Hatari:Shule yavamiwa na sungusungu.

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
271
Habari nilizozipokea majira ya jioni nikuwa kundi la sungusungu wapatao70 wameivamia shule ya sekondari ya Ukenyenge iliyopo wilayani Kishapu Shinyanga na kuzua tafrani na hofu kubwa kwa wanafunzi,walimu na wakazi wa eneo hilo.Binafsi ningefurahi kusikia uchunguzi wa kina unafanyika ili kubaini chanzo cha tatizo kwakuwa imeonekana raia wana mtazamo hasi na taasisi hiyo. Binafs kwakuwa eneo hilo ninawatu nafahamiana nao hivyo nikadodosa,inasemekana chanzo ni ndama ambaye alikamatwa kwakuingia eneo la taasisi hiyo ya serikali,ndama alishikiliwa kwamuda wa mwezi mzima pasipo mwenyewe kufika kumchukuapamoja na matangazo kutolewa kwa wanafunzi.j3 mmiliki alifika na kuamrisha walimu wampatie maliyake bila masharti yoyote huku akiwatukana kuwa hawana akili kwavile walitaka kumtoza faini. Mfanyabiashara huyo ambaye anasadikika alikuwaamejiandaa kwa mapambano aliendelea kufoka na kutaka ndama huyo maramoja aachiwe. Walimu waligoma na kuamua kwenda mahakamani kumshtaki kwa kuwadhalilisha napia kuingiza kinyume cha sheria mifugo katika eneo la shule. Mfanyabiashara huyo wa ng'ombe yeye aliamua kwenda serikali ya kijiji na sungusungu ambapo aliwadanganya kuwa ng'ombe huyo walimu walimwiba na kumhifadhi shuleni hapo.j4 jioni sungusungu wakakusanywa nakuambiwa na kiongozi wao waende wakamchukue ndama,walimu wakakataa ila wakawaambia kwakuwa mmekuja kumchukua basi mchukueni,wakati huo wanafunzi waliokuwa kwenye maandalizi yamahafal j5 wakaanza kupiga miluz wakiashilia kuwashambulia endapo wangethubutu. Ratiba yote ikavurugika na hata shule ya msingi iliyojirani iliathirika kwani msafara wa kelele ulipita katikati ya shule nakufanya vipindi visite.Ni muhimu uchunguz wa kina ufanyike na sheria zitazamwe ili taasis na watumishi waheshimiwe kwani hapo walimu ilikuwa manusura washambuliwe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom