Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 5,602
- 6,381
Nimejaribu kusoma andiko lililiochapishwa na shirika la Afya Duniani lililochapishwa tarehe 4/4/2020 likitoa maelekezo juu ya janga la COVID-19 na Tuberculosis (TB).
Andiko hili linasisitiza Serikali kutoacha kudhibiti Ugonjwa wa TB unaoenezwa na bacteria na kuathiri mfumo wa upumuaji kwa sababu huenda waathirika wa ugonjwa wa TB kuwa hatarini zaidi ikiwa hawatajikinga vyema dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.
Ikumbukwe uenezwaji wa uenezwaji wa ugonjwa wa TB unakaribiana sana na huu wa COVID-19 ila tofauti ni muda wa uatamiaji (incubation period) ambapo Virusi wansoeneza ugonjwa wa COVID-19 hutumia muda mfupi kuatamiwa ila bacteria wanaoweza ugonjwa wa TB hutumia muda mrefu kidogo kuatamiwa.
Mtu anapokuwa na magonjwa yote haya mawili yanayoshambulia mfumo wa upumuaji huwa kwenye hatari kubwa zaidi.Hivyo ni muhimu sana kwa Serikali kuendeleza jitihada za kupambana na ugonjwa COVID-19 huku ukiendelea kudhibiti ugonjwa wa TB.
My take: Wataalamu wa Afya, Serikali, Asasi za kiraia, waraghibishi,watu binafsi, asasi nyingine mbalimbali wanapaswa siyo kutoa elimu ya kujikinga na ugonjwa wa COVID-19 tu ila kujikinga na magonjwa mengine hatarishi kama TB,Ukimwi n.k katika kipindi hiki ambacho janga la COVID-19 limeshika kasi.
Pamoja na elimu ya kujikinga bado jamii yetu inapaswa kupewa elimu ya kujihami ili kupunguza unyanyapaa" social stigma" wa waathirika wa waginjwa wa maradhi hayo kwa sababu jamii isipopewa elimu itakayowasaidia juu ya kujihami wanapokuwa na wagonjwa unyanyapaa wa kijamii unaweza kuwa janga jingine ndani ya janga lililopo.
Watu kuhofia unyanyapaa wanaweza wakaeneza zaidi maradhi kutokana na kunificha na kutokwenda kwenye vituo vya Afya na hivyo kueneza zaidi ugonjwa huu hatari.
Kwa kuwa tayari vyombo vyenye mamlska vimeshabaini kuwa ugonjwa wa COVID-19 umeshafikia katia ngazi ya jamii na maambukizi ya ndani kwa ndani ni vyema matangazo yanayotolewa yatoe elimu bora ya kuiamsha jamii kujihami na kutonyanyapaa waathirika wa maradhi haya hatarishi katika kipindi hiki.
Kumbuka kuwa salama kwa kufuata maelekezo yote ya wataalamu wa afya na Serikali, usisahau kuwa yapo maradhi mengine pia mathalani UKIMWI bado nao unaua.Jilinde mlinde na mwenzako.
Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania.