Hatari,Vodacom M-PESA si salama

Hatari,Vodacom M-PESA si salama

dah, kumbe ni wengi nilifikiri nikopeke yangu yaani hawa jamaa wa voda sijui
vipi. Hata miminaambiwa nisichoke kupiga simu na mpaka sasa nimepiga zaidi ya mara 20
kudai shilingi 38,000 tu ambazo zilienda kwa wakala mwingine

hata miminashangaa kwani sikuandika namba ya huyo wakala sijui imekujaje tena dakika 2
baada ya tatizo hilo nilipiga simu lakini hawakunisaidia yaani toka tarehe 22/6/13 mpaka leo
hawataki kurudisha na ushahidi ni huu hapa chini.
R98zy852 imethibitishwa tarehe 22/6/13 saa 9:36pm
toa tsh38,000 kutoka 859138 - esmail athumani
shabani salio lako jipya la mpesa ni tsh700.

Jamaa hawana msaada kabisa ni wasumbufu sana na
nina wasiwasi ni wezi ndio maana jina haliji mpaka pesa
iwe imetumwa tofauti na tigo ambao linakuja jina kwanza

vodacom wapo makini bwana.mbona mi nlipata tatizo kama lako wakarudisha baada ya dk 5
 
Aisee hivi vichwa vyenu vya habari vya kutisha ni hukohuko kwa shigongo, kumbe makosa ni ya kwako mwenyewe, jiangalie bwana..
 
Kwanza nakupa pole. Naamini ulitumia namba yao ya M-PESA customer service (15366) kuripoti tatizo lako. Maswali yangu ni je, walikupa reference namba ya tatizo lako? Kwanini wakwambie usiache kupiga simu wakati umesharipoti tatizo?Nasema hivyo kwani nimeshawahi kupata tatizo kama hilo lako na baada ya kuripoti nikapewa reference namba ambayo nilitakiwa niitume kwenda namba 100 yakipita masaa 24 bila hela yangu kurudi tangu nilipo ripoti tatizo lakini sikuambiwa nipige simu. Niliipata hela yangu baada ya masaa kama 40 hivi. Kwa msaada zaidi nakushauri ufike ofisi ya Voda iliyo karibu nina uhakika watakusaidia.
 
Ukikosea pesa ukapiga simu ikiwa yule ulomtumia kimakosa hajatoa basi hurudishwa. Ila kama umekosea Na upande Wa Pili MTU katoa basi unaambiwa uendelee kupiga simu ili akiweka wakutudishie pesa yako.usitegemee kurudishiwa hela kama part b hana hana hela.
 
Voda wapo vizuri sana kwa upande wa M-pesa.Mi nashangaa watu mnapolalamika kuhusu ku-comfirm namba.EE iko hivi unapotuma M-pesa inakuambia bonyeza 1 kudhibitisha,ama 2 kubatilisha sasa wapi mbayaaa???aaa simseme tu hamuelewi mueleweshwe.
 
dawa ni kuwaibukia ofisini kwao, wote mnalalamika lakini sijaona hata mmoja amesema alifika ofisini kwao ku-claim, na kama hakieleweki unawapa mtiti wa ukweli, wakati mwingine kupiga simu tu haitoshi. anyway labda mpo mbali sana na ofisi za vodakom zilipo.
 
wewe ni wale wahuni mlioko jf hapa watu wana discuss idea hata kama huyu alikosea,ni muhimu kwa wahusika wasaidie haraka kurecover hiyo pesa. pili wengine wametoa suggestion mzuri kuweka mechanism itakayosaidia kupunguza error kama vile tigo, wewe unaleta mambo ya chooni,hivi vidigrii vya kugushi matatiizo kwelikweli
Na siku ukilewa ukalala choooni badala ya chumbani kwako uje uwalaumu vodacom hapa
 
Hawana mana,ukiwapigia wanakujibu ujinga.Niliwahi watukana wakanifungia line yangu ilibidi niwe mpole.Hata hivyo nilishukuru kwakua line yangu ilikuwa na tatizo lakununua muda wamaongezi toka M-pesa ,baada yakufunguliwa ikaanza kufanya kazi kama kawa.
 
Ni huduma hatari sana hasa pale unapokosea kutoa pesa ikaenda kwa wakala au namba nyingine. Nashangaa kwa hili lililonitokea nilikuwa natoa pesa kwa wakala hapa Songea lakini pesa imeenda kwa wakala ambaye yuko Shinyanga. Mpaka leo nafanya kazi ya kupiga simu fedha hazirudishwi naishia kukatwa 100 tu na hizo 150,000 hazirudi halafu sio mimi tu nimekutana na watu wawilia ambao wanadai mpaka wamechoka.
likuw

ilitokea kwangu nikawahi kupiga simu vodacom,wakazirudisha. Wewe ilikuaje? Pole sana, nenda vodacom wakala atakusaidia au piga simu customer care watakusaidia
 
nami pia ni mhanga wa hili.
toka tarehe 15/02/2013 hadi leo sijapata 60,000/= zangu nilizozitoa kwa kupewa namba isiyo sahihi na wakala.
pamoja na kupiga simu saaaana,niliishia kuambiwa msumbufu na kashfa mbalimbali kutoka kwa wahudumu wa vodacom.
kama tcra watapita humu basi watupe njia ya kuyapeleka malalamiko ya wateja (walaji) panapostahili.
huu unaweza kuwa wizi wa design mpya.
 
MTU anapotoa pesa kwa bahati mbaya ikaenda kwa wakala mwingine kwa kweli vodacom hawawezi kukurudishia pesa yako hadi wakukutanishe na wakala husika ili haki itendeke. Lakini endapo utakosea namba pesa ikaenda kwa MTU mwingine then hapo wanaweza kukurudishia. Alma kuhudu customer Ukiona wamekufokea basi ujue wamekuelewesha Sana ukawa huelewi. Lakini wao wana sheria Moja kuwa akiongea na wewe lazima ataje jina lake ili Kama hujaridhika unaweza kushtaki mbele. Leo Voda wameleta charges Mpya kwa waliotoa pesa na hili wamefanya bila kutoa matangazo yyt huu ni wizi na hapa wametuibia
 
Tunaomba yyt mwenye namba ya wakubwa WA Voda atusaiidie ili tukiwa na shida turned mbele
 
Mimi nimeshatumiwa pesa ndogo lakini mara mbili pesa zinakataa kutoka mara ya mwisho nilikwenda mpaka Vodacom Mlimani City, nilichokiona ni siasa tu.

Bado sijapata tatizo nikituma mimi pesa, kuna kamchezo kanaendelea kuna watu ipo siku watakwenda jela wait n see.

Pia ningeshauri msitumie kabisa simu banking hizi za kuunganisha na M pesa mtakuja kulia, na mjiepushe kuweka password za miaka yenu ya kuzaliwa. msije mkasema sijaawambia.
 
Inawezekana hamjamuelewa mtoa mada mimi niliandika namba ya wakala na nikaihakikisha
mara tatu lakini hela imeenda kwa wakala mwingine. Nikapiga simu nikaambiwa sistim ilisumbua
hela itarudi hii ni wiki ya tatu sasa sijapata hela yangu nimeamua kuivunja hiyo laini yangu ya
Voda kwani nilimkuta mtu mwingine ana malalamiko kama yangu.
VODA MPESA NI WEZI
 
ni kama vile umetuma pesa kwa mtu kimakosa then yule mtu akazitoa je vodacom ndo wanatakiwa wakulipe au. Nijuavyo mimi wataifunga account ya aliyetoa mpaka siku akiweka ela au kutumiwa ndo utarudishiwa sawasawa na ulivyotoa kwa wakala kimakosa.napenda sana utaratibu wa tigo kwene kutoa au kutuma ela kabla hujaconfirm wanakuuliza jina la unaemtumia au jina la wakala unayetoa
 
Kwenye transaction zote zinazohusisha fedha kwa njia ya electronic LAZIMA kuwe na mechanism ya 1. Kumsaidia mteja asifanye makosa rahisi katika transaction 2. Ku-recover fedha zake iwapo itatokea akakosea transaction. Hi ni kazi ya yule mtoa huduma eg vodacom na hawezi kusema ni uzembe wako! Record zote zipo kwanini ishindikane?

Na zaidi ya hapo mkuu, huwa nahoji hivi ni sheria zipi zinasimamia uendeshaji wa hizi huduma za M-Pesa, Tigo pesa airtel money, easypesa n.k? Nachojua mabenki, maduka ya kubadilishia pesa yana sheria na taratibu zake ila sijafaham hizi huduma serikali inautaratibu gani? Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom