Hatimae mzee kavuta 98m za kiinua mgongo

Kwani hao wa kike sio watoto wake?

Kwenu watoto ni wa kiume pekee wanaorithi?

Vijana wenzangu, tuwatengenezee watoto maisha yao. Hela za kustaafu ziwe zetu, watoto wasizitolee macho.

Kama unazaa zaa tu kama kuku huku hujawawezesha watoto wako ndio wanakuja kua kama huyu anaetegemea mafao ya baba yake aolee.

Tusisahau watoto wa kike pia ni watoto wetu, wana haki ya kurithi mali ya baba yao.
Sasa wakike si ataolewa ataenda kuanzisha mji wa mume wake! Nadhani ndio maana hawapewi kipaumbele sana ila dume la mbegu lazma liendeleze u Bin wa mshua.
 
Wakuu habari zenu Jana
Mzee wangu ni mstaafu alistafu mwezi Wa pili Mwaka huu hivyo 25% haimuhusu sasa Jana salio lake likasoma 98M kwakuwa Mimi ndio mtoto wake kidume wengine wakike imenibidi nisafiri toka dar kwenda mbeya kuhesabu kama ziko sahihi sasa hivi ninatafakari cha kumshauri afanye maana age yake imeenda ana 65 years nyumba anazo mbili sehem tofaut mashamba anayo ng'ombe amefuga boda boda anayo sasa wakuu nisaidieni mawazo awekeze wapi ili angalau asikaukiwe nadhani namimi sasa naweza kuoa maana Mahali imepatikana
Miaka 65 ni mzee au lishe mbovu! Anatakiwa kwanza aoe mke kijana ili mwili urudi na mtafutie kausafiri ka vijana sio bajaji tupa huko.
Kifustacho sasa kinafurahisha, mlete Dar mpangishie Sinza au Kinondoni ili apigwe na taa za mjini, wiki moja atangaa na uzee utakwisha. Ila nakushauri mpe uhuru wake usimbanebane.
Nitajaribu kukutafuta sehemusehemu kwa ushauri zaidi kwa mzee wetu, baba yetu mpendwa na mtu wa watu.
 
Dah, Mkuu natumaini unatania! Yaani salio liliposoma tu mafao ya Mzee wewe ukachukua likizo ya dharura kwenda 'kuzihesabu', wakati ziko Benki?
Unahakiki nini?
Halafu katika Mil 98 ya mafao ya Dingi tayari umeishavuta Mil 20 mkuu!?
Kwa kasi hiyo baada ya miezi 6 tu hiyo hela ni Historia.
fanyeni hivi. muambie mzee avute kama mil 5 aweke ndani kama hela yake ya matumizi ya mwezi mzima akae nyumbani akili itulie akitafuta la kufanya.
hiyo Mil 20 uliyochukua angeweza kuiweka benki kwenye Acc ya muda maalumu ikawa ikamzalishia japo mdogo mdogo wakati akitafuta la kufanya.
nyinyi wengine mnaweza mkapewa tu sadaka ya milioni moja moja, kama hampo wengi, na mkaendelea na maisha yenu ya kawaida ya kila siku.
Msije mkamgeuza mzee wenu Vikoba, kila mwenye kashida kake hata kununua sare ya mwanaye ya shule hahangaiki kivyake kukatatua...bali kiguu na njia kwa Baba!
Mfano mzuri ni wewe mkuu, umeshindwa kutafuta mahari ya kuolea unasubiri fao la dingi kutoa mahari!
Muacheni mzee wenu ajilie kivulini chake alichotolea jasho juani!
My two cent..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom