Hata wenye Range Rover huvitamani vi Baby Walker

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,636
Reaction score
2,731
Binadam ni mtu wa ajabu sana. Utakuta hata wale wenye mi Rengi Rover na Mi VX Kilimo kwanza wanatole macho ki Vitz! Eti kina rangi nzuri, mwingine mi nimependa rim zake...
Ndivyo ilivyo hata kwenye mahusiano. Utakuta mtu ana mke mzurri, lakini bado anachepuka na 'li mwanamke' ambalo huwezi kabisa kulinganisha na yule mkewe...
Ni kwa nini binadam huwa hatutosheki na wingi au uzuri wa vile tulivyo navyo?
 
Tungekuwa tunatosheka maendeleo yasingekuja duniani.

Marekani ana reserve ya mafuta lakini kila siku anazunguka duniani kuzidi kukusanya.

Billgates ana utajiri kuliko GDP ya Tanzania lakini bado anafanya kazi ili ziongezeke.

Nkurunziza amesha tawala vya kutosha lakini anazidi kuongeza kipindi kingine kidikteta.

Mayweather ameshinda mataji ya kutosha lakini anazidi kupigana ashinde zaidi na zaidi.

Ni hulka ya binadamu kutotosheka, vitu vipya vinavumbuliwa kila siku. Changamoto zinachukua nafasi kila asubuhi ukiamka. Usiridhike na ulichonacho, kazana songa mbele.

Ukiona umeridhika ujue wewe ni masikini, na utakufa masikini.
 
Mkuu bili yako leta hapa tafadhali! !
 
Wanakuwa wanataka kujaribu ili kuona upande wa pili kukoje?.
 
nina v8 nitamani vits?????
mengine ni kujitia moyo tu na kujifariji nawewe umo....
 
Utajiri wa kwanza na ulio mkubwa kwa mwanadamu ni afya...wapo watu waliofirisika wakipigania afya zao...wapo watu walioahidi kutoa sehemu ya mali zao kwa ajili ya kupigania afya zao....wapo watu waliolala vitandani wakipigania pumzi zao huku wakiwa wamepaki magari yao ya kifahari mpaka yanashika vumbi.....wapo watu pamoja na kuwa na uwezo wa kula wakitakiacho lakini wanalazimika kula vyakula maalumu kwa ajili ya afya zao....wapo watu ambao kila siku wanalazimika kudungwa sindano moja kwa ajili ya kupigania uhai wao...DUNIA NI ZAIDI YA UINAVYO.........
 
Hii ya kuchepuka sawa.
Ila ya v8 kutamani vits hapana.

Naamini una simu laki nane,umeishawahi kuifikiria itel ya elfu hamsini eti sababu ina rangi ya blue!!!:-$
 
Binadam ni mtu wa ajabu sana. Utakuta hata wale wenye mi Rengi Rover na Mi VX Kilimo kwanza wanatole macho ki Vitz! Eti kina rangi nzuri, mwingine mi nimependa rim zake...
Ndivyo ilivyo hata kwenye mahusiano. Utakuta mtu ana mke mzurri, lakini bado anachepuka na 'li mwanamke' ambalo huwezi kabisa kulinganisha na yule mkewe...
Ni kwa nini binadam huwa hatutosheki na wingi au uzuri wa vile tulivyo navyo?

Kwenye Gari umesema uongo,mwenye Range rover hawezi kutamani vits au passo hata siku moja.

Kwa mwanamke ni kweli kabisa kwa sababu unaweza kua na mwanamke mzuri ila akawa na tabia mbaya,majibu mabaya,kauli mbaya,maringo,majivuno kwa uzuri wake na wanaume tunataka mwanamke myenyekevu na msikivu,mwenye heshima na muelewa sasa ukivikosa hivyo kwa mkeo hata awe mzuri namna gani utavitafuta kwa alienavyo haijalishi ana sura mbaya kiasi gani.
 
Kuzungumzia Range Rover na Vita ilikua anajenga utangulizi wa filamu Maudhui ni Tamaa ya vidogo wakati una vikubwa.
Una mke/dem mkaliii na Hana kasoro ila unamchepukia mke/dem wa jirani au house girl
 
Kuwa na rangerover na kutamani kama vits ni sawa tu, kwa kuwa kila gari lina matumizi yake kutokana na mazingira si kwamba utalitumia rangerover kila safari na kila siku. Na utakuwa mtu wa ajabu sana umiliki range halafu usiwe hata na gari nyingine hata ya kawaida tu.Tofauti nj mke ukiwa na mke kutamani mwanamke mwingine ni tatizo, lakini gari waweza kuwa nazo kulingana na uwezo wako
 
Kuwa na rangerover na kutamani kama vits ni sawa tu, kwa kuwa kila gari lina matumizi yake kutokana na mazingira si kwamba utalitumia rangerover kila safari na kila siku. Na utakuwa mtu wa ajabu sana umiliki range halafu usiwe hata na gari nyingine hata ya kawaida tu.Tofauti nj mke ukiwa na mke kutamani mwanamke mwingine ni tatizo, lakini gari waweza kuwa nazo kulingana na uwezo wako
 
Binadam ni mtu wa ajabu sana. Utakuta hata wale wenye mi Rengi Rover na Mi VX Kilimo kwanza wanatole macho ki Vitz! Eti kina rangi nzuri, mwingine mi nimependa rim zake...
Ndivyo ilivyo hata kwenye mahusiano. Utakuta mtu ana mke mzurri, lakini bado anachepuka na 'li mwanamke' ambalo huwezi kabisa kulinganisha na yule mkewe...
Ni kwa nini binadam huwa hatutosheki na wingi au uzuri wa vile tulivyo navyo?

kumbuka makassy aliimba, ooh jamani mwanadamu hatosheki hata ukimpa nini milele hataridhika
 
Tungekuwa tunatosheka maendeleo yasingekuja duniani.

Marekani ana reserve ya mafuta lakini kila siku anazunguka duniani kuzidi kukusanya.

Billgates ana utajiri kuliko GDP ya Tanzania lakini bado anafanya kazi ili ziongezeke.

Nkurunziza amesha tawala vya kutosha lakini anazidi kuongeza kipindi kingine kidikteta.

Mayweather ameshinda mataji ya kutosha lakini anazidi kupigana ashinde zaidi na zaidi.

Ni hulka ya binadamu kutotosheka, vitu vipya vinavumbuliwa kila siku. Changamoto zinachukua nafasi kila asubuhi ukiamka. Usiridhike na ulichonacho, kazana songa mbele.

Ukiona umeridhika ujue wewe ni masikini, na utakufa masikini.
na mimi naongezea hapo kwa nkurunziza,CCM imeitawala tanzania zaidi ya miaka 50,lakini mpaka leo viongozi wa chama hicho wanapambana usiku na mchana kuhakikisha chama hicho kinaendelea kutawala kwa miaka mingi zaidi na zaidi.
 
Back
Top Bottom