Hatari ya kutafuta mume au mke kwenye mtandao

Man Mudi

Senior Member
Oct 13, 2014
159
113
1-Mume mwenye mke hudanganya kua hana mke.

2-Mume hudanganya anavitu asivyo navyo.

3-Wasichana wenye watoto hudanganya hawana watoto.

4- Wanawake wengi na hata waume hupenda kupunguza umri wao na kujifanya wadogo.

5- Wengi hueka picha au kutumiana picha za zamani alipo kua kijana tofauti alivyo sasa.

6-Wengine hueka picha au kutumiana picha za mtu mwengine .

7- Wengine ni wake za watu ila hudanganya kua waliachwa na waume hudanganya wameachana na wake zao.

8-Wenye roho mbaya hujifanya na roho nzuri.

9-Wengi pia hujifanya wachamungu ilhali sivyo walivyo huko waliko.

10-Wengi huahidiana kuowana ila mmoja akiwa mkweli mwengine hua na ahadi ya uongo.

❗❗❗❗❗❗❗❗❗❗

Msiba mkubwa huu ndugu zangu yani mtindo sasa ni kila mmoja ni bachelor hana mume wala asie mke wala asie mtoto kila mmoja anatafuta mke mwema na mume mwema ila ni hadaa tupu.

Tahadharini sana ndugu zangu tusipurupuke tu kujiamulia mambo mazito kama haya bila kufuatilia kupata uhakika kwani uaminifu umetoweka zama hini wengi wanaishia kula mbovu.
 
Suala za Umri mimi naona halina mashiko...Age are just numbers labda iwe tofauti kubwa sana mbayo itaonekana
Kuhusu kuwa na mtoto...mbona kuna makabila kadhaa ku date mwenye mtoto ndio dili kwao?
Hayo ya Roho mbaya au wacha mungu hata ukidate mtaani ni hivyohivyo
Sasa hao wake za watu au waume za watu wanaojifanya hawana wenzi...hata siwaelewi???hao watakuwa limbukeni
Binafsi naona bado kuna nafasi ya kupata mwenza kwenye mtandao kwani wapo watu wengi wazuri tu...tatizo hawajapata au mwenza walio pangiwa na mungu hayupo maeneo yao...
La msingi ni kuacha kukurupuka...
Fanya uchunguzi wa kina na bila kuwa na haraka sana....
Unaweza kuwa na maswali ya mtego...na kuja kuyarudia kwa ujanja baada ya muda...
Mwongo ni mwongo tu utamjua....
 
Inamaana ndoa zote ambazo mume na wake wanadanganyana walikutana kwenye mitandao ya kijamii?
Siyo ndoa zote ambazo watu hukutana mitandaon hudanganya bali mimi nimesema nyingi wengi huwa si waaminifu
 
kweli mkuu upo sawa.
Wengi wako hivyo ila kuna wachache ndio wapo serious.
Message delivered
 
Yah, ni kweli wengine wanafanikiwa kama wote watakuwa ni waaminifu ila wengine huwa hawafanikiwi kwa sababu huwa si wakweli na wawazi
 
Yoote uliyoandika ni kweli, ila kupata mke kupitia mtandao inawezekana
Yah, ni kweli wengine wanafanikiwa kama wote watakuwa ni waaminifu ila wengine huwa hawafanikiwi kwa sababu huwa si wakweli na wawazi
 
Yoote uliyoandika ni kweli, ila kupata mke kupitia mtandao inawezekana
Yah, ni kweli wengine wanafanikiwa kama wote watakuwa ni waaminifu ila wengine huwa hawafanikiwi kwa sababu huwa si wakweli na wawazi
 
Back
Top Bottom