KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,759
- 39,496
Habari wakuu.
Jana mwanajamii mwenzenu ilibaki kidogo tu ni rest in peace kutoka kwa wananchi wenye hasira Kali. Ilikuwa kwenye daladala...kama mnavyojua wana JF usafiri wa umma tabu zake hasa nyakati za asubuhi.
Basi baada ya daladala kuingia kituoni watu tukaanza kugombania..hatimaye nikafanikiwa kuingia..lakini sikufanikiwa kupata siti....nilisimama na mdada Fulani hivi pembeni yangu huku akiwa amening'iniza mkoba wake upande Wangu..wakati tunaendelea na safari na hizi barabara zetu zilizo kwenye marekebisho. Ule mkoba ukawa unaning'inia kuniegemea mimi.
Sasa kuna mtu alikuwa anashuka kituo kinachofuata ikanilazimu kusogea mbele kidogo ili kumpisha mshukaji..kwa bahati mbaya wakati nampisha Yule mshukaji mabega yetu yakawa kama yanauvuta ule mkoba wa yule dada.
Kasheshe likaanzia hapo baada kunihisi mimi ndiye niliyekuwa nauvuta ule mkoba kwa makusudio ya kuiba..akaanza kunipigia makelele ya wizi.
Jambo ambalo liliwapa hamaki abiria wengine wakaanza kunishambulia hadi konda alipoanza kunitetea kwa kuwa alilishuhudia. Na ukijumlisha na personality ...abiria wakaanza kunielewa kwamba sikuwa mwizi.
Ikanibidi nishukie kituo kinachofuata ili kuondoa nuksi...duh..kweli si kila anayekufa kwa wizi basi kaiba kweli..wengine wanasingiziwa tu...tuweni tunaposhambulia wezi.