Hatima ya Air Tanzania

Full 8

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
313
271
IMG_20170404_160510.jpg
IMG_20170404_160452.jpg

Niliwahi kusoma juu ya hujuma za shirika la ndege la Afrika kusini kwa air Tanzania na ilivyopelekea kulidumaza kwa kuuza ndege zilizokuwepo kama chakavu na kuimalisha za kwao katika ardhi yetu.

Wote tumeshuhudia namna shirika letu la ndege lilivyokua dhaifu kabla ya kuja bombardier mbili hivi karibuni limeonekana kujitutumua kidogo.
Lakini hii ya kuruhusu shirika la ndege la Ethiopian airline kufanya kazi hapa nchini kutapelekea kifo kingine cha shirika hilo.
Wahusika sijui wamejipangaje!
 
Kuwa msemaji na muamuzi wa kila kitu wewe mwenyewe mwisho lazima tu utaharibu, sijui alifikiri au aliongea tu kutaka kupigiwa makofi?
 
Kwn ni kosa kupanua wigo wa kibiaahara,imeshaonekana shirika letu peke yake haliwezi kutosheleza majukumu yake,sio mbaya na mashirika mengine kufanyakazi hapa ili mradi kutakuwa na manufaa kw taifa
 
SASA PANGABOI TANGU LINI IKASHINDANA NA BOEING AU AIRBUS ZA KISASA ZENYE HADHI YA DUNIA??
 
SASA PANGABOI TANGU LINI IKASHINDANA NA BOEING AU AIRBUS ZA KISASA ZENYE HADHI YA DUNIA??
Ndiyo haziwezi lakini kwa kuwa tumeamua kuimarisha shirika letu la ndege ambalo bado linatambaa halijaweza kusimama lenyewe na kuhimili ushindani wa mashirika makubwa, nilidhani si sawa kumruhusu Ethiopian air kuleta huo ushindani.
 
Tunajua kung'ang'ania madaraka tu!!!
Mwandishi wa makala hiyo ya Daily news anasema kumpa Ethiopian air ruksa kufanya hivyo ni sawa na kumpa plot jirani yako ajenge nyumba kwa kuwa tu mwanao hawezi kujenga.
 
Mwandishi wa makala hiyo ya Daily news anasema kumpa Ethiopian air ruksa kufanya hivyo ni sawa na kumpa plot jirani yako ajenge nyumba kwa kuwa tu mwanao hawezi kujenga.
Namuunga mkono mwandishi, nawe umefanya la maana kuifahamisha hadhira mtandaoni.
 
Back
Top Bottom