HATIMA YA POGBA CARRINGTON JIJINI MANCHESTER

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
*Manchester United inajiandaa kumuuza Pogba!?*

Kwa akili ya kawaida unaweza ukaonekana mwehu unaposema Manchester United imeanza kujiandaa kuishi bila kiungo wake ghali muite Poul Pogba.

Ni ukweli ulio wazi kwa msimu huu Pogba ndani ya Man United amekuwa hana mchango mkubwa na pia ameshindwa kuisaidia timu yake kufikia malengo ya ndani ya uwanja.

Na muda mwingi kwa msimu huu ameutumia akiwa juu ya vitanda vya matibabu akiuguza hili kisha likipona hili ujue litafuata lile. Kwa ufupi Pogba msimu huu anaongoza ligi ya wachezaji majeruhi wa Man United kuliko Phil Jones.

Na muda mwingi amekuwa ni kama kirusi ndani ya United si mara moja ama mara mbili bila hofu wala heshima juu ya mashabiki na klabu yake inayomlipa mshahara kila mwisho wa juma amekuwa akiongea wazi mbele ya wana habari kuwa anatamani kuondoka Man United.

Na wakala wake jasusi katika dili za kuamisha wachezaji Mino Raiola amekuwa akimtumia ama akimuendesha Pogba ili aweze kufanikisha dili la kumpeleka Real Madrid, PSG ama Juventus ili na yeye achukue ujira wake.

Hakuna siri kama Poul Pogba akiweka kando 'maungwadu gwadu' yake bado ni mchezaji wa kiwango cha juu ambae anaweza kuingia kikosi cha kwanza kwa vilabu vikubwa vingi kama sio vyote.

Mshindi wa medali ya Kombe la dunia pale nchini Urusi akiwa na Ufaransa ni kama amekinai kuvaa jezi ya Man United. Na hilo sio la kuuliza hata lugha yake ya mwili inaongea mengi hasi juu ya Man United.

Nafikri aioni future nzuri ya Man United chini ya Mr Ole. Nafikiri ni Edd Woodward na Ole ndio wanadam pekee ndani ya United wanaomuamini Poul Pogba. Lakini mashabiki wao tayari wameanza kumfuta vichwani mwao.

Wana ridhishwa na Fred pamoja na Mac Tominay wakicheza pamoja kuliko akiwepo Pogba. Na kwa usajili waliofanya wa Bruno Fernandez kutoka Sporting Lisbon ya Ureno nafikiri watakuwa tayari kuishawishi bodi, Mr Ole na Woodward wamuuze Pogba mwisho wa msimu ili waweze kupata pesa ya kuendelea kukisuka kikosi chao.

Kelele za Pogba kwa mashabiki wa United zimeendelea kufifia kwakuwa wamegundua sio mwenzao na wamekuwa wakiudhiwa na jinsi anavyokubali kuendeshwa kibiashara na wakala wake Mino Raiola.

Pogba akiuzwa me sitashangaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom