Hati za mashamba 5 makubwa zafutwa Tanga

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania Mheshimiwa Dr. John Pombe Magufuli amefuta hati za mashamba matano makubwa yaliyokuwa na hati za miaka 99 chini ya umiliki wa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ambayo yamebainika kuwa hayaendelezwi na kusababisha baadhi ya wananchi kuathirika kwa kukosa maeneo ya kilimo katika maeneo hayo.

Akizungumza jijini Tanga na kamati ya ulinzi na usalama mkoa kisha baadae kusikiliza kero na malalamiko ya waathirika zaidi ya 600 waliokuwa wamekusanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Tanga kueleza kero ikiwemo kunyang'anywa maeneo yao ya ardhi kisha kupewa wawekezaji, waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Mheshimiwa William Lukuvi amesema baadhi ya waliopewa mashamba hayo wamefanya kuwa ndio biashara ya kwenda kuchukua mikopo benki na kwenda kuwekeza maeneo mengine.

Waziri Lukuvi amemuagiza mkuu wa mkoa wa Tanga kupitia kamati yake aliyounda ya kuchunguza migogoro ya ardhi kisha kumpelekea taarifa, ianze ukaguzi wa mashamba 13 waliyohodhi baadhi ya wafanyabaishara katika wilaya nne za mkoa wa Tanga kisha mkuu wa mkoa kumueleza adha wanayokabiliana nayo wananchi hasa katika migogoro ya ardhi ambayo hivi sasa imeanza kuchukua sura mpya.

Hatua hiyo inafuatia waziri Lukuvi kwenda kuzungumza na waathirika wa migogoro ya ardhi katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga ambapo diwani wa kata ya Maweni Bwana Joseph Gervas kumueleza waziri Lukuvi kuwa wananchi wa kata hiyo wapatao 280 wameathirika.

Baada ya watendaji wa ardhi katika jiji la Tanga kuuza maeneo yao wanayomiliki kisheria hatua ambayo imeanza kuleta viashiria vya uvunjifu wa amani


Chanzo: ITV
 
Last edited by a moderator:
Hii nchi watu wanaiba sana. Utachukuaje mkopo halafu ukafanya kazi isiyo stahili mkopo?
 
Back
Top Bottom