Hatimaye barabara Pamba yaanza kukarabatiwa

ram

Platinum Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
9,345
Reaction score
8,565
Kama wiki moja imepita, tulijiuliza hapa ndani kwamba mmiliki wa hii barabara ya pamba hapa mwanza ni nani, watu tuliongea hapa, kweli barabara ile haifai, barabara ina mahandaki na iko katikati ya mji, hatimaye barabara imeanza kukarabatiwa, imefungwa upande wa kuanzia Kenyatta road hadi hapa bank ya barclays, ngoja tuone itafungwa kwa muda gani na ubora wa hiyo barabara utakavyokuwa

idumulwa, Aaron, kalimizzle, Honey Faith, Super H, charminglady, Marire, Ndeticha
 
Last edited by a moderator:
Sio ajabu sana kwa kipande hicho kifupi kufungwa kwa zaidi ya miezi miwili.
 
Inafumuliwa yote au wana ziba viraka? Ina urefu wa kilometer ngapi.
 
wanaziba viraka, less than 2 km kuania maungio ya Kenyata hadi Tanganyika bus na budget yake inatosha kujenga barabara ya lami yenye urefu wa zaidi ya km 15. chezea green wewe...
 
Kwani tsh. ngapi kwa maana km 15 ni kutoka jengo la ccm mkoa hadi Kisesa.
 
Miezi miwili mbona michache sana mkuu, mwaka jana ilifungwa takribani miezi 9, imefunguliwa hata mwaka haujaisha tangu ianze kufanya kazi mahandaki yakajaa barabarani

Sio ajabu sana kwa kipande hicho kifupi kufungwa kwa zaidi ya miezi miwili.
 
Wametoa lami yote iliyokuwepo...... ila naona mjenzi ni yule yule wa miaka yote, sitashangaa kuona itatumika miezi sita inarudi pale pale

Inafumuliwa yote au wana ziba viraka? Ina urefu wa kilometer ngapi.
 
Miezi miwili mbona michache sana mkuu, mwaka jana ilifungwa takribani miezi 9, imefunguliwa hata mwaka haujaisha tangu ianze kufanya kazi mahandaki yakajaa barabarani

C ndo hayo ya kila mbuzi kula kwa urefu wa kamba yake
 
  • Thanks
Reactions: ram
wanaziba viraka, less than 2 km kuania maungio ya kenyata hadi tanganyika bus na budget yake inatosha kujenga barabara ya lami yenye urefu wa zaidi ya km 15. Chezea green wewe...

ishakuwa mambo ya green tena si mbunge wenu wana kyadema
 
Kama wiki moja imepita, tulijiuliza hapa ndani kwamba mmiliki wa hii barabara ya pamba hapa mwanza ni nani, watu tuliongea hapa, kweli barabara ile haifai, barabara ina mahandaki na iko katikati ya mji, hatimaye barabara imeanza kukarabatiwa, imefungwa upande wa kuanzia Kenyatta road hadi hapa bank ya barclays, ngoja tuone itafungwa kwa muda gani na ubora wa hiyo barabara utakavyokuwa

idumulwa, Aaron, kalimizzle, Honey Faith, Super H, charminglady, Marire, Ndetichia

Mum... Wala hata usiumize kichwa na hiyo barabara, make ni mradi wa watu fulani. Haiwezekani kila mwaka hiyo barabara inatengewa fungu. Et kisa eneo korofi, hivi unaikumbuka barabara ya mabatini ilivyokuwa inatitia enzi hizo? Mbona ile kampuni (jina limenitoka) ilijenga na mpaka leo haina tatizo.

Vipi kuhusu barabara ya Kilimahewa, majaruba barabara nzima mbona ilijengwa na haina tatizo???

Chezeiya miradi ya watu wewe
 
  • Thanks
Reactions: ram
Ile kampuni ilikuwa inaitwa sijui Astad kama sijakosea nadhani

Mum... Wala hata usiumize kichwa na hiyo barabara, make ni mradi wa watu fulani. Haiwezekani kila mwaka hiyo barabara inatengewa fungu. Et kisa eneo korofi, hivi unaikumbuka barabara ya mabatini ilivyokuwa inatitia enzi hizo? Mbona ile kampuni (jina limenitoka) ilijenga na mpaka leo haina tatizo.

Vipi kuhusu barabara ya Kilimahewa, majaruba barabara nzima mbona ilijengwa na haina tatizo???

Chezeiya miradi ya watu wewe
 
Bila shaka wajenzi ni Nyanza Road works.

nyanza road kwa sasa ni kampuni bora sana, aliwachukua wale waitaliano wa astald, na tangu anyimwe tenda na EU baada ya kuona kazi zake mbovu alishakataa kujenga barabara chini ya kiwango yuko radhi kutema mzigo kuliko kujenga chini ya kiwango.
 
Mkuu ile ya kuingia Sahara vp?? Nayo wameiweka kwenye mchakato au mpaka KIN,GU.NGE awe NAIBU WAZIRI WA UJENZI..?
 
Kwa hiyo nyanza road wanajenga barabara zenye viwango?
Ninachojua Mr Pombe anahusika kwenye hii kampuni ndo sababu wanapewa kazi japo kazi zao haziridhishi, hii barabara wanajenga kila mwaka,why? Kma wana ubora unaosema why waijenge hii barabara kila mwaka

nyanza road kwa sasa ni kampuni bora sana, aliwachukua wale waitaliano wa astald, na tangu anyimwe tenda na EU baada ya kuona kazi zake mbovu alishakataa kujenga barabara chini ya kiwango yuko radhi kutema mzigo kuliko kujenga chini ya kiwango.
 
Thubutu.....labda wakimaliza kuijenga hii

Mkuu ile ya kuingia Sahara vp?? Nayo wameiweka kwenye mchakato au mpaka KIN,GU.NGE awe NAIBU WAZIRI WA UJENZI..?
 
Wametoa lami yote iliyokuwepo...... ila naona mjenzi ni yule yule wa miaka yote, sitashangaa kuona itatumika miezi sita inarudi pale pale

Uchaguzi serikali za mitaa umekaribia
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom