Hatimae mswada wa mafao ya vigogo wapita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimae mswada wa mafao ya vigogo wapita

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdulahsaf, Mar 29, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Posted on March 28, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]
  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza majumuisho ya mswada huo...

  Hatimae wajumbe wa baraza la wawakilishi leo walipitisha kwa sauti moja mswada wa sheria wa maslahi ya viongozi wa kisiasa baada ya mswada huo kukataliwa kupitishwa mara mbili na wajumbe hao. Mswada huo ambao ulijadiliwa kwa hamasa kubwa ndani na nje ya baraza la wawakilishi una lengo la kuweka utaratibu wa kuwalipa maslahi viongozi baada ya kustaafu.
  Kupitishwa kwa mswada huo ambao hatua inayofuata ni rais wa Zanzibar kuutia saini na kuwa sheria kamili umetokana na serikali kusalim amri kwa madai ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kukosoa baadhi ya vipengele vya mswada huo. Baadhi ya vipengele ambavyo serikali imevifanyia marekebisho ni pamoja na kufutwa kwa kifungu kilichokuwa kinazungumzia maslahi kwa washauri wa rais pamoja na watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wa viongozi wa juu kuhudumiwa na serikali baada ya viongozi hao kustaafu.

  Kipengele chengine ni kile kinachohusiana na utaratibu wa ulipaji wa maslahi kwa viongozi wote bila ya kubagua pamoja na kukubaliana kwamba muda uliowasilishwa mswada huo haukuwa mwafaka. Wakati wa kujadili mswada huo wajumbe wengi akiwemo Mwakilishi wa Kitope (CCM) Makame Mshimba Mbarouk na Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu kwa pamoja walikosoa msawada huo kwa kusema kuwa serikali inajitwika majukumu yasio na lazima wakati wananchi wengi pamoja an wafanyakazi wa serikali wakikabiliwa na maisha magumu.

  Katika mswada huo rais mstaafu, makamu wa rais, spika wa baraza la wawakilishi, mawaziri, manaibu mawaziri, mwanasheria mkuu na wajumbe wa baraza la wawakilishi watalipwa maslahi mazuri baada ya kustaafu hata hivyo waziri wa nchi afisi ya rais, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini hakuweka bayana malipo hayo.

  Kwa mujibu wa mapendekezo ndani ya mswada huo ni kwamba rais mstaafu atakuwa na wasaidizi wa nyumbani, makatibu wasaidizi, walinzi na madereva ambao wote watalipwa na serikali kama livo sasa lakini kwa kuongezewa viwango vya maslahi yao.
  Akifanya majumuisho kabloa ya wajumbe kupitisha mswada huo waziri Dk Makame alisema kwamba lengo la serikali la kuleta mswada huo ni kutoa heshima kwa viongozi na kuhakikisha kwamba wanaishi vizuri baada ya kutumikia taifa lao. Dk Makame alisema kwamba serikali haina nia ya kuwabagua watumishi wake na kwamba washauri wa rais na watoto ambao wameondolewa katika amrekesbisho ya mswada watafanyiwa utaratibu maalumu wa kulipwa maslahi yao.

  Spika wa baraza la wawakilishi, Pandu Ameir Kificho alisema baada ya wajumbe kupitisha mswada kwamba wananchi na wajumbe wa baraza hilo wamesaidia katika marekebsisho ya mswada huo kutokana na maoni yao kuzingatiwa na serikali. Kwa mara ya kwanza mswada huo uliwasilishwa mwezi Octoba mwaka jana amabpo serikali ililazimika kuuondoa baada ya wajumbe wengi wasiokuwa mawaziri (Backbenchers) kupinga kwa nguvu mswada huo kutokana na kuwa haujazingatia hali halisi ya uchumi wa Zanzibar.

  Lakini mswada huo ukarejeshwa tena kwa mara ya pili mwezi Januari mwaka huu na kujadiliwa kwa kina huku serikali ikiahidi kufanyia marekebisho baadhi ya vifungu ambavyo vilionekana vina mapungufu wajumbe hao. Makamo wa pili wa rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd alisema kwamba serikali haijakusudia kupotosha wananchi kutokana na mswada huo na kulaumu baadhi ya wananchi na vyombo vya habari kwa kuzidisha kutia chumvi.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Mbona hatuoni mahesabu
   
 3. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  hii nchi tumeshakuwa malimbukeni kwa viongozi. Yaani watoto uzae wewe, hawafanyi kazi,hufanyi kazi aafu walipwe kwa kodi zetu!! Ci bora wawape hayo mafao bora watumishi ambao bado wapo kazini! Hii nchi inabidi tuchinjane kidogo ili katiba isimamishwe na hizi sheria zote zifutwe tuanze upya. Siku si nyingi watanganyika nao watakuja na huo muswada.
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Yaani mibunge inakaa kujadili kuboresha, narudia "kuboresha" mafao (ambayo bado ni bora kupindukia) ya viongozi wakati wananchi wako hoi bin taabani!!!!!! kweli mkuu bora tuchinjane huu sasa ungese!!!
   
 5. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Itasaidia kuondoa ufisadi?
   
 6. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wapeleke muswada mwingine wa Utumishi....!
  Pindi kiongozi akiwa kama mtumishi wa umma akalitia hasara taifa au kuingia mikataba mibovu, waweke vifungu vya adhabu na isiwe chini ya miaka 40 jela mpaka kifungo cha maisha. haya maboresho yalitakiwa yaendane na adhabu sio wao wafurahie maisha, sisi tufurahie umaskini.

  Sie tukulipe vizuri, ili ututumikie vizuri ukiharibu basi tukuhadhibu
   
Loading...