo ndiyo huleta maendeleo kwenye majimbo kutokana na kipato cha jimbo, mfano kule South Africa kila jimbo lina mfalume wake licha na kuwa na Serikali kuu.

Lakini kila jimbo lina asilimia zake za kuendeleza jmbo kabla ya kupeleka mapato Serikali kuu na ukitembea South Africa kila jimbo limejengeka kwa pesa za jimbo si pesa toka Serikali kuu.

Hata kenya sasa wameiga Utawala wa majimbo ambao upo Marekani miaka mingi umesaidia kukuza uchumi na maendeleo kwa kasi huu mfumo wa kuwa na wakuu wa mikoa ni mfumo Analojia sana na umepitwa na wakati kwa Dunia ya sasa.

Tukitaka Tanzania iwe Nchi Tajiri lazima katiba mpya ije na hayo na ifute vyeo vya wakuu wa mikoa kwani hata china nchi ya chama kimoja haina mkuu wa mkoa wanatumia utaratibu mwingine kabsa.
 
Back
Top Bottom