Elections 2010 Hatima ya Tanzania na ya Vyama Mbadala Baada ya Uchaguzi 2010

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
6,716
2,000
kufuatia matokeo ya uchaguzi 2010, ambapo inaelekea kuchachuliwa kwa namna mbali mbali hivyo kupotosha utashi na matumaini wa watanzania, hofu ya watu /yangu ni hatima ya vyama vya upinzani, pamoja na hatima ya tanzania kama nchi, kwani walioshinda ni "si watanzania bali mafisadi" ambao wana nguvu ya kipesa na pia wana tumia vyombo vya dola kugandamiza demokrasia, na tatizo hili linajionyesha kuwa kubwa zaidi, toka zama zile za kuwachoma vibaka/kibaka/jambazi nk. Sasa zama hizi ni za mafisadi na serikali iliyo kuwepo/zilizo pita zimeshindwa kuwachukulia hatua stahili mafisadi iwe kwa kuwa na nasaba nao au kutokana na uzembe wa serikali zetu au kutokuwepo na nia ya kupambana na huo ufisadi,, njia iliyo baki kwa wananchi ilikuwa ni kwa kufanya kampeni na uchaguzi katika hali iliyo sawa na serikali iliyopo madarakani, lakini bahati mbaya imeonekana njia hiyo nayo ni ngumu, kwa watu kuitumia kuonyesha kupinga kwao ufisadi, sasa tatizo linalo kuja hapo baadae , nalo linaweza kuwa ni watu kujichukulia sheria mkononi, ndipo hapo ninapo kuwa na mashaka ya baadae ya tanzania ya leo yenye "amani", la pili ni kuwepo kwa vyama mbadala kwani kwa mafisadi kuwa wame neemeka na utawala/tawala zilizo pita wanazidi kujikita zaidi na zaidi katika siasa na uchumi wa nchi hii, hivyo kuwanyima nafasi watu wengine au vyama mbadala, matokeo hali hii haimpi mtu yoyote yule matumaini kwa tanzania ijayo, kwani wahenga walisema kama huwezi kupigana nao basi jiunge nao, wapo walio amua kijiunga nao kama hatua za kupunguza makali ya maisha na wapo ambao hawata jiunga nao. je watachukua hatua gani ili kujikomboa?
 

Mwafrika

JF-Expert Member
Nov 20, 2006
5,490
0
ccm wanapanda chuki mbaya sana dhidi yao. Vijana wengi Tanzania hawana kazi. Vijana wengi Tanzania wana maisha magumu sana. Vijana wengi Tanzania walimuunga mkono Dr Slaa na wabunge wengi wa upinzani.

CCM walichofanya, ni kupanda chuki ya kudumu ndani ya mioyo ya hawa vijana. SIku wakikosa mtu mwenye busara wa kuwaongoza (kama Dr Slaa), basi ccm wajue kuwa hakuna risasi au mabomu yatakayotosha kuwatuliza vijana hawa.
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,478
2,000
2015 vyama vingi vya mafisadi vitaundwa ili kura zigawanyike na CCM washinde tena
Kuna haja wapinzani wakaungana
 

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
6,716
2,000
2015 vyama vingi vya mafisadi vitaundwa ili kura zigawanyike na CCM washinde tena
Kuna haja wapinzani wakaungana
kuungana ni kugumu maana vyama vingi ni vya watu binafsi, na vile vya jumuiya, sera zao hazikubaliani, mfano cuf iliundwa zaidi ikiwa na agenda za visiwani, kuwepo bara ni kutokana na sheria ina taka hivyo na sasa kuna madai ya ndoa na ccm, chadema agenda yao ni ya huku bara na udp, lakini leo hii mzee mapesa kaachana na hiyo agenda naona yupo kwenye agenda yake binafsi, nccr nayo sio ile ya mwanzo, labda sasa hivi wamepata fundisho, na hiyo tlp waamue kuungana na chadema, na wakati huo huo serikali inatakiwa ibadili sheria kuruhu vyama kuungana na wagombea uraisi wakipata kura asilimia fulani waruhusiwe kuingia bungeni
 

MartinDavid

JF-Expert Member
May 22, 2009
875
225
Chadema tutajipanga na kujenga chama kuanzia kata, wilaya, mkoa na taifa..

CCM kitaendelea kufa taratibu mpaka kufika 2015 kitakuwa kimekwisha...
 

Membensamba

Senior Member
Nov 4, 2010
157
170
Nadhani kinachotakiwa ni kuita kikao makini cha wataalamu wa mambo na wanachama makini na wote wanaoitakia mema Tz kwa lengo la kufanya "situation analysis" na ku-come-up na strategy kabambe ya jinsi ya kujenga mtandao utakaomfikia kila mtanzania, na kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa mabadiliko na siasa makini. Pia ni muhimu kujenga mfumo utakaohakikisha kuwa uchaguzi ujao unafanyika kwa haki, ikiwa ni pamoja na kushinikiza iundwe tume huru na inayowajibika, pamoja na kuwaandaa wanachama na wananchi kudhibiti uchakachuaji wa kura.

Ukiangalia utaona kuwa maeneo yote walikompigia kura Slaa ni kule ambako kiasi fulani watu wamepata kuamka kisiasa, kule ambako bado matokeo ni tofauti. Hivyo elimu si muhimu tu bali ni lazima. Kazi ya ukombozi wa kifikra sio ndogo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom