Ilimchukua Mwanabalozi wetu ambae pia ni mlezi wa jumuiya ya Watanzania waishio Uigereza(TA UK), mama Mwanaidi Maajar kuonyesha ufundi wake wa Kidiplomasia, Hekima, Busara na Nguvu za ushawishi, Kuwakubalisha zaidi ya Watanzania 200 Kuukubali mfumo wa uchaguzi uliowekwa mbele yao na Kamati maalum (Task Force) na hivyo uchaguzi kufanyika na kuwapata viongozi wa jumuiya hiyo watakaoongoza kwa kipindi cha miaka miwili. Malumbano na Mdahalo mkali vilizuka pale Watanzania walioshiriki wakitegemea hatimae wangepiga kura kuchagua viongozi wao, walipoambiwa kuwa haki hiyo iko kwa Wawakilishi wa Mikoa 12 tu ambayo imetuma timu ya watu 5 kila mkoa. Karibu wapingaji wengi wa mfumo/utaratibu walioyesha kukasirishwa na kutoamini kuwa Kikundi hicho cha watu 60 ndio kingewaamulia Uongozi wao. Pamoja na majibu ya Kamati Maalum kuwa faida ya mfumo huo ni kujenga nguvu za jumuiya kuanzia Chini (Grassroots) Bado hali ilikuwa mbaya kiasi cha kutishia kutowezekana kuwepo kwa uchaguzi.
Ndipo Shujaa wetu alipopanda Mimbari Na kwa ustadi mkubwa
Akalirudisha Jahazi lililokuwa tayari limeenda Mrama katika njia sahihi. (Pongezi mama Mwanaidi) Balozi aliwaasa Watanzani wakubali Mageuzi na wasiwe wapotezaji wakati, kwani kuahirisha uchaguzi huu ni gharama na wakumbuke kuwa uongozi uliokuwepo umeshajiuzulu na kuwa Serekali inawategemea sana katika mradi huu wa Mtu kwao (Dispora) na haitakuwa rahisi kuuendesha ikiwa hamtakuwa na uongzi.
Baada ya hutuba yake ukumbi ulisimama kumpongeza na baada ya hapo mfumo mpya ulitumika kuwapata vingozi na Bw. John Lusingu aliekuwa katibu mkuu wa chombo hicho alichaguliwa kuwa Mwenyekiti. kuna mjumbe mwengine mmoja toka timu ya zamani na wengine wote kumi ni wapya.
Kwa tafsiri yeyote ushindi wa leo ni wa Mh. mama Balozi.