Hataki relationship anataka situationship (story ni ndefu)

Hataki relationship anataka situationship (story ni ndefu)

Tembomtata

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
266
Reaction score
427
Writing for someone..
Mwaka jana mwezi wa sita aliajiriwa dada mmoja mzuriiiiii ofisini kwetu, kama ilivyo kawaida kwenye sehemu nyingi zenye ma bachelor na ma bachelorete, watu tulianza kumtolea macho. Vijana wakaanza kutupa karata zikawa zinachomolewa baadae yule dada akatolewa kwenye teller akahamishiwa kwenye kitengo niliko mimi. Boss wetu akawa anatupa kazi pamoja mara nyingi tuwe tunashirikiana tukawa karibu sana tukawa marafiki, Sikumoja akawa ananiomba ushauri kwamba bwana ake ameenda kusoma US na inavyoonyesha jamaa yupo ashapata mwanamke mwingine kule na akanionyesha chat kwamba jamaa ana mwambia waachane. Baada ya kama wiki demu akawa yuko stressed sana ofisini kila kazi ananiachia, nikaona sio sawa nikamwambia inakuwa je hataki kufanya kazi akanieleza kwamba wameachana na bwana ake so hayuko sawa nikamwambia anatakiwa atenganishe mambo ya kazi na mambo ya mahusiano ili maisha yaendelee kweli baada ya siku mbili tatu akarudi akawa sawa.

Mimi kuona jamaa ameacha mtoto nikaona ndo fursa lakini nikasema asinione papara ngoja nimpe kama miezi mitatu, in between nikawa na mpa care zakutosha. Siku moja nikamwomba tutoke hiyo ni mwezi wa kwanza mwaka huu kwenye outing nikampiga sound duh ikawa suprise sana kwake, akaniambia haitawezekana anaona kama this time anataka achukue muda wakujiassess akiingia kwenye mahusiano awe commited alipo niambia hivyo wala sikubembeleza na kiburi changu tena nikamwambia wala usiwaze sana.

Tukio la Kwanza

Baadae demu akapunguza mazoea tukawa marafiki tu kawaida na mimi nikapotezea, mwezi wa 3 nimekaa zangu Brajec akanipigia mhhh nilivyoona simu yake nikahisi labda ana shida nikapokea anakaniuliza niliko nikamwambia akaomba niende kwake Mikocheni nikamuuliza kuna nin akaniambia niende, sikukataa wito nikaenda zangu nikamkuta yuko na mdogo wake wa kike akaniomba nimtoe out for a drink. Nikamwambia yaani unanitoa brajec kujakukufuata nikutoe out siungeniambia nikutumie Bajaj, aka apologise tukatoka tukaenda Mbalamwezi tumekaa ikafika mida kama saa 1 siku hiyo kulikuwa na nyama choma festival tukaenda, tumekaa almost mpaka saa 8 usiku. Akaniambia nimrudishe kwao Mikocheni. Kufika akawa anampigia mdogo wake simu hapokei, kampigia kama mara 5, tumekaa pale almost half an hour nikamwambia mimi niko mwenyewe nyumbani ts better twende then nitamrudisha asubuhi akakataa katakata ah na mimi iliasione na njaa sana ya ile kitu nikamwambia pale Sayansi kuna hoteli nyingi basi tukaenda mpaka pale kuna Hoteli moja inaitwa Grand Royal kufika imejaa nikamwambia tutazunguka sana halafu tutapoteza muda wakati mimi nina nyumba akakaa kimya ah alivyokaa kimya mi nikapiga gia mpaka nyumbani kwangu Sinza kumekucha. Tukafika nikamwonyesha chumba cha kulala akaingia kulala mimi chap nikapiga maji naingia kwenye kitanda kuna kagiza flani naona yupo na kyupi tu dah nikakaza roho kama kwa nusu saa hivi mwishowe nikaanza kumzingua akawa hataki baadae akaachia mwenyewe nikapiga, tukalala kama mpaka saa 4 akaamka akasema anataka kwenda kwao. Basi nikamrudisha nikarudizangu gheto kulala.

baada ya hapo akawa anazingua kweli, ofisini haongei yupo tu wala hataki mazoea na mim na mimi simbembelezi

Tukio la Pili

Ijumaa moja tumemaliza kazi tukatoka mpaka samaki samaki na wafanya kazi wengine, siku hiyo anafuraha kweli, tumekaa mpaka mida ya 3 usiku mimi nikaaga. Nimefika kwenye gari nataka kuondoka ikaingia message mbona hujaniaga vizuri? Nikamwita kwenye gari nikamuuliza nikuagaje vizuri akaniambia alitaka nimuage in person badala ya group. Nikamtania nikamwambia kama vipi twende home akaniangalia kwa ukali then akaniambia nimsubiri akaenda kuchukua hand bag akaja kiutani utani tukaenda catalunya nikachukua chakula haooo mpaka home nikagonga vitu haswa akachoka kweli kweli. Asubuhi nimeamka nimekuta amevaa tshirt yangu akaniambia thanks I have really enjoyed sikujibu. Akasema kama kawaida anataka kurudishwa kwao….

Tukio la tatu

Baada ya tukio la pili akaendelea na mambo yake ya kupotezea baadae akahamishwa kutoka tawi la mlimani city akahamishiwa tawi la UDSM, sasa jana kanipigia akaniambia kuna harusi anataka jumamosi twende wote nimemkatalia nimemwambia siwezi kwenda akaniuliza kwanini nikamwambia mimi naende kwenye harusi kama nani akacheka akakata simu…..

Changamoto ni kuwa nashindwa kudecide what to do? Should I move on ama nimkomalie? Lakini sasa kumbuka unakaribia mwaka sasa haeleweki……..
 
Anaonekana alikuwa na matarajio makubwa saana kwa mshkaji wake wa State. Kumwacha imemuumiza na matarajio yake haamini kama ndiyo yameyeyuka.

Bado haja-move kwa jamaa yupo katikati mguu mmoja kwako mwingine unamatarajio jamaa wa state atarudi kana kwamba jamaa akijirudi tu binti asogeze mguu mmoja tu....

Kuwa makini unaweza kuumizwa wewe... nawe kuwa kama yeye mguu mmoja nje mwingine ndani.... maana kwa maelezo yako hayafurahii mahusiano yenu, haji-proud wala kuonyesha nje yupo na wewe.

BtW, kama umempenda unaweza kumbadilisha kisaikolojia taratibu ataelewa somo.....
 
No strings attached.... Kina wanapenda hiyo lifestyle
 
Its difficult for me to tell labda wwe uniambie unaona je?......Inawezekana anataka huduma mahusiano hataki
She is playing a game...hataki committment au hakutaki wewe pia.
Sasa fanya hivi hutokuja kujuta ila utamuweka yeye kwenye position ya kukutaka na kukulilia wewe...piga mzigo,afu uwe unampotezea pia tafuta mtu ili huyu asikufanye ufall awe option B kama wewe alivyokufanya.
Huenda ana mtu wake hapa hapa Bongo.Kajua umeshampenda.
 
Talk to her about rooting your relationship so deeply
And not juu juu
Kindly and soften language should be used ataelewa
Mind you she psychological woman is not normal so make you you don't add more pain to her brain
She need guidance & counseling
By professional psychologist.
PM when necessary.
 
Inavyoonekana kila mmoja wenu ana lengo na matarajio tofauti juu ya uhusiano uliopo., ukaribu wenu unasababishwa na Mazingira ya kazi, Upweke & tamaa za kimwili otherwise baadae haionekani kuwa njema sana..,
 
I think she is totally interested in you two dating, but she is just being " extra";Si unajua mambo ya watoto wadogo, wengi wao wananadhani getting into a relationship without putting up a fight means they'll look cheap or perhaps ni wale wanao believe a man loves you as much as anavyo kusotea so lazima akupime na hizo mbwembwe
 
Mi nadhani huyo mwanamke hayupo series na wewe. Situation uliyopo ni mbaya sana na inaweza ikawa mbaya zaidi kwako if you dont do something about it. Unachoweza kufanya ni kukaa na kuongea naye, umueleze jinsi unavyojisikia kuhusu yeye na yeye akueleze anavyofeel kuhusu wewe, na kama yupo tayari kujicommit kwako. Zaidi ya hapo, atakusumbua mno huyo mkuu
 
NIMESHA MJUA [emoji23][emoji23][emoji23] kama ndio huyo nimjuaye kaka piga tu, huyo ndivyo alivyo,,,,,,, KISEBUSEBU NA KIROHO PAPO[emoji23][emoji23][emoji23]
Nilijua tu watu wa bank mlimani city mta nyoosheana vidole setting is totally differen ingawa ni mtu wa bank..... yeye akisoma ataelewa lakini sio mwingine
 
Yaani bado hujampachika mimba moja matata kbs ile ambayo haiwezi kuwa aborted? unachelewa sana
 
Back
Top Bottom