Mrejesho: Mzee Wangu amepata 98m za mafao yake baada ya kustaafu

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Hatimae mzee kavuta 98m za kiinua mgongo - JamiiForums
Nimesha rudi dar nashukuru kwa mlio nishauri ushauri wenu tumeufanyia kazi kwa kuweka 50M fixed account wakati mzee akifikiria cha kufanya mbeleni 20m nilipewa mie 8m aliwapa Dada zangu watatu Wa gawane hiyo nyingine wanakula taratibu na Bi mkubwa huku 50m iko bank sasa basi nafikiria ninunue Kiwanja goba then nitafute mke nikalipe mahari mambo mengine yatajiseti mbeleni karibuni Leo jioni 40/40 Bima kupunguza stress
 
We jamaa,yaani pesa ya Mzee wako unaanza kuitumia kupunguza stress zako?
Mara unawaza kununulia kiwanja na kuoa kabisa!?

Jiangalie upya,kabla wakati wa majuto haujakufikia,maana naona unapata kiwewe kwa pesa za mzee,ni wakati wako kufikiria namna gani bira ya kufanya pesa hiyo izalishe zaidi na kuanza kumtunza mzee wako,hiyo pesa ni nyingi lakini ni ndogo sanaaa!!!

Badili mawazo na uwe mwangalifu oohoooo!!!
 
Sawa boss tutakuja hapo 40/40 kula mbuzi, tukitoka tuhamie the great!
 
Kuna siku utakuja kuandika thread au Post kinyume kabisa na hizi threads zako 2 .

Ndio maana kuna maneno yanaitwa "ukiwa muongo usiwe msahaulifu"

Mimi nakukumbusha tu usije ukajisahau siku ukapost vingine.
 
Kuna familia wana hasara mtoto Kama wewe si Bora Mzee angefuga ng'ombe apate maziwa una mawazo ya ajabu Sana
Hata mwezi hautaisha utavunja mkataba na Bank uchukue hata hiyo 50m
Na utamuua huyo Mzee mapema
 
........Bwanaeh!kweli mkuu mkumbushe huyu maana hawachelewi kurudi hapa oohh naomba kwa mwenye kazi au kibarua chochote anisaidie nimehangaika mwaka wa pili huu sijapata kazi.

Ukimfuatilia unakuta ameshawahi post vitu kama hivi.
 
We jamaa,yaani pesa ya Mzee wako unaanza kuitumia kupunguza stress zako?
Mara unawaza kununulia kiwanja na kuoa kabisa!?

Jiangalie upya,kabla wakati wa majuto haujakufikia,maana naona unapata kiwewe kwa pesa za mzee,ni wakati wako kufikiria namna gani bira ya kufanya pesa hiyo izalishe zaidi na kuanza kumtunza mzee wako,hiyo pesa ni nyingi lakini ni ndogo sanaaa!!!

Badili mawazo na uwe mwangalifu oohoooo!!!
Zilikuwa za mzee zilipokuwa mikononi mwake saivi ni zangu maana zipo mikononi mwangu
 
Kuna siku utakuja kuandika thread au Post kinyume kabisa na hizi threads zako 2 .

Ndio maana kuna maneno yanaitwa "ukiwa muongo usiwe msahaulifu"

Mimi nakukumbusha tu usije ukajisahau siku ukapost vingine.
Nitapost maana cm yangu bando langu
 
Kuna familia wana hasara mtoto Kama wewe si Bora Mzee angefuga ng'ombe apate maziwa una mawazo ya ajabu Sana
Hata mwezi hautaisha utavunja mkataba na Bank uchukue hata hiyo 50m
Na utamuua huyo Mzee mapema
Ng'ombe wapo na maziwa anapata
 
Wazo zuri. Tafuta kiwanja cha bei nafuu Chanika cha M4, M 10, anza ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu, milioni moja kula bata, milioni tano, za kuolea.
Ukienda Goba, milioni zote 20 zitaishia kwenye kiwanja alafu utakuwa unaenda kukisalimia kila siku kama kinaumwa vile.
Mind you, tofali elfu nne zinazogharimu M4.5 zinatosha kumaliza nyumba ndogo Chanika. Hizo 5.5 ukizipeleka kwenye material, nyumba inaweza kufika kwenye lenta.
 
Back
Top Bottom