"Hate tranquility, move forward"

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Messages
2,385
Points
2,000

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2015
2,385 2,000
Igweeeeeeee Wanazengo!!!!!!

Jioni hii kulikuwa na shida sana ya usafiri. Wakati nimetoka kazini pale posta mpya kulikuwa na idadi kubwa sana ya watu wakingoja magari.

Nikaamua kuto kusubiria gari hapo, nikazid kutembea direction ya kuelekea kariakoo. Ghafla nikakutana na bajaji inaelekea gerezani nikapanda, haijapita dakika 10 nikajikuta kariakoo gerezani.

Destination yangu ni kufika Kimara, kukawa pia pale kariakoo kuna uhaba wa magari na watu ni wengi wanasubir kwenye kituo na kuna foleni pia ya magari.

Nikaamua kama mwanzo kutembea mbele nikielekea direction ya Karume, ile nafika Karume inatokea gari tupu inaelekea Makumbusho kupitia mabibo. Nikaingia ndani ya gari, kama dakika tano foleni inaruhusiwa.

Njia ya Mabibo haina foleni, dakika kama kumi na tano nimeshafika shekilango tayar.

Ile kushuka tu nakutana na gari ya moja kwa moja Kimara ambayo haikuchukua mda mrefu kufika kwenye destination yangu.

FUNZO NILILOPATA LEO

1) Daima songa mbele kwenye visions zako. Hata pale mazingira yanapokuwa magumu kiasi gani wewe songa mbele tu. Unaposonga mbele unapanua wigo wa kupata fursa nyingi ambazo zitafanya ndoto zako kutimia.

2) Unapofuata ndoto zako, usiangalie watu wa pembeni yako wanafanya nini. Wewe as long as umeshafanya plan zako just move forward. Mfano kwa case yangu, pale posta nikakutana na staff mwenzangu akaniambia "leo kiboko, mvua imetukomesha sijui nitafika nyumbani saa ngap" Yaani yeye ameshakata tamaa ya kufika nyumbani lakini mimi kichwani nasema inawezekana na kweli nimefanikisha. Ningesema nimsikilize nisingekuwa nime move popote na likely ningekuwa naye tu tunasubiria gari.

3) Usitafute sababu za excuse, wakati natembea kufika karume kulikuwa na kama dalili ya mvua. Ingekuwa mtu mwingine angesema .. "aaaah mi ngoja tu nisubir gar kituoni, hii mvua kama itaanguka mda si mrefu.. Yaani ni kama mtu unatafuta excuse ya kwanini hufanyi kitu fulani ambacho kitainua maisha yako.. .... NO EXCUSES!!!


Ni hayo tu Wanazengo.

Kwa hisani ya mvua ya leo..
 

Forum statistics

Threads 1,366,351
Members 521,454
Posts 33,367,612
Top