Hatari: Nimeacha kutumia Nyama

Wamasai tunakula nyama asubuhi, mchana na jioni....saa nyingine hata tikikurupuka kukojoa usiku tunaenda kutafuta nyama kabla ya kurudi kitandani kuendelea na usingizi.
 
Mungu alisema " tutawale viumbe vyote na tuvitumie kama chakula " unapingana na Mungu ?
 
Acha uongo. Unaikimbia nyama au protein?
Kama suala la protein hujakwepa kitu.
 
Umejitahid kusoma lakn sehem zingn umebugi na kweny udaktar hakun kukisia mfan, ini halitengenezi insulin, nilivoona ivyo nikaacha kusoma !!
 
Bandiko zuri sana. Umeniongezea kitu .

Nimepata baadhi ya majibu ya maswali niliyouliza kwenye Uzi wangu wa "Nataka Kuwa Vegetarian ......"

Hongera mkuu
 
Wanga haufai..nyama hazifai...mboga mboga hazifai kwa sababu zinalomwa kwa madawa mengi...khaaaa..sasa tule nini
 
Kwa hiyo hutakufa siyo?
 
yaani nimekuelewa sana,natangaza kuacha nyama,lakini inahitaji uwe shujaa.
 
Mie naona katoa somo zuri! Halafu Kuna suala la msingi Ni SISI wasomaji kukubali au kumkatalia. Hata makanisani, misikitini na imani zingine SI wanakemea dhambi! Lakini watu HAWAACHI sasa Ni jukumu letu sisi tuliomsoma!

MWISHO; Mimi binafsi siachi nyama pamoja na supu yake!
Sasa nikipata bia zangu mbili, NICHOMESHE KABICHI AU MCHICHA? Baada ya bia mbili lazima kanyama ka kuchoma kawepo!😁
 
Reactions: etb
Ukisimuliwa ubaya wa kila chakula hakika unaweza kufa njaa, naacha kula kule kinachonidhuru direct tu
 

ukifatilia sana unaweza kujikita unaishi peke yako na hupo uchi kichakani.maana kila utakacho kisikiliza utaishi kama wale waafrika weusi wapo kisiwa cha india
 
Vyuma vimekaza watu wanatafuta sababu ukimuona na mafurushi ya mchicha kila siku aseme nyama ni sumu. Magu safi sana wanyonge sasa michicha yetu sasa ina wateja.
Hata mimi nashangaa, ukifuatilia historia unakuta mababu zetu huko nyuma chakula chao kikuu kilikuwa ni matunda na nyama nalikuwa wanadunda tu
 
Ningeamini kama ungezisema hizo tafiti watu tukarejea/tukazisoma. Haitoshi kutumia neno "tafiti" peke yake. Andika kulingana na utafiti uliofanyika ...... (nani alifanya na kuchapisha matokeo ya utafiti huo?) vinginevyo hujanishawishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…