Huo ndio uwajibikaji ndugu yangu. Ni vizuri sana kuwa makini na afya zetu na za watu walioko chini ya himaya/uangalizi wetu. Mazingira tunayoishi yana hatari nyingi kwetu na kwa jamii zetu. Hatari ziko za kibayolojia (utapiamlo, sumu uharibifu wa mazingira,vijidudu vya magonjwa nk), ziko physical risks (ajali mbalimbali kama moto, umeme, magari), na hatari kwenye social environment (kama mijibaba inayoweza kuzengea binti zetu, uharibifu wa maadili nk). Mizigo yote hii tunatupiwa wazazi tukabiliane nayo katika kulinda uzao wetu na kuhakikisha afya zao. Kazi ngumu hii!
Nazidi kukutakia heri katika juhudi za kujikinga na majanga hayo