Hatimaye aliyeniibia pesa zangu amechomwa moto

Uswiss

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
765
1,000
Hakuna kitu kinauma kama kuibiwa pesa. yaani mtu unajinyima, unajitesa kuwekeza pesa zako alafu mtu anakuja kuzichukua kirahisi tena anaenda kunywea pombe na kuwapa malaya.

Hawa wahuni walikua wawili waliniotea usiku nimelala fofo (usingizi wa mlevi) wakaniibia laki tisa na elfu thelathini. Kupitia dirishani pesa zilikua kwenye mfuko wa suruali ambayo niliivaa siku hiyo Na suruali yenyewe waliondoka nayo. Hiyo ilikua ni mwaka jana.

Kwa kuwa wahuni wote wa mtaani nawajua tena wengine nilisoma nao nikaona hapa nikienda polisi ni kujisumbua tu. Nikafanya upelelezi mwenyewe mpaka nikawagundua wezi wangu.

Ni madogo wahuni walioshindikana mpaka kwa wazazi wao na mpaka jela washakaa na muda huo pesa yenyewe yote walikua washaimaliza.

Nikaamua kuwapotezea tu lakini niliwalaani sana kwa sababu walinirudisha nyuma sana. Week mbili zilizopita mmoja kati ya wale wa wawili amekufa kifo kibaya sana.

Alichomwa moto na madereva boda boda baada ya kuiba piki piki ya mwenzao. Bado huyu mwingine nae siku zake zinahesabika.
 

reyzzap

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,813
2,000
Duu, Watu wengine mna roho ngumuu, uliachaje Mia 9 inaning'inia kwenye suruali kirahisi rahisi hivyo?

Hiyo pesa unaingia ndani unaihifadhi sehemu salama, hata Paka akikuangalia unaacha kwanza, kati ya wanyama sijawahi kua na imani nao ni Paka.
 

adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
6,174
2,000
kuna machalii flani kipindi cha nyuma walikuwa mapacha walikuwa wanatwa mapachaa!
asee walikuwa wezi wale sijapata kuona afu uboya wao walikuwa wanaiba kitaa.

waliniibia baskeli yangu mpya niliumiaga sana hadi leo nawalaani kaburini

siku hiyo wakaingia kwenye 18 za mzee kigagu

maana walimsafisha nyumba nzima afu watu 2 sijui walikuwa wanaweza vipi kuiba vitu vyote hivyo yaani walikuwa wanakusafisha hata duka zima!! wanakuachia mafi tuu ndani.

huyo mzee kigagu walipomuibia akaenda zake upareni kwao,
aliporudi wale mapachaa wenyewe wakajipeleka kama mbwa kaona chatu!

mzee aliwakata kata vipande vipande km vya mishkaki ndio ukawa mwisho wa pachaa...
 

Uswiss

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
765
1,000
Hii ni chai kabisa. Huwezi kuacha hela nyingi kiasi hicho kwenye suruali. Mimi hata iweje nilishindwa kabisa kutoa wallet au pesa mfukoni Ni Bora hiyo suruali niitupe uvunguni au niiweke chini usawa wa dirisha
nidanganye ili nipate nin mzee. Sikua na wazo la kuibiwa siku hiyo hiyo pesa ilikua nikaiweke bank kesho yake asubuhi. Wazee wakapita nayo. Jamaa amechomwa moto Kibamba tu hapo. Lakin ni mkazi wa Kibaha maili moja. Kwa wenyeji wa maeneo hayo watakua wamelisikia hilo tukio.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom