Hatimaye aliyeniibia pesa zangu amechomwa moto

Hakuna kitu kinauma kama kuibiwa pesa. yaani mtu unajinyima, unajitesa kuwekeza pesa zako alafu mtu anakuja kuzichukua kirahisi tena anaenda kunywea pombe na kuwapa malaya.

Hawa wahuni walikua wawili waliniotea usiku nimelala fofo (usingizi wa mlevi) wakaniibia laki tisa na elfu thelathini. Kupitia dirishani pesa zilikua kwenye mfuko wa suruali ambayo niliivaa siku hiyo Na suruali yenyewe waliondoka nayo. Hiyo ilikua ni mwaka jana.

Kwa kuwa wahuni wote wa mtaani nawajua tena wengine nilisoma nao nikaona hapa nikienda polisi ni kujisumbua tu. Nikafanya upelelezi mwenyewe mpaka nikawagundua wezi wangu.

Ni madogo wahuni walioshindikana mpaka kwa wazazi wao na mpaka jela washakaa na mda huo pesa yenyewe yote walikua washaimaliza.

Nikaamua kuwapotezea tu lakini niliwalaani sana kwa sababu walinirudisha nyuma sana. Week mbili zilizopita mmoja kati ya wale wa wawili amekufa kifo kibaya sana.

Alichomwa moto na madereva boda boda baada ya kuiba piki piki ya mwenzao. Bado huyu mwingine nae siku zake zinahesabika.
Weka picha zao
 
Dislike
 
Sio wale waliochomwa kwa mathias pale?au wamechomwa kibamba ipi?
Sio hao. Wale walikua wanakaa kwa mathias mitaa ya jamaica. Huyu alikua ni mkaazi wa kibaha maili moja maeneo ya loliondo. Walienda kumuulia kibamba. Sikumbuk ilikua kibamba ipi.
 
sijipongez bali nawapongeza raia na madereva boda boda kwa kupunguza vibaka mtaani.
Bodaboda wananikela kwa tabia zao za kutofata sheria za barabarani ndio mana wengi wanaishia kupata ulemavu wa kudumu ila ktk swala la ulinzi mitaani wamesaidia kwa namna flani. Jamaa wakikamata mwizi chance ya mwizi kupona ni ndogo sana na akipona lazima amrudie mwenyezi mungu. Vijiwe vingi vya bodaboda vimesaidia mitaa kupunguza idadi ya wezi
 
Kwer kabisa mkuu.
 
Duu, Watu wengine mna roho ngumuu, uliachaje Mia 9 inaning'inia kwenye suruali kirahisi rahisi hivyo?

Hiyo pesa unaingia ndani unaihifadhi sehemu salama, hata Paka akikuangalia unaacha kwanza, kati ya wanyama sijawahi kua na imani nao ni Paka.
We jamaa Comments zako, zinaonesha upo talented, Hua nacheka kabla sijasoma..
 
nidanganye ili nipate nin mzee. Sikua na wazo la kuibiwa siku hiyo hiyo pesa ilikua nikaiweke bank kesho yake asubuhi. Wazee wakapita nayo. Jamaa amechomwa moto Kibamba tu hapo. Lakin ni mkazi wa Kibaha maili moja. Kwa wenyeji wa maeneo hayo watakua wamelisikia hilo tukio.
Sijui nikwanini wahujumu uchumi wanaachwatu wazurure na mashangingi
Nao wangewekewa hukumu nzito wangeogopa kupelekwa mahakamani hivyo wasingeiba
 
duh!!..hiyo ni kizamani sana.

kwa nyakati hizi, sehemu salama kwangu ni mifumo ya kidijitali ya kutuma na kupokea pesa. hapa nazungumzia tigopesa,mpesa, airtel money nk.

kama simu yako ipo well secured, hata kama kibaka akaiba, sio rahisi kwake kujua password yako ya tigopesa, mpesa au airtel money.

labda abahatishe tu au awe anashirikiana na watu wa ndani wa kampuni husika ya huduma za simu. na wanaofanya hivi sio vibaka wa mtaani, ni wahalifu wakubwa wenye wanamtandao mpana wa wezi.
Kwa nchi yetu bado utajikuta kuna siku unalazimika kukaa na cash hata kwa usiku mmoja. Wote tunajua sehemu salama ni benki lakini mara moja moja unaweza kujikuta una cash.
 
Sidhani kama ni busara kuweka na picha zao. Ukizingatia huyo mmoja tayar ni marehemu.
Kwa kusoma tu naamini kabisa ulichosimulia ni kweli japo kuna watu wanaona kama ni uongo. Cha muhimu ujifunze. Unapolala usiku kitu chochote cha thamani usiweke sehemu ya wazi amabyo mwizi anaweza ''kuvua'' kwa ndoano kupitia dirishani.
 
Back
Top Bottom