Hatima ya CCJ kesho


Status
Not open for further replies.
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
13
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 13 0
Kutoka Tanzania Daima

HATIMA ya usajili wa muda wa Chama Cha Jamii (CCJ), ambacho Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, amekuwa akikipiga chenga, inatarajiwa kujulikana kesho katika mkutano kati yake na viongozi wa chama hicho.

CCJ, chama ambacho kimesababisha mtikisiko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimekuwa kikipigwa kalenda na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa karibu miezi miwili sasa tangu kuwasilisha maombi yao ya usajili wa muda Januari 20, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya msajili, Tendwa ambaye amekuwa safarini Arusha na kuingia ofisini jana, amepanga kukutana na viongozi wa CCJ kesho ofisini kwake.

Wakati Tendwa akiwa kwenye mtihani mzito wa kukipa usajili wa muda chama hicho, viongozi wa CCJ; Katibu Mkuu Renatus Muabhi na Mwenyekiti wake, Richard Kayabo, kwa nyakati tofauti, waliliambia Tanzania Daima Jumatano jana kwamba wamekamilisha taratibu zote za usajili.

"Sisi tunamsubiri msajili, sijui atatupa visingizio gani tena, hatuna kitu kingine tunachodaiwa maana kila kitu anajua yeye... tutamsikiliza, lakini tunachohitaji sasa ni usajili wa chama chetu, tumeshakaa vya kutosha," alisema Kayabo.

Hata hivyo habari zaidi ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, zinadai kuwa CCJ kimekamilisha mambo mengi ya msingi ikiwa ni pamoja na kuweka sahihi za wanasheria katika baadhi ya nyaraka pamoja na kukabidhi bendera ya chama hicho katika ofisi ya msajili.

Habari zaidi zinasema kuwa hatua iliyofikiwa sasa na CCJ inamuweka katika wakati mgumu Tendwa kukisajili chama hicho kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CCM wanaotaka kisipewe usajili.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, kadi za CCJ zimekaa muundo sawa na kadi ndogo ya kuchukulia fedha kwenye mashine maalumu za benki maarufu kama ATM huku kwa nyuma zikiwa na picha ya Mwalimu Nyerere, tofauti na nyingine ambazo ni kubwa kama za CCM.

Duru za kisiasa zinauangalia ujio wa CCJ kama tishio kwa CCM na Rais Jakaya Kikwete, kutokana na kutajwa kuhusisha vigogo wa chama hicho tawala ambao wanataka kujitenga na kugombea urais Oktoba mwaka huu.

Tayari Spika wa Bunge Samuel Sitta, aliwahi kusema kwamba haoni tatizo la kusajiliwa CCJ, huku pia akisema hawezi kuzuia watu kumuhusisha na chama hicho kama mgombea hapo Oktoba. CCJ imekuwa ikitikisa nchi tangu taarifa zake kuchapishwa kwenye vyombo vya habari, kwani kuna majina makubwa yanatajwa kuwemo akiwemo Spika Sitta, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, John Malecela. Lakini wote wamekanusha.
 
PJ

PJ

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
297
Likes
2
Points
35
PJ

PJ

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
297 2 35
Tendwa alishaagizwa asikisajili mwaka hivyo lazima afuate masharti ya waajiri wake.
 
Kituko

Kituko

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2009
Messages
9,557
Likes
7,455
Points
280
Kituko

Kituko

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2009
9,557 7,455 280
kinaweza kuwa chama kizuri, lakini wajaribu zaidi kuangalia matatizo yaliyopo ndani ya nchi kuliko kurudi sana nyuma na kufuata kila kitu cha Nyerere, anyway baadhi ya mambo ya Nyerere yalikuwa madhuri lakini wasikiweke hicho chama kama ni TANU au CCM nyingine
najua mtu kama SALIMU, WARIOBA, BUTIKU, MAKWETA na wengineo wao ni Nyererelism lakini inawapasa kukijenga hicho chama kufuatana na upepo wa sasa wa kisiasa
 
Jayfour_King

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Messages
1,141
Likes
12
Points
0
Jayfour_King

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2009
1,141 12 0
Yetu macho na masikio kwani kesho sio mbali.
 
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Messages
10,407
Likes
5,803
Points
280
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2008
10,407 5,803 280
Kama mzalendooo....halisi akisajili aachane na siasa za uoga
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,251,904
Members 481,940
Posts 29,789,806