Uswiss
JF-Expert Member
- Oct 15, 2016
- 842
- 2,160
Hakuna kitu kinauma kama kuibiwa pesa. yaani mtu unajinyima, unajitesa kuwekeza pesa zako alafu mtu anakuja kuzichukua kirahisi tena anaenda kunywea pombe na kuwapa malaya.
Hawa wahuni walikua wawili waliniotea usiku nimelala fofo (usingizi wa mlevi) wakaniibia laki tisa na elfu thelathini. Kupitia dirishani pesa zilikua kwenye mfuko wa suruali ambayo niliivaa siku hiyo Na suruali yenyewe waliondoka nayo. Hiyo ilikua ni mwaka jana.
Kwa kuwa wahuni wote wa mtaani nawajua tena wengine nilisoma nao nikaona hapa nikienda polisi ni kujisumbua tu. Nikafanya upelelezi mwenyewe mpaka nikawagundua wezi wangu.
Ni madogo wahuni walioshindikana mpaka kwa wazazi wao na mpaka jela washakaa na muda huo pesa yenyewe yote walikua washaimaliza.
Nikaamua kuwapotezea tu lakini niliwalaani sana kwa sababu walinirudisha nyuma sana. Week mbili zilizopita mmoja kati ya wale wa wawili amekufa kifo kibaya sana.
Alichomwa moto na madereva boda boda baada ya kuiba piki piki ya mwenzao. Bado huyu mwingine nae siku zake zinahesabika.